Poleni wadogo zangu, ni kweli wanaume wengi hawajazoea dada kueleza hisia zake when it comes to love, lakini niwatie moyo, naomba msikate tamaa endelea kutafuta iko siku mtapata. Niwaombe sana msijirahisi kwa hai vicheche na wekeni msimamo kwamba suala la ngono wasubiri mpaka mfunge ndoa tu, kwa hapo mwenye nia na aliyemaanisha itakuwa rahisi kumjua. Na wakati mwingine mtu anaweza kuja na mawazo ya ngono lakini akikukuta uko serious na mwenye msimamo hatakueleza upumbavu wake wa kutaka ngono hovyo. La msingi zaidi ya yote mtangulizeni Mungu na shirikisheni na wacha Mungu wengine wawaombee.
Mimi kwa raha ninayoipata kwa wifi yenu nawaombea na nyie mpata your dream husbands, kila la heri.