Msigwa alalamikiwa kuwalamba block CHADEMA wenzake

Msigwa alalamikiwa kuwalamba block CHADEMA wenzake

inauma sana unapoona wengine kila mara wanawezeshwa huku frame aka CDM ikiendelea kuwepo, anajua nini kinaendelea kwa Covid 19 behind the scene, anajua mwenyekiti kwa sasa mlengo wake ni upi, anajua nini kilifanyika kwa EL.... amekataa kuwa boya kila siku kutundishwa nini cha kufanya huku anajua wengine wanafanya nini...
 
Itafahamika tu ushauri wa lowassa ulikuwa wa maana sana chama kutoka kwenye uanaharakati!

Lowassa hakuwa mwanasiasa, bali mwizi aliyefanikiwa kuiba kupitia mlango wa siasa, hadi akawa na ndoto ya kuwa rais. Kwa kiwango kikubwa Lowassa alichangia kuitoa CDM kwenye siasa zake, kisha akarudi kwenye siasa za mbeleko ya vyombo vya dola ili aendelee kula asali.
 
Chadema, wanaharakati hawajui siasa na ndio maana inakuwa taabu kuaminiwa...

Chadema ina vijana wengi ambao ni waropokaji tu

Hizi ni porojo za kila mwanaccm.
 
Huyo Hilda anashangaa yeye kublokiwa mbona mimi huyo Hilda aliniblock baada ya kumchalenji akanipiga tofati la utosi? CHADEMA wanaaminiwa sana na wananchi ila wao wengi sio watu wa kucheza na upepo wa siasa,hawanaga ajenda ya kufa kupona wakienda na ajenda miezi miwili inapotelea mawinguni

Wenzao CCM wanapita humo humo kwenye udhaifu wao. Hali ni ngumu jobless sio titlle nzuri aisee mwacheni mchungaji apate haki yake kikatiba
 
CHADEMA imeharibiwa na wanaharakati wa mtandao akina maria na martini na wenzao. Chama hakina sera wala mwelekeo tena.
Martin ni nani CHADEMA? Ana uongozi Gani? Tatizo lenu mnaleta content za mtandaoni kama ndio misimamo ya chama. Chama kinaendeshwa na vikao rasmi Sio clubhouse au Mariaspaces so maoni binafsi yaheshimiwe maana ndio Demokrasia hiyo ila by any means hayana correlation na masuala ya chama.

NB: Mmekua mkisema CHADEMA hakuna Demokrasia sasa why watu wakipishana kauli kidogo ionekane sio Demokrasia ila udikteta? Au mnataka afungwe mdomo mrudi kusema Mbowe ni mkatili!!?
 
Msigwa kumbe yuko soft minded sana, sikujua; ieleweke kwamba siku zote kutofautiana na wenzio kimsimamo kwenye taasisi yenu kuhusu jambo fulani, hakumaanishi umejiunga kwa wale unaodhaniwa, unachotakiwa kufanya ni kubaki ukijitambua huku ukiujua uelekeo wako.

Namaanisha kwamba, hata mkitofautiana jambo moja kitaasisi/binafsi, bado kuna uwezekano mkakubaliana kwenye jambo lingine, na hili kama lingefanyika lingemrudishia Msigwa kuaminiwa.

Lakini kwa kisirani chake cha kuwa "block" wenzake, na kuendelea kubaki na msimamo wake kuhusu Ngorongoro huku akipigiwa debe na lumumba, ameharibu.

Alitakiwa awaache wale waendelee kumsema vibaya lakini bado awe nao pamoja, awe marafiki nao asijenge nao uadui, kwani mbele angekuja kuaminika tena hili la sasa litakapopita, huu ni upepo tu, lakini Msigwa ameacha huu upepo umchukue.

