1.mizimu ni mapepo ,maroho(roho chafu)/majini ya ukoo asili yao ni serikali ya kuzimu kiongozi wake ni lucifer/shetani/joka kuu.
2.hakuna majini au mapepo wazuri
3.kazi yake hiyo mizimu mapepo ni uharibifu,kuleta laana,mikosi,magonjwa,vifo,umasikini,ufakara,vifungo vya dhambi kama uzinzi ndoa za mikataba na majini,roho zinazofuatilia kuleta uharibifu katika koo familia ,ulevi,kufikisika,kukataliwa,ugumba kutozaa,mimba kuharibika,kutokuendelea kielimu,kiuchumi,kiafya n.k
4.uganga wa kienyeji mizimu inaweza kukufanya mganga wa kienyeji au mchawi ambavyo vyote ni ushirikina uleule hakuna tofauti kati ya uchawi na uganga wa kienyeji
5.asili yake ni shetani na shetani hana urafiki na binadamu ,shetani ni baba wa uongo ni bingwa wa kudanganya wanadamu kupitia mizimu,waganga wa kienyeji ,mizimu n.k mwisho wa siku ni MAUTI na laana zinazotembea katika vizazi vya wote wanaoamini au kuabudu mizimu
6.Hakuna ushirika kati ya kuabudu mizimu / kuamini mizimu na kumuabudu Mungu wa kweli wa Mbinguni, yani ukisha anza kuabudu mizimu na kuiamini automatically umeshakuwa mpagani umekuwa vuguvugu/michanganyo huwezi kuchanganya ibada ya miungu mizimu leo kesho kuabudu Mungu wa kweli kanisani hapo wewe unahesabika ni mpagani.
7.upagani ibada za mizimu ibada za wafu zinafanywa hata na baadhi ya madhebu ya dini ya kikristo wame dilute imani kwa kuingiza tamaduni zao za kipagani katika baadhi ya madhebu ya dini ya kikristo na watu wanaabudu wafu mizimu na wameenda mbali na hata kuita ni watakatifu fulani wanawaomba wawaombee kana kwamba wao hawawezi kuomba direct kwa Mungu akawasikia..ndio maana baadhi ya wachangiaji wameuliza mbona katika baadhi ya madhehebu wana abudu mizimu ya wazungu??.Ni kweli hata ndani ya baadhi ya madhehebu kuna ambayo yameacha misingi ya kumuabudu Mungu wa kweli na kuingiza ibada za wafu mizimu makanisani.
HITIMISHO.
MUNGU wa mbinguni,pekee ,Yesu KRISTO pekee,ndio wa kutusaidia na
.SHETANI na mawakala zake (mizimu,majini,waganga wa kienyeji,wachawi) wao kazi yao ni uharibifu na si kusaidia
.Ukishajiingiza kwenye ibada za mizimu lazima hiyo familia au ukoo na vizazi vyao viambatane na laana ya mikosi na majanga mabalaa mbali mbali.