Msibani imesemwa Hayati Lowassa alikuwemo JWTZ hadi Ukapteni na akashiriki vita vya Uganda. 2015 mzee Makamba alisema Lowassa hakwenda jeshini

Tumeona picha ya JK na Kinana wakiwa wamevaa kijeshi ila kama kuna ya Lowassa pia naomba watoto watuwekee pia ili tuwekane sawa au sio
Kumbukumbu lazima zipo
Hiyo sio tatizo kuvaa sare. Hata baba yangu mdogo baada ya kurudi na medali kadhaa aliweka kila kitu kabatini. Yawezekana Lowasa alifanya hivyo.

Wazee Kikwete na Kinana wakati ule waliendelea kuvaa sare hadi walipoingia kwenye siasa.
 
ALISHIRIKI VITANI lakini kwa majukumu ambayo hayakuhusisha battle field ….utaratibu wa vita rais akishasaini operesheni ya vita wote mlioagizwa kuwemo mnakuwa mko vitani ……sasa wengine wanaweza ikawa jukumu Lao lilikuwa kuhamasisha vijana kujiandikisha na kuwaandaaa kwenda vitani , wengine wana jukumu la kutafuta resources , wengine kufanya diplomasia ya vita kwa kutafuta kuungwa mkono etc ….
Vema sana mkuu.
Alikuwa kwenye kundi la wataalam.

Hawa wengi walipewa nyota tatu za ukapteni.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=SH9ks-0_wQ8

Mimi ni mmoja wa watu tulobahatika kuhudhuria msiba wa marehemu Edward Ngoyai Lowassa na nikawa na shauku kubwa ya kusikia historia ya mwanasiasa huyu.

Bila shaka protokali ya msiba haikukosa kuwa na kasehemu ka kueleza wasifu wa mzee huyu ili wengine kama mimi tulokuwa hatufahamu uzuri historia ya mzee huyu tungepewa fursa ya kufahamu historia hiyo.

Mwelezaji akaingia na wasifu wa marehemu Lowasa na kwa hakika historia hiyo ilikuwa imetayarishwa kwa umakini huku ikiwa imepangwa kwa üstadı katika sehemu ndogondogo kama vile elimu yake, kazi zake kama mwanasiasa, ubunge, utumishi wake wa jeshi la wananchi wa Tanzania, uwaziri wake na uwaziri mkuu.

Pia tuliambiwa kuwa Marehemu Lowasa amewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama cha mapinduzi kama za ukatibu mikoa na hata ndani ya sekretarieti.

Lakini ni sehemu ya utumishi wake ndani ya jeshi letu la wananchi wa Tanzania ambayo ilinifanya nisikilize kwa umakini.

Kwanza katika sehemu hii tulielezwa kwamba kati ya mwaka 1973-1974 marehemu Lowasa alitumikia Jeshi la kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria na hiyo ilikuwa ni kabla hajajiunga na masomo ya chuo kikuu baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita.

Kisha mwelezaji wetu akatuambia waombolezaji kuwa kati ya mwaka 1978 na 1980, marehemu Edward Lowasa aliwahi kutumikia jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha ukapteni huku akiongoza brigedi na pia akashiriki vita vya Uganda. Pia yaonyesha kwamba alikuwemo ndani ya jeshi kwa muda kidogo kama miaka miwili hivi.

Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 17 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.

Kupigiwa mizinga 17 na shughuli nzima kufanywa na JWTZ si tukio geni, lakini ni kutokana na mazungumzo na mijadala mbalimbali juu ya historia ya kiongozi huyu khasa na baadhi ya wanasiasa wengine na ambao pamoja nao walikuwa na urafiki na ukaribu mkubwa na marehemu.

Sasa basi, nikajaribu kudadisi kumbukumbu zangu na nikatua kwenye kampeni za kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 ambapo kampeni zilikuwa zikipita sehemu mbalimbali hapa nchini.

Lakini katika kampeni zake huko Morogoro CCM ikiwa imempitisha mgombea wao hayati John Magufuli, mzee Yusufu Makamba alipewa nafasi ya kueleza machache kabla hajampisha mgombea wa CCM Magufuli.

Ni katika maelezo yake ambayo yamo katika video ya Youtube, mzee Yusuf Makamba (kuanzia dakika ya 15) alidai kuwa marehemu Edward Lowasa alikuwa mwongo na alidanganya kwa kusema kwamba alikwenda jeshini na alipigana vita vya Uganda.

Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusikia wasifu ule mimi nikachukua "note book" yangu na nikaandika hii mada ili nije niwaletee hapa wakuu wa JF tuijadili.

Je, pale wanasiasa wanapoamua kuwaghilibu wananchi kwa minajili tu ya kutaka kura je, ni lazima binadamu wenzetu tuwashuhudie uongo hata ikiwa ni kwa gharama zozote?

CCM imejaaliwa kuwa na wazee waongo na wachawi.

Historia inajieleza yenyewe
 
Aliyesema siasa ni Uongo uliokomaa hakukosea.
Mwanasiasa yupo tayari kuongea lolote bila kujali anadanganya.
 
Hiyo sio tatizo kuvaa sare. Hata baba yangu mdogo baada ya kurudi na medali kadhaa aliweka kila kitu kabatini. Yawezekana Lowasa alifanya hivyo.

