Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
😀😀😀😀😀😀😀😀😀 Forex haijawahi kumuacha mtu salama hata Ontario naye alisomeshwa namba kwenye Forex.
 
Hta kwenye betting hakutaki hicho kitu, tamaa.

Betting yenyewe weka hela yako ili upate 50℅ had 100% ya hela yako tu. Hapo utaenjoy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukisoma michango ya watu wengi humu unapata hasira kabisa na kugundua yani Tanzania ni nchi yenye mbumbu wengi kuliko nchi nyingi na huenda wanaochangia wengine ni vongozi wa taasisi kubwa kubwa na wanaaminiwa ila mtu anafananisha FOREX market na ponzi scheme yani basi tu
 
Umeandika vizuri sana mkuu... Big up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Q-NET pia wanatoa elimu vzr tu darasani lakini kama wewe Forex inakunufaisha basi endelea tu kuvuna pesa Mpendwa lakini mimi kama mimi kufanya biashara kama hizo ni NO, nitapambana na hizi biashara zingine za kawaida hata kama nitaanguka zaidi ya mara 7 lakini bado nitakuja kukaa imara tu na naamini nitafanikiwa zaidi na zaidi kimaendeleo Chifu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee baba nasikitika mnoo kuona hawa ndo wasomi wetu aisee watu wanafanya maamuzi kwa hisia binafsi forex ndo inanipa sababu za kuishi kabla sijaanza kidogo ndoa yangu ivunjike ila inenuchukua mwaka mzima kumfanya wife aache kazi na nikampa mtaji wa m 20 na sijuwahi kumuomba hata shilling anabaki kushangaa tuu Forex inahitaji mpambanaji anaejitambua na anaejua anachofanya siyo get rich quick

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena hata hiyo QNET huwa wanaitangaza kwenye magazeti kama Mwanachi n.k, so ngoja nipambane tu na hali yangu kivingine lakini siyo kuhusu online trading businesses.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inauma saba , nipo kwenye channel moja na watu wa mataifa ya ulaya, Asia na America. Kuna vijana Niko nao kule wanaijua forex tangu wakiwa na miaka 9. Kuna huyo mmoja anatokea Dubai yeye alikuwa anafundishwa na baba yake kufanya stocks tangu akiwa na miaka 10. Baada ya kuwa mtu mzima ndio kajiongeza kufanya Forex.


Kuna mzungu mmoja yeye huwa anatengeneza indicators za forex kwa kila anachosoma. Yaani kama ameaoma Quoter Theory yeye anaitengenezea indicator ili imsaidie trader. Jamaa nilisoma Biography yake kuwa ameijua forex tangu akiwa na miaka 16. Leo unashangaa mtanzania tena kwa cheap reasons anasema forex ni utapeli .



Ujamaa ulituharibu saaaana. Ulituziba kujua mambo mengi ya kidunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kwa maana nyepesi tuseme forex ni biashara ya wasomi au sio!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…