Msiache kuiomba mizimu yenu, hii ndo njia rahisi ya kufanikisha mambo

Msiache kuiomba mizimu yenu, hii ndo njia rahisi ya kufanikisha mambo

Mizimu sio yote mizuri mingine ni uchawi kwenda mbele mfano kwetu mizimu ya kwetu ni uchawi mtupu ivyo ngoja tubaki na bwana yesu tu
 
1.mizimu ni mapepo ,maroho(roho chafu)/majini ya ukoo asili yao ni serikali ya kuzimu kiongozi wake ni lucifer/shetani/joka kuu.
2.hakuna majini au mapepo wazuri
3.kazi yake hiyo mizimu mapepo ni uharibifu,kuleta laana,mikosi,magonjwa,vifo,umasikini,ufakara,vifungo vya dhambi kama uzinzi ndoa za mikataba na majini,roho zinazofuatilia kuleta uharibifu katika koo familia ,ulevi,kufikisika,kukataliwa,ugumba kutozaa,mimba kuharibika,kutokuendelea kielimu,kiuchumi,kiafya n.k
4.uganga wa kienyeji mizimu inaweza kukufanya mganga wa kienyeji au mchawi ambavyo vyote ni ushirikina uleule hakuna tofauti kati ya uchawi na uganga wa kienyeji
5.asili yake ni shetani na shetani hana urafiki na binadamu ,shetani ni baba wa uongo ni bingwa wa kudanganya wanadamu kupitia mizimu,waganga wa kienyeji ,mizimu n.k mwisho wa siku ni MAUTI na laana zinazotembea katika vizazi vya wote wanaoamini au kuabudu mizimu
6.Hakuna ushirika kati ya kuabudu mizimu / kuamini mizimu na kumuabudu Mungu wa kweli wa Mbinguni, yani ukisha anza kuabudu mizimu na kuiamini automatically umeshakuwa mpagani umekuwa vuguvugu/michanganyo huwezi kuchanganya ibada ya miungu mizimu leo kesho kuabudu Mungu wa kweli kanisani hapo wewe unahesabika ni mpagani.
7.upagani ibada za mizimu ibada za wafu zinafanywa hata na baadhi ya madhebu ya dini ya kikristo wame dilute imani kwa kuingiza tamaduni zao za kipagani katika baadhi ya madhebu ya dini ya kikristo na watu wanaabudu wafu mizimu na wameenda mbali na hata kuita ni watakatifu fulani wanawaomba wawaombee kana kwamba wao hawawezi kuomba direct kwa Mungu akawasikia..ndio maana baadhi ya wachangiaji wameuliza mbona katika baadhi ya madhehebu wana abudu mizimu ya wazungu??.Ni kweli hata ndani ya baadhi ya madhehebu kuna ambayo yameacha misingi ya kumuabudu Mungu wa kweli na kuingiza ibada za wafu mizimu makanisani.

HITIMISHO.
MUNGU wa mbinguni,pekee ,Yesu KRISTO pekee,ndio wa kutusaidia na
.SHETANI na mawakala zake (mizimu,majini,waganga wa kienyeji,wachawi) wao kazi yao ni uharibifu na si kusaidia
.Ukishajiingiza kwenye ibada za mizimu lazima hiyo familia au ukoo na vizazi vyao viambatane na laana ya mikosi na majanga mabalaa mbali mbali.
 
Hatufanikiwi maana mizimu hatuipi sadaka na hizi tunaita dini za wazungu na arabs hatutoi ukitoa ni alimradi ila si kwa kufuata kanuni, fuatilia wahindu,hao arabs n species zenye zina mafanikio nyuma wanatoa sadaka na kuheshimu wanachoabudu mno mno ...#upumbavu wangu.
 
