Mshangao: Wanafunzi wa shule moja ya msingi wote wamechaguliwa secondari moja

muhala.jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
746
Reaction score
655
Leo nilikutana na bwana mdogo mmoja akaniomba nitazamie shule aliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza.

Cha ajabu nikakuta wanafunzi wote 230+ wamechaguliwa kwenda secondary moja yani ni kama kuhamisha shule nzima kwend secondary moja.

Je hii imenifanya nitafakari Sana namna selection zilivyofanyika au wote walichagua io shule.
 
Shule ya Sekondari ipo kwenye kata yao hao wanafunzi wa shule ya msingi, unataka wakasome wapi? Waanze kuijaza shule yao ya kata kwanza kabla ya wageni. Kama kijana hataridhika kubaki shule hiyo anaweza kuhama, mzazi au mzazi wake kama anajimudu apelekwe shule ya binafsi
 
Umesoma primary ukafanya kitu ukawa unataniwa , ila unajip moyo nikienda sec haya yataisha mara sec ni watu wale wale eneo ndio tofauti, unaendelea kutaniwa au kuonewa.
Ukiingia sekondari inabidi ubadilishe mtazamo, kaza msuli soma kama hautasoma tena! Wanataniwa watu wengi mno.

Ukizidiwa piga ngumi ya shingo atakayenyenyua mdomo kukutania.
 
Leo nilikutana na bwana mdogo mmoja akaniomba nitazamie shule aliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza.

Cha ajabu nikakuta wanafunzi wote 230+ wamechaguliwa kwenda secondary moja yani ni kama kuhamisha shule nzima kwend secondary moja.

Je hii imenifanya nitafakari Sana namna selection zilivyofanyika au wote walichagua io shule.
hii ni common sana kwa miaka hii, kama miaka 5+ hivi trend ni hii wakienda mbali sana ni shule mbili au tatu. na kama kuna vipanga wachache kwenye hilo darasa wao wataenda zile special
 
Sisi wengine hatuna nguvu ya kupigana mkuu.😔
Unavizia unampatia kwenzi ya kichwa! Ukitoka hapo unakimbilia kwa mwalimu mkali kush'taki, huko unaanza kulia kama dakika mbili kisha unatiririka kuhusu kutaniwa. Unamwambia mwalimu kwamba umepata "Anguko la kihisia"
 
Tunaua vipaji vingi kwa kuwanyima vijana wetu fursa yakwenda kuishi maeneo mengine na jamii zingine.

Nafikiri 40% ya wahitimu wa msingi wanatakiwa wakasome shule.za bweni mikoa mingine.

Hii ingetusaidia sana kama taifa.
Wamechaguliwa watoto wachache walioonyesha kitu cha ziada katika ufaulu wao! Kwa wale ambao wana uwezo wa akili wa kawaida nao wamepewa nafasi ya kukaa pamoja mpaka pale watakapoanza kujishtukia na kupiga msuli.
 
Unavizia unampatia kwenzi ya kichwa! Ukitoka hapo unakimbilia kwa mwalimu mkali kush'taki, huko unaanza kulia kama dakika mbili kisha unatiririka kuhusu kutaniwa. Unamwambia mwalimu kwamba umepata "Anguko la kihisia"
Hii mbinu nzuri ila watanivizia tukitoka shule njiani
 
Leo nilikutana na bwana mdogo mmoja akaniomba nitazamie shule aliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza.

Cha ajabu nikakuta wanafunzi wote 230+ wamechaguliwa kwenda secondary moja yani ni kama kuhamisha shule nzima kwend secondary moja.

Je hii imenifanya nitafakari Sana namna selection zilivyofanyika au wote walichagua io shule.
Ndiyo lengo la shule za Kata
 
Screenshot_2024-12-16-19-03-32-719_com.android.chrome.jpg
 
Wamechaguliwa watoto wachache walioonyesha kitu cha ziada katika ufaulu wao! Kwa wale ambao wana uwezo wa akili wa kawaida nao wamepewa nafasi ya kukaa pamoja mpaka pale watakapoanza kujishtukia na kupiga msuli.
Ina maana hao vijana hawatakuwa na maarifa mapya ya kijamii maana wanafahamiana tangu utotoni. Uwezo wa kuchangamana na tamaduni zingine kwao utakuwa mdogo sana.

Huku ndio kuja kuwa na watu wanaoamini vyakula ni Ugali, wali na makande 😂 maana hawajui jambo jipya lolote.
 
Back
Top Bottom