Hili kama lingefanyika lingesaidia kubadilisha "mindset" ya upinzani wetu, kuunga mkono jambo la mpinzani wako kungeanza kuzoeleka, isingeonekana na kosa, lakini Msigwa ameshindwa kujiongeza ili aje kuonekana shujaa baadae, Msigwa kaamua kuendeleza "precedence" hii ya kumuunga mkono mpinzani wako kisiasa kwa jambo fulani ionekane ni kosa.

Matokeo yake kwa huu uamuzi wake sasa atazidi kuwa na maisha magumu ndani ya Chadema, na asipokuwa makini atajikuta anakimbilia CCM bila kupenda ila kwa kukosa kwake maarifa ya kui "handle" situation aliyopo.

Sijui kama akikimbilia huko CCM halafu itokee akatofautiana tena na wenzake atakimbilia wapi kwa hiki kisirani chake..
Msigwa ni mwanasiasa mwenye fikra huru siyo wale wanasiasa wa wengi wake au benders kufuata upepo uendako Msigwa atabaki kuamini anachoamini kuwa ni sahihi hata kama atapingwa na CHADEMA wote
 
Huyo Hilda anashangaa yeye kublokiwa mbona mimi huyo Hilda aliniblock baada ya kumchalenji akanipiga tofati la utosi? CHADEMA wanaaminiwa sana na wananchi ila wao wengi sio watu wa kucheza na upepo wa siasa,hawanaga ajenda ya kufa kupona wakienda na ajenda miezi miwili inapotelea mawinguni

Wenzao CCM wanapita humo humo kwenye udhaifu wao. Hali ni ngumu jobless sio titlle nzuri aisee mwacheni mchungaji apate haki yake kikatiba
CCM Wana serikali ni rahisi kupeana vyeo kutulizana which is not the case kwa upinzani. Huku hakuna maslahi binafsi ni more of kujitolea kiharakati so mtu akisusa hakuna kikubwa Cha kumpa Ili atulie ndio maana ikawa ngumu Mbowe kumshawishi Mdee aache ubunge. Ila CHADEMA ingekua na serikali Ina maana Mdee angepewa hata ubalozi huko n.k

On the contrary, Unadhani CCM ingekua chama Cha upinzani kina Polepole,Bashiru, au Nape wangebaki baada ya kudhalilishwa vile?? Ila hawaondoki sababu wanajua power ipo CCM so kesho tu wanaweza pewa cheo wakipiga kelele mbili tatu.
 
wamemalizana na JPM now wameanza kuparurana wenyewe kwa wenyewe
 
Msigwa kaamua kujitenga na uanaharakati

View attachment 2268322
Kama Msigwa kafika bei mwacheni aende zake, kwangu mimi mtu pekee akiwapiga block makamanda au kujitenga na CDM nitasikitika nusu kufa ni Freeman Aikael Mbowe peke yake! wengine wote wakishuka atreni na kupanda wakashuka tena sina habari, safari itaendelea kama kawa! CDM wameikuta, na itaendelea kuwapo! Period
 
Denoo hata wewe unafanya makosa,unapinga maono ya wenzako ukitaka wafuate maono yako. Let’s all agree to disagree
Hapana, demokrasia sio kukubali hata mawazo ya kijinga, ndio maana kwenye chaguzi za kidemokrasia mshindi hupatikana kwa kura nyingi atakazopigiwa.
 
Msigwa hataki unafiki kama kawaida ya wanyalukolo walivyo.

Utakuwaje pamoja na watu ambao hamko pamoja kimtazamo. na hata ukichunguza kwa undani sababu ya kutokuwa pamoja, hakuna hoja nzito na makini za kutokuwa pamoja. watu wameamua kujitoa ufahamu na kupinga kila kitu ambacho serikali inafanya. Vingine vinaonekana wazi kabisa ni vya msingi, lkn kwa sababu vinatoka serikalini, basi ni kupinga tu.

Pia nadhani neno chama cha upinzani libadirishwe, viitwe vyama mbadala, maana ukisema upinzani, uwezo wa kufikiri unapotea, yaani hivyo vyama vinakuwa ni kupinga tuuu. Hata jambo ambalo kwa wazi kabisa lina masilahi ya taifa, wenyewe ni ubishi tu.

