Mabibi na mabwana, inastaajabisha pale mshindani mmoja anapojipa wajibu wa kuweka sheria, kanuni, taratibu n.k kwa washindani wengine kufuata ili wapate kushinda mpambano ambapo yeye naye ni mnufaika.
Kwa minajili hii ni vipi mamba akamwongoza binadamu kuvuka mto salama? Vipi Fisi akashauri namna madhubuti ya bucha kuwa ili nyama isiwe hatarini kuliwa na fisi?
Namna gani ngedere akashauri ulinzi sahihi kwenye shamba la mahindi? Vipi shetani akamwongoza binadamu kufika kwa Mungu salama?
Labda kama ni maajabu ya Firauni!
Yapo mengi ya kushangaza ambayo CCM kupitia mamlaka na wakala mbalimbali imekuwa ikishinikiza kuwa sheria, kanuni au taratibu kwa kupitua mlango wa nyuma.
Muungano wa vyama vya siasa eti hata ushirikiano tu sasa ni haramu. Eti hata mgombea wa chama kimoja akimnadi mgombea wa chama kingine nayo sasa ni haramu.
Magufuli akimnadi Wenje Rorya, hiyo sawa. Lissu kumnadi Maalim au Maalim kumnadi Lissu hiyo haramu.
Mrema alimuunga mkono Magufuli. Hiyo halali. Ila kwa wengine kumwengua mwingine mkono, hiyo haramu.
TCRA nayo sasa haitaki TVs zionyeshe umati uliohudhuria. Eti beaming iwe kwa mnadi sera tu. Hawataki umati wa waliohudhuria kuonyeshwa. Kwamba nyomi za upinzani imekuwa nongwa!
Yako mengi na mengine ambayo hadi Oct 28 yataendelea kuzalishwa.
Hii ngozi kwenye kwamba hii ngoma inayovutiwa kwetu kiasi hiki na kuwataka wengine wote waicheze hii ngoma yetu vilivyo haiwezi kutufikisha mbali.
Palikuwa na haja ya kuipa hali hii isiyokuwa na afya msukumo tofauti.
Hivi nyie kina Spunda, Prof. Lipumba, Mbatia nk tofauti zenu na Chadema au ACT nini?
Umoja ni nguvu. Utengano wetu ndiyo unaotuletea longo longo hizi.
Kwa pamoja tunao uwezo na nguvu zaidi ya kuamua kusuka au kunyoa.
Kwanini tusiunganishe nguvu zetu kupinga kanuni, sheria na taratibu uchwara hizi zinazoendelea kuchipuka kama uyoga kila leo?
Kwa kufuata anachotaka mshindani mmoja kuwa tu ndiyo kifuatwe hatuwezi kutoboa.
Hatuwezi kuweka maslahi binafsi nyuma kwanza ili tupambane kwanza kuhakikisha tunapata mazingira yaliyo sawa kwa wote?