Msidanganywe eti sasa hivi hali ya maisha ughaibuni ni rahisi

Ulikuwa unabeba boksi Galleriet ile mall Bergen Sentrum?
 
Kuna culture shock gani huko mkuu?Nimependa sana hiki kipengele!
 
Chiku hajawahi kuwa na mtoto, ni watu tu wanazusha. Mtoto wake mmoja tu wa kuakisi aka amemu adopt kutoka Tanzania.
 
Simjui. Mimi ni old school.Ila Chiku ndiyo Mtanzania nlimkuta ameishi Bergen miaka mingi zaidi. lkn kuna Watanzania wengi niliwakuta Bergen, watu poa sana
Mkuu ni hivi mimi nilipelekwa Denmark 2009 nikiwa mdogo sana 19 years 2008 na ex wangu. Tulipishana maswala flan kwasababu alizidi umri sana. Nikakimbilia Oslo baadaye nikaenda Bergen halafu Trondheim. Trondeim nimekaa sana mwaka mmoja wakati huo na makaratasi ya Denmark. Kuna msala nilifanya Trondeim wakanirudisha Denman 2012 nikasettle hadi 2017 nikapata permanent residence yangu. Bergen na Trondheim napafaham vema sana
 
Sawa. Wewe inabidi uniamkie Shikamoo maana wakati huo hata Norway nilishaondoka😅😅😅
 
Hivi mama ngonyani bado yupo huko

Ova
 
Nimepiga boksi hadi kufikia viwango vya wenyeji. Nilikuwa mjanja sana sanaaa. Hadi leo, lakini mwishowe nikasepa
 
Simjui Hamisa Mkuu ili namuonaga yule Hamisa Mrembo Mobetto 😜
Haha mkuu BAK. Huyu Hamisa bana sikumoja akaniita Ghetto kwake basi kulikuwa na wanorwegian tupu kasoro mimi na yeye. Piga kitu cha Arusha na larger kama hatuna akili nzuri. Sasa kuna mzee flani lager ilimlemea alikuwa na mguu wa kuku akaichomoa na kuwasha moja juu maamae nilitoka nduki. Hamisa alimaindi kichiz. Nikaenda kujificha kichani.

Ila Hamisa bana nitamtembelea tu almost ten years. Halafu anaongea Kinorsk kama mwenyeji.

Love Norway
 
mkuu kama na huko ulaya hali ni ngumu namna hiyo, vijana wetu mliopo huko mchunge sana msije mkaanza kumegwa na kuliwa tako,

mkafanana na dada zetu huku bongo wanaojiita madada poa, maana naskia wazungu si watu wazuri.
 
mkuu nikija ulaya naweza pata mke wa kizungu? au wanazengua?
 
Naomba Nisaidiwe Kuelewa Maana Ya Kazi Ya Kubeba Box
 
NAOMBA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA. MIMI NIMEISHA ULAYA ZAIDI ITALY NA UK KIDOGO SANA SPAIN PORTUGAL NA POLAND. KUSEMA UKWELI ANACHOKISEMSA HUYU JAMAA (JAPOKUWA ANAPIGA CHA ARUSHA) NI KWELI NA UKWELI MTUPU JAPO UNAWEZA KUWA MCHUNGU KWA WALE WANAOTAMANI KWENDA ULAYA. BINAFSI KWA RESEARCH NILIYOIFANYA KWA WAAFRIKA WENGI WANAKWENDA EUROPE KUTOKA NIGERIA NA GHANA, NI 5% AU CHINI YA HIYO WANAOFANIKIWA. NIMEISHI ITALY KWA MIAKA 5 WAKATI HATA KORONA HAIJAINGIA LAKINI HALI IKIKUWA MBAYA SANA KWA MIGRANTS WACHACHE SANA WALIKUWA WANAFANIKIWA KUPATA SEHEMU YA KULALA WENGI WALIKUWA WANAISHI NA KULALA STEND ZA METRO KAMA KUNA MTU AMEISHI ITALY HASA ROMA ATAKUWA ANAPAFAHAMU SANA TERMINI.
KUNA MTU AMEULIZA KUHUSU UAE [emoji1256] KWA SASA MIMI NIPO HUKU KUSEMA UKWELI KIDOGO FURSA ZIPO JAPO COMPETITION NI KUBWA SANA KUTOKA KWA WAHINDI, WAFILIPINO, WASRILANKA, NA WABANGLADESH. MALIPO NI KIDOGO JAPO HUWEZI KUFANANISHA NA BONGO OF COURSE LAKINI KUWA COMPANY NYINGI BINAFSI NI ZA WAHINDI BASI WANAPEWA KIPAUMBELE SANA.
UZI WA YULE JAMAA ANAYE SAVE 80,000KRN KWA MIEZI 3 SIYO REALISTIC JAPO INATEGEMEA NA KAZI ANAYOFANYA. SIYO RAHISI SANA KUPATA KIPATO HICHO KTK UHALISIA.

SIMKATISHI TAMAA MTU ANAYETAKA KUCHOMOKA BONGO MAANA UTAFUTAJI HUWEZI JUA RIZIKI YAKO ILIPO ILA KABLA HUJATOKA BONGO NASHAURI UWE UMEJIRIDHISHA BEYOND ANY QUANTUM OF DOUBT LA SIVYO UTAJUTA SANA.

Tuendelee kupambana, na Mungu atatubariki.
Naomba kuwasilisha.
 
Amina Mkuu, mwaka 2011 nilikuwa nasee gepu niende botswana, zimbu na swaz...ila kwa sasa namshukuru mungu naiona bongo tamu sitaman kusepa wala kwenda nje..
Nami nishauri kwa uelewa wangu mdogo na xposure ndogo basi bongo kuna fursa nyingi za kutoka kuliko huko kwingine, cha muhimu ni kuzingatia principles za mtu kuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba Nisaidiwe Kuelewa Maana Ya Kazi Ya Kubeba Box
Ni kazi ambazo haziitaji elimu yoyote, ni Kama vile kuhamisha mizigo mfano bizaa kutoka kweNye magari kuingiza super market, kubeba maboksi kutoa sehemu 1 kwenda sehemu nying, kufanya usafi super market, kupanga bidhaa super market n.k Yani kwa kifupi ni kazi za kuzaraulika zisizohiyaj elimu ila kwa Ulaya watu kupitia kaz hizo wanaishi wanajenga na kusomesha watoto kwa huku kwetu Africa.
 
Reactions: svc
Bak? 😳 🤔
 
Kwa mtu aliyekulia Masaki na Oysterbay (Wa Kishua) Ulaya maisha ya Box ni Magumu lakini kwa watoto wa Manzese, Mwembe Yanga na Kiwalani Bom-Bom life la Box Ulaha ni afadhali kuliko Bongo.
 
Mkuu masuala ya ajira ni magumu dunia nzima, lakini nchi za ulaya magharibi kuna unafuu mkubwa sana ukilinganisha na sehemu zingine za dunia, kama upo ulaya na unaishi kihalali huwezi kukosa kazi labda kama unachagua kazi za taaluma fulani tuu, hivi sasa ulaya magharibi kazi ni nyingi sana na hata wana anza kuleta wafanya kazi wa muda kutoka asia
 
Tutakuja tu hivyo hivyo hata iweje .."mtembea bure siyo sawa na mkaa bure, huenda akaokota"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…