JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mshauri wa Rasilimali watu Mosses Raymond amezungumzia upande wa pili wa msongo wa mawazo kitaalamu kwa kusema huwa inasaidia kuleta mabadiliko katika maisha ya mtu binafsi na inaweza kumfanya anenepa.
Mosses amesema wengine wakipata msongo wa mawazo hunenepa na kupata nuru kwa sababu hupenda kula sana na mwili ukipitia hali hiyo unahitaji ‘quickly recovery’.
Amefafanua kuwa watu wengi wanapenda kuangalia katika upande wa hasi pindi wanapokuwa wanazungumzia msongo wa mawazo ndiyo maana kawaida inaonekana msongo wa mawazo ni chanzo cha mwili kupukutika.
“Kitaalamu huwa tunasema msongo wa mwazo kwa kiwango fulani huwa ina faida kwa kuwa inakufanya utumie nguvu ya ziada kupata kile unachokitaka au ulichokikosa.
"Kuna wengine wakati wa msongo wa mawazo wanapenda chakula fulani na kuupa mwili unachokipenda ili kujitafutia nafuu na faraja ya mwili, hivyo lazima utanenepa.
“Kuna wengine wanakunywa pombe sana, wanavuta sigara sana, nk hiyo inamaanisha anakuwa anakula au kutumia kitu ambacho anaona kinampa faraja kwa wakati huo, kama ni chakula anaweza kukila mara nyingi zaidi ya kawaida, hiyo inafanya mwili unakuwa unapokea chakula kingi,” anasema Mosses.
Source: EATV