Msiache kuiomba mizimu yenu, hii ndo njia rahisi ya kufanikisha mambo

mkuu hivi unajua kinachoitwa mizimu ni majini?
 
biblia ipi imeelzea tumuombe Maria. Tunapaswa kuomba kwa Mungu tu through Yesu.
Vinginevyo ni umizimu

1 Timotheo 2:5​

Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu
 
watu Wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Wazungu wenyewe hawataki makanisa wala udini, wanasema kanisa ni taasisi za kisiasa na wanaenda wazee tu makanisani.

We komaa na madini ya watu ya kuletewa uache mizimu ya kwenu uone kama utatoboa utabaki kujiita mtakatifu hadi ufe.

Unakuta mtu anakomaa na jina la Yesu na Maria wengine wanakomaa na Muhammad.
Alafu anamsahau mzee mtafungwa, mzee Semfukwe mzee Chambo.
 

Yeye sio mzimu? Au kwa kuwa ni mzimu wa watu weupe?
 
Mizimu ni nini? Tuanzie hapo kwanza.
 
Mpaka sasa sijawaona atheists kwenye huu uzi ila ingekuwa ni kuhusu Mungu chap wangewahi kuuliza thibitisha kama Mungu yupo😀😀😀
Kama Mungu hayupo na kama mizimu haipo sijui ni nini kinacho wawasha washa kujadili vitu ambavyo havipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…