Tujiongeze, tuachane na fikra za wazungu, waliposema opposition party, basi sisi ni kupinga kwa kwenda mbele.
Kuwa pamoja na watu msio pamoja kimtazamo ni jambo la kawaida maishani, ila kwa wenye akili timamu, hamuwezi kufanana mtazamo kwenye kila jambo.

Msigwa alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuondoa hiyo dhana ya wapinzani/vyama mbadala kupinga kila jambo, na angeijenga heshima yake kupitia hapo kama angeamua kukaa meza moja na hao wasiomuelewa, waendelee na shughuli zao naamini iko siku wangekuja kuelewana kwenye issue nyingine, hivyo uaminifu kati yao ungefufuka.

Lakini kwa kuwa block maana yake amejitenga nao, amezidi kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kuliondoa, na hii itasababisha tofauti baina yao kuchukua muda mrefu zaidi kupatiwa ufumbuzi.
 
Kuwa pamoja na watu msio pamoja kimtazamo ni jambo la kawaida maishani, ila kwa wenye akili timamu, hamuwezi kufanana mtazamo kwenye kila jambo.

Msigwa alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuondoa hiyo dhana ya wapinzani/vyama mbadala kupinga kila jambo, na angeijenga heshima yake kupitia hapo kama angeamua kukaa meza moja na hao wasiomuelewa, waendelee na shughuli zao iko siku wangekuja kuelewana kwenye issue nyingine, hivyo uaminifu kati yao ungefufuka.

Lakini kwa kuwa block maana yake amejitenga nao, amezidi kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kuliondoa, na hii itasababisha tofauti baina yao kuchukua muda mrefu zaidi kupatiwa ufumbuzi.

Umejenga hoja mujarabu katika maisha ni kawaida kujikuta katika hali kutokubaliana na jambo fulani. Msigwa aendelee kuwaelimisha kwamba ukiwa chama cha upinzani kazi yako siyo kupinga tu. Na kupinga haimaanishi ndiyo kujenga, nyakati nyingine unaweza kupinga kitu fulani na matokeo yake hayawi chanya, bali fungu la kukosa na kuharibu. Hilo Msigwa lazima alijue pia, aweke hisia na kuwafahamu aina ya watu hao pembeni.

Lakini kwa upande mwingine inaumiza sana, maana unakuta mtu anabisha kuhamisha wamasai kutoka kondeni, huku hali akiiona kuwa mbaya kiasi hiki. Wewe umewahi ona wapi makazi ya wanyama wa kondeni wakiishi pamoja na binadamu waliojenga nyumba ambayo si rafiki kwa mazingira.



1655904125686.png
 
Mkuu inaonekana una GUBU SANA [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hapana mkuu,

Haya machadema ni manafiki sana!

Zitto akikutana na Samia wanasema kanunuliwa,

Mbowe na Lisu wakikutana na Samia wanapiga makofi kwamba hiyo ndio democrasia!

Kwenye mkutano mkuu wa chama mwezi uliopota Mbowe aliwaambia wafuasi wake waache kutukana watu wanaotofautiana nao mawazo!

Bila shaka Mbowe ameshaanza kujua kwamba anaongoza genge la wahuni.
 
Lowassa hakuwa mwanasiasa, bali mwizi aliyefanikiwa kuiba kupitia mlango wa siasa, hadi akawa na ndoto ya kuwa rais. Kwa kiwango kikubwa Lowassa alichangia kuitoa CDM kwenye siasa zake, kisha akarudi kwenye siasa za mbeleko ya vyombo vya dola ili aendelee kula asali.
Mwizi akataka kuitumia chadema kwenda ikulu?

Yani chadema ilitaka kupeleka mwizi ikulu!

Huoni kama hicho chama ni cha mazuzu?
 
Back
Top Bottom