Ni kweli sadaka ina nguvu sana ikitolewa kwa kanuni kikamilifu kwa moyo wa kupenda katika madhabahu ya Mungu ulimwengu wa ufalme wa NURU na hata katika madhabahu ya shetani(mizimu,waganga wa kienyeji,majini wachawi n.k ulimwengu wa kiroho wa falme za giza.
Tofauti ni moja tu
1)Ukitoa sadaka nono kwa MUNGU utaimarisha nguvu ya madhabahu ya Mungu wa kweli ,na nguvu ya kukusaidia,kukulinda wewe familia na shughuli kazi zako na vizazi vyako,pia utaimarisha ulinzi wako na mali zako,na utabarikiwa afya,kazi zako na familia yako,utastawi.
2)ukitoa sadaka nono kwa mizimu utaimarisha madabahu ya kuzimu katika kutambua hatima ya maisha yako na vizazi vyako katika kuleta uharibifu kwako ,familia na vizazi vyako shetani ni bingwa wa UONGO kudanganya anaweza kukupa mafanikio ya muda mfupi ila utalipi gharama kubwa ,kama unavyoona hao ma freemanson ,au matajiri wanaopata utajiri wao kwa mizimu ,waganga wa kienyeji,unaweza ukawaona kwa nje wanafuraha na wamefanikiwa ila kiroho wameuza roho zao kwa shetani wako kwenye vifungo,vizito na kuna baadhi wanatamni hata kujitoa huko..
MIZIMU inatesa hata umewahi kuona mtu anayesumbuliwa na mizimu ya uganga wa kienyeji?au mizimu inayoleta utasa,ugumba ,magonjwa ,ufukara umasikini,ulevi,uzinzi,vifo ktk familia,ulemavu,uchawi,kuvunja ndoa kuto kuoa au kuolewa,ndoa za majini,n.k
Mizimu inatesa sana watu ,wengine hawajui kwa nini wanateseka,wengine wanateseka kwa sababu ya mababu zao walitolea sadaka mizimu zamani hata kabla ya wao kizaliwa lakini ile sadaka imenena hata kizazi cha vitukuu na inawatesa leo.
 
shetani anafanya kazi kwa siri na kwa uongo mkubwa ukiona unashiriki ibada za kutoa sadaka kwa mizimu /kutambika una iamini mizimu na unaona kila kitu kipo sawa na unaona unapata mafanikio.Basi jichunguze vizuri shetani hana kitu cha bure lazima kuna sehemu katika maisha yako amekufunga anaharibu.
 
Msiache kuomba mizimu.

Utofauti wa maombi ya mizimu na maombi ya kawaida maombi ya mizimu yanajibu haraka Sana.

Na pia gharama za kuomba mizimu ni nafuu Sana.

Dini za magharibi ziliundwa kwa ajili yao ndo maana wao wanatukuza mizimu yao.

Sasa wewe unamuacha Babu yako unaenda kumuomba Maria au sijui nani unakuwa haupo serious.
Haya mambo vizazi vipya hawajui yashasahaulika
 
YESU PEKEE NDIO NJIA YA KWELI NA UZIMA MIZIMU HAIJAWAHI SAIDIA KITU

MIZIMU IMELAANIWA NI ROHO CHAFU

MSAADA WA YESU NI WA AJABU WAKATI UNAONA HAJAKUSAIDIA KUMBE TAYARI KAKUSAIDIA HAPO NDIPO WENGI HUWA HAWAELEWI NA KUONA YESU ANACHELEWA

LAKINI NENO LINASEMA BWANA HAWAI WALA HACHELEWI KWA HAO WAMTUMAINIO
Huu ndo ujinga wa wa waafrika walio wengi kuamini upuuzi wa wazungu na kusahau vya kwao
 
Habari za Yesu hata katika Historia zimeandikwa.
All historians believe Jesus existed here on the Earth na kama huamini historia basi utasema hata vita vya majimaji ni stori za kufikirika
Kuelewa huu uzi unahitaji kuwa na akili kidogo iliyochangamka.Wazungu walitengeneza mbinu ambazo ziliingilia mifumo yote ili kuutawala ubongo wa mwafrika kuanzia elimu hadi kwenye siasa na uchumi
 
Msiache kuomba mizimu.

Utofauti wa maombi ya mizimu na maombi ya kawaida maombi ya mizimu yanajibu haraka Sana.

Na pia gharama za kuomba mizimu ni nafuu Sana.

Dini za magharibi ziliundwa kwa ajili yao ndo maana wao wanatukuza mizimu yao.

Sasa wewe unamuacha Babu yako unaenda kumuomba Maria au sijui nani unakuwa haupo serious.
Vitabu vingi vya kimizimu vinasema mizimu ya afrika ilitekwa na wakoloni Bado ipo utumwani.
Hata wewe nikikuuliza uchawi wa kizungu na wa kiaafrika ni upo juu utanijibu ni wa kizungu
Au kati ya mchawi na jina la yesu nani zaidi? jibu unalo mwenyewe
 
Unaomba mizimu ya kizungu ikusaidie, unaifahamu? Hapo tumepotoka, Waafrika nawashauri kuanzia sasa tuirudie mizimu yetu na tutaona mafanikio.
 
Back
Top Bottom