Msiba wa Ruge uwe fundisho Kwa maprofesa

Msiba wa Ruge uwe fundisho Kwa maprofesa

Hivi maprofessor wamewakosea nini watanzania. Uprofesa ni cheo tu kule chuoni yaliyobaki ni kujiongeza kutegemea na mazingira. Mnategemea makubwa sana toka kwao lakini ni wachache wajuao ni mazingira gani wanafanyia kazi. Kwani kuzikwa kama mwanakijiji wa kawaida kuna tatizo gani?
Yaan pamoja na uwezo mkubwa wakusaidia jamii hawakufanya hivyo, hawana msaada, ndo mana wanafananishwa na wanakijiji,,, maprof wa kibongo baadhi yao ni vapour tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu professor ni mtu mkubwa Sana ndani ya jamii, ni mtu ambae anatakiwa kutengenezea wengine fursa, lakini hawa wa kwetu wengi wao wanaishia kwao wenyewe na ngazi ya familia zao Tu. Akijitahidi Sana atagusa kidogo watu wa kabila lao na kanda Yao Tu basii.
 
Kodi nyingi za wauza vitumbua zilitumika kumfanya yeye awe professor lakini hajarudi kwao kuwaonyesha namna bora ya kuoka vitumbua bila kuumizwa na moshi wa mafuta na mkaa wakati wa kuchoma vitumbua. Kazi Yao ni kuandika tafiti za kupandia vyeo na kuishia kwenye makabati ya maktaba. Nyambafu
Unataka kuwadhalilisha tu Maprofessor. Hivi unafikiri kama mtu amefundisha miaka 30 kwa mfano, ametoa ujuzi kwa watu wangapi achilia mbali tafiti zake na ushauri wake. Wewe unafikiri concept ya tafiti kaiweka nani? Na Professa asiye tafiti dunia hii ni professor wa wawapi. Tembelea SUA au Muhimbili uone maprofessor wanafanya kazi gani. Tafiti kuishia kwenye kabati ina mambo mengi nyuma yake na mara nyingi sio tatizo la professor duniani wachumi husema tuna "division of labor". Na hii inaweza kumaanisha kuwa siyo lazima professor apeleke kazi yake kijijini ingawa wako wengi tu wanaofanya tafiti moja kwa moja huko vijijini. Usichokijua ni kama usiku wa giza.
 
Maprofesa wetu wamezaliwa kijijini na wakunga wa jadi, walichapwa sana shuleni hadi wanaingia woga na hofu iliyobaki vifuani mwao hadi uzeeni.

Professor wetu hawezi kujiajiri mwenyewe hata kidogo, atazeekea kwenye vibarua na atafia kwenye vibarua vya watu. Amejaa hofu ya maisha, Hana ndoto amejaza tafiti asizoziamini, ziko kabatini kwake hakuna hata moja aliyoitekeleza. Akiulizwa anakwambia no funds. Akina Ruge walikuwa wanatafuta funds za kutengeneza ndoto zao ziwe kweli.
Utasema mengi sana, nashangaa kusema professor atazeeka kwenye vibarua, ulitaka azeeke wapi. Naona concept ya human capital huifahamu kabisa. Watu wana mazingira tofauti yanayo waruhusu kufanya mambo tofauti. Ili unayo taka yatimie basi badilisha mfumo waote wa vyuo vikuu duniani ikiwa ni pamoja na mfumo wa promotion. Binadamu huendana na incentives zilizopo. Hivi unajua hao maprofessor hela za huo utafiti wanazitoa wapi? Ruge amefanya yakwakwe aliyoweza, baba yake Ruge ambaye ni professa nae amefanya na anafanya yake anayo weza ikiwa ni pamoja na kumlea mwanae afike hadi hapo. Wewe unajua yule mzee amefundisha na kuwapa ujuzi watu wangapi?
 
Yaan pamoja na uwezo mkubwa wakusaidia jamii hawakufanya hivyo, hawana msaada, ndo mana wanafananishwa na wanakijiji,,, maprof wa kibongo baadhi yao ni vapour tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mnataka hao maprofessa wasaidiaje jamii? Kwa mfano chuo kama SUA kina outreach activities na utafiti ambao hufanya na jamii. Kama hawasaidii jamii unajuaje wana uwezo mkubwa wa kusaidia jamii?
 
Heshima ya mtu haitatokana na umri wako, elimu yako wala cheo chako kwenye jamii, bali itatokana na huduma yako Kwa jamii.

Unaowahudumia ndio watakaokukweza sio waliokuteua.