Wazee Kikwete na Kinana wakati ule waliendelea kuvaa sare hadi walipoingia kwenye siasa.
Sio kuvaa mkuu
Hata mimi nina picha tangu nijunge
Naongelea picha sio show
 
Na akina Kapteni Komba.

..Moses Nnauye, Abdulrahman Kinana, Yussuf Makamba, na wenzao, walikuwa ktk uhamasishaji wakati wa vita vya Kagera.

..Kikwete sina uhakika kama alikwenda vitani mstari wa mbele.

..Kuna interview moja nimemsikia Kikwete akisema aliitwa kwenda vitani, lakini ikatumwa barua nyingine aripoti makao makuu ya chama.

..Mwanasiasa ambaye anafahamika kutumikia vitani ni marehemu Brig.Gen.Hassan Ngwilizi ambaye aliongoza operation safisha dhidi ya magaidi wa Renamo wa Msumbiji.

NB:

..zitafutwe rekodi za wahitimu wa chuo cha Maafisa Monduli, na waliotunukiwa nishani ya vita vya Kagera, ili kuthibitisha suala la Lowassa.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=SH9ks-0_wQ8

Mimi ni mmoja wa watu tulobahatika kuhudhuria msiba wa marehemu Edward Ngoyai Lowassa na nikawa na shauku kubwa ya kusikia historia ya mwanasiasa huyu.

Bila shaka protokali ya msiba haikukosa kuwa na kasehemu ka kueleza wasifu wa mzee huyu ili wengine kama mimi tulokuwa hatufahamu uzuri historia ya mzee huyu tungepewa fursa ya kufahamu historia hiyo.

Mwelezaji akaingia na wasifu wa marehemu Lowasa na kwa hakika historia hiyo ilikuwa imetayarishwa kwa umakini huku ikiwa imepangwa kwa üstadı katika sehemu ndogondogo kama vile elimu yake, kazi zake kama mwanasiasa, ubunge, utumishi wake wa jeshi la wananchi wa Tanzania, uwaziri wake na uwaziri mkuu.

Pia tuliambiwa kuwa Marehemu Lowasa amewahi kushika nafasi nyeti ndani ya chama cha mapinduzi kama za ukatibu mikoa na hata ndani ya sekretarieti.

Lakini ni sehemu ya utumishi wake ndani ya jeshi letu la wananchi wa Tanzania ambayo ilinifanya nisikilize kwa umakini.

Kwanza katika sehemu hii tulielezwa kwamba kati ya mwaka 1973-1974 marehemu Lowasa alitumikia Jeshi la kujenga Taifa JKT kwa mujibu wa sheria na hiyo ilikuwa ni kabla hajajiunga na masomo ya chuo kikuu baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita.

Kisha mwelezaji wetu akatuambia waombolezaji kuwa kati ya mwaka 1978 na 1980, marehemu Edward Lowasa aliwahi kutumikia jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha ukapteni huku akiongoza brigedi na pia akashiriki vita vya Uganda. Pia yaonyesha kwamba alikuwemo ndani ya jeshi kwa muda kidogo kama miaka miwili hivi.

Hivyo hii sehemu ikanifanya nielewe maana ya shughuli hii kubwa ya maziko ya kijeshi ilofanywa kwa heshima ya marehemu Edward Lowasa na pia kupigiwa mizinga 17 kuonyesha heshima ya juu kwa kiongozi huyu.

Kupigiwa mizinga 17 na shughuli nzima kufanywa na JWTZ si tukio geni, lakini ni kutokana na mazungumzo na mijadala mbalimbali juu ya historia ya kiongozi huyu khasa na baadhi ya wanasiasa wengine na ambao pamoja nao walikuwa na urafiki na ukaribu mkubwa na marehemu.

Sasa basi, nikajaribu kudadisi kumbukumbu zangu na nikatua kwenye kampeni za kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 ambapo kampeni zilikuwa zikipita sehemu mbalimbali hapa nchini.

Lakini katika kampeni zake huko Morogoro CCM ikiwa imempitisha mgombea wao hayati John Magufuli, mzee Yusufu Makamba alipewa nafasi ya kueleza machache kabla hajampisha mgombea wa CCM Magufuli.

Ni katika maelezo yake ambayo yamo katika video ya Youtube, mzee Yusuf Makamba (kuanzia dakika ya 15) alidai kuwa marehemu Edward Lowasa alikuwa mwongo na alidanganya kwa kusema kwamba alikwenda jeshini na alipigana vita vya Uganda.

Mzee Makamba alidai kuwa alieandikisha majina ya walochaguliwa kwenda vitani wakati huo alikuwa ni alekuwa raisi wa awamu ya nne Jakaya Kikwete. Mzee Makamba akadai kuwa marehemu Lowasa alitakiwa ataje brigedi alokuwemo na pia ataje mkuu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusikia wasifu ule mimi nikachukua "note book" yangu na nikaandika hii mada ili nije niwaletee hapa wakuu wa JF tuijadili.

Je, pale wanasiasa wanapoamua kuwaghilibu wananchi kwa minajili tu ya kutaka kura je, ni lazima binadamu wenzetu tuwashuhudie uongo hata ikiwa ni kwa gharama zozote?

Makamba hana hata elimu.
 
Sasa hapa SUMAYE kaingiaje tena?
'Mafaili' ' yapo shaghalabaghala.
 
Back
Top Bottom