gaijin, tell u what... kwa wengine kiukweli ni charity! kuna mtu kijijini huko anakuambia mchukue huyu mwanangu ukakae nae na usimlipe mshahara, manake hapo home hata msosi ni issue! yaani kuna mtoto anahitaji a place to eat, and sleep! dada aliyenilea mimi ni nesi mkunga, na amekua sehemu ya familia yetu kabisa na hakosi kusimulia alivyopewa maisha na wazazi wangu! wanae wawili wamesoma chuo kikuu kwa msaada bado wa wazazi wangu na wamesoma kozi niliyosoma mimi (i guess insipiration an vitabu etc). undugu wetu haueleweki kwa watu wa nje, lakini tumekuwa familia!
unyanyasaji ni tabia ya mtu nadhani. usiangalie kigezo kimoja tu cha maisha ya bongo ukataka kutatua mfumo mzima wa maisha, haitowezekana. mtu anakaa mbagala anafanya kazi kariakoo, anaondoka alfajiri anarudi usiku. hana washing machine wala umeme wa kupikia. anakaa mbali coz ndo ana-afford pango. hata kama uko single pengine utahitaji hgeli ili kulinda vijana wa mtaani wasichukue katv kako!