Tunao maprofesa hapa nchini kama watakufa leo watazikwa kama wanakijiji wa kawaida Tu. Elimu zao hazihusiki katika kutatua shida na kero za wanajamii wa kawaida kabisa. Ruge pamoja na umri wake mdogo na elimu ya kawaida kabisa (sio PhD wala Master's) lakini watu walifaidika nayo moja Kwa moja kiasi cha kuwafanya wajitokeze Kwa wingi kumlilia.

Elimu yako, cheo chako na umri wako ni bure kabisa kama raia wa kawaida kabisa kule nanjilinji.
Unafaidika vipi unapozikwa na mamilioni ya watu?
 
Mkuu professor ni mtu mkubwa Sana ndani ya jamii, ni mtu ambae anatakiwa kutengenezea wengine fursa, lakini hawa wa kwetu wengi wao wanaishia kwao wenyewe na ngazi ya familia zao Tu. Akijitahidi Sana atagusa kidogo watu wa kabila lao na kanda Yao Tu basii.
Unajua ni watu wangapi wanapata elimu kutoka kwa professor kila mwaka elimu ambayo inawasaidia katika maisha yao yote wao na familia zao?
 
Unataka kuwadhalilisha tu Maprofessor. Hivi unafikiri kama mtu amefundisha miaka 30 kwa mfano, ametoa ujuzi kwa watu wangapi achilia mbali tafiti zake na ushauri wake. Wewe unafikiri concept ya tafiti kaiweka nani? Na Professa asiye tafiti dunia hii ni professor wa wawapi. Tembelea SUA au Muhimbili uone maprofessor wanafanya kazi gani. Tafiti kuishia kwenye kabati ina mambo mengi nyuma yake na mara nyingi sio tatizo la professor duniani wachumi husema tuna "division of labor". Na hii inaweza kumaanisha kuwa siyo lazima professor apeleke kazi yake kijijini ingawa wako wengi tu wanaofanya tafiti moja kwa moja huko vijijini. Usichokijua ni kama usiku wa giza.
Hatukatai professor kafundisha watu wengi sana, lakini hawa waliofundishwa na professor mbona hawamuinui professor wao siku akifa kama Ruge alivyowahangaisha hata viongozi wote wakuu wa nchi alipokufa? Hivi iko haja professor atafute part time hata baada ya kustaafu rasmi? Badala ya kuajiri yeye anaajiriwa uzeeni kuwazibia fursa vijana. Yaani professor kashindwa kutengeneza mtu wa kumuachia kazi yake baada ya yeye kustaafu.
 
Hivi mnataka hao maprofessa wasaidiaje jamii? Kwa mfano chuo kama SUA kina outreach activities na utafiti ambao hufanya na jamii. Kama hawasaidii jamii unajuaje wana uwezo mkubwa wa kusaidia jamii?
Tena SuA Ndiyo usiitaje kabisa. Watu walitarajia sua ndo ingeongoza Mapinduzi ya kilimo nchini lakini hakuna kitu kabisa. 90% ya wakulima, wavuvi, wafugaji wanalima vilevile walivyokuwa wakilima, kuvua na kufuga kabla mkoloni hajafika. Ndio maana prof wa aina hiyo akifa anakufa kama mwanakijiji wa kawaida Tu. Hawaangalii hata vitabu wakaachia wananchi wasome. Nchi hii bado inaagiza vitabu toka kwingineko
 
Hatukatai professor kafundisha watu wengi sana, lakini hawa waliofundishwa na professor mbona hawamuinui professor wao siku akifa kama Ruge alivyowahangaisha hata viongozi wote wakuu wa nchi alipokufa? Hivi iko haja professor atafute part time hata baada ya kustaafu rasmi? Badala ya kuajiri yeye anaajiriwa uzeeni kuwazibia fursa vijana. Yaani professor kashindwa kutengeneza mtu wa kumuachia kazi yake baada ya yeye kustaafu.
Ungekaa ukajiuliza kwa nini Ruge anazikwa kitaifa kuliko hata viongozi wa kitaifa achilia mbali hao maprofesa usingeleta uzi wako wa kipuuzi kuwakejeli maprofesa! Kuna uzi humu unajaribu kujibu swali hili nenda kausome!

Maprofesa hawana jambo na msiba wa Ruge. And by the way unamdhalilisha pia baba yake Ruge Prof. Mutahaba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ona kama prof. Lihumba kaandika mwenyewe barua ya kujiuzuru na kisha akaikana kuwa haitambui. Maamuzi kama haya mtu kama Ruge asingeweza kufanya hivyo.
 
Ona kama prof. Lihumba kaandika mwenyewe barua ya kujiuzuru na kisha akaikana kuwa haitambui. Maamuzi kama haya mtu kama Ruge asingeweza kufanya hivyo.
Tena hawa maprofesa ni vigeugeu kuzidi hata wanasiasa sasa wataisaidiaje jamii wakati wenyewe ni maprofesa zero
 
Back
Top Bottom