Msibani imesemwa Hayati Lowassa alikuwemo JWTZ hadi Ukapteni na akashiriki vita vya Uganda. 2015 mzee Makamba alisema Lowassa hakwenda jeshini

Tumeona picha ya JK na Kinana wakiwa wamevaa kijeshi ila kama kuna ya Lowassa pia naomba watoto watuwekee pia ili tuwekane sawa au sio
Kumbukumbu lazima zipo
Hiyo sio tatizo kuvaa sare. Hata baba yangu mdogo baada ya kurudi na medali kadhaa aliweka kila kitu kabatini. Yawezekana Lowasa alifanya hivyo.

Wazee Kikwete na Kinana wakati ule waliendelea kuvaa sare hadi walipoingia kwenye siasa.
 
Vema sana mkuu.
Alikuwa kwenye kundi la wataalam.

Hawa wengi walipewa nyota tatu za ukapteni.
 
CCM imejaaliwa kuwa na wazee waongo na wachawi.

Historia inajieleza yenyewe
 
Aliyesema siasa ni Uongo uliokomaa hakukosea.
Mwanasiasa yupo tayari kuongea lolote bila kujali anadanganya.
 
Hiyo sio tatizo kuvaa sare. Hata baba yangu mdogo baada ya kurudi na medali kadhaa aliweka kila kitu kabatini. Yawezekana Lowasa alifanya hivyo.

Wazee Kikwete na Kinana wakati ule waliendelea kuvaa sare hadi walipoingia kwenye siasa.
Sio kuvaa mkuu
Hata mimi nina picha tangu nijunge
Naongelea picha sio show
 
Na akina Kapteni Komba.

..Moses Nnauye, Abdulrahman Kinana, Yussuf Makamba, na wenzao, walikuwa ktk uhamasishaji wakati wa vita vya Kagera.

..Kikwete sina uhakika kama alikwenda vitani mstari wa mbele.

..Kuna interview moja nimemsikia Kikwete akisema aliitwa kwenda vitani, lakini ikatumwa barua nyingine aripoti makao makuu ya chama.

..Mwanasiasa ambaye anafahamika kutumikia vitani ni marehemu Brig.Gen.Hassan Ngwilizi ambaye aliongoza operation safisha dhidi ya magaidi wa Renamo wa Msumbiji.

NB:

..zitafutwe rekodi za wahitimu wa chuo cha Maafisa Monduli, na waliotunukiwa nishani ya vita vya Kagera, ili kuthibitisha suala la Lowassa.
 
Makamba hana hata elimu.
 
Sasa hapa SUMAYE kaingiaje tena?
'Mafaili' ' yapo shaghalabaghala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…