Msigwa alalamikiwa kuwalamba block CHADEMA wenzake

Msigwa alalamikiwa kuwalamba block CHADEMA wenzake

Msigwa kumbe yuko soft minded sana, sikujua; ieleweke kwamba siku zote kutofautiana na wenzio kimsimamo kwenye taasisi yenu kuhusu jambo fulani, hakumaanishi umejiunga kwa wale unaodhaniwa, unachotakiwa kufanya ni kubaki ukijitambua huku ukiujua uelekeo wako.

Namaanisha kwamba, hata mkitofautiana jambo moja kitaasisi/binafsi, bado kuna uwezekano mkakubaliana kwenye jambo lingine, na hili kama lingefanyika lingemrudishia Msigwa kuaminiwa.

Lakini kwa kisirani chake cha kuwa "block" wenzake, na kuendelea kubaki na msimamo wake kuhusu Ngorongoro huku akipigiwa debe na lumumba, ameharibu.

Alitakiwa awaache wale waendelee kumsema vibaya lakini bado awe nao pamoja, awe marafiki nao asijenge nao uadui, kwani mbele angekuja kuaminika tena hili la sasa litakapopita, huu ni upepo tu, lakini Msigwa ameacha huu upepo umchukue.

Hili kama lingefanyika lingesaidia kubadilisha "mindset" ya upinzani wetu, kuunga mkono jambo la mpinzani wako kungeanza kuzoeleka, isingeonekana na kosa, lakini Msigwa ameshindwa kujiongeza ili aje kuonekana shujaa baadae, Msigwa kaamua kuendeleza "precedence" hii ya kumuunga mkono mpinzani wako kisiasa kwa jambo fulani ionekane ni kosa.

Matokeo yake kwa huu uamuzi wake sasa atazidi kuwa na maisha magumu ndani ya Chadema, na asipokuwa makini atajikuta anakimbilia CCM bila kupenda ila kwa kukosa kwake maarifa ya kui "handle" situation aliyopo, na sijui kama akikimbilia huko CCM halafu itokee akatofautiana tena na wenzake atakimbilia wapi kwa hiki kisirani chake cha kitoto alichofanya.
Msigwa ana haki ya ku block yeyote asiyependa kuwasiliana nae, ni uhuru wake na asipangiwe. Tatizo kubwa ndani ya upinzani wanahubiri demokrasia ilia hawezi kuishi kwenye demokrasia. Ukiwa tofauti kimtizamo utaitwa msaliti, umefika bei, au kibaraka.
 
Katika kuunganisha dot tunaweza kusema kuna jambo la siri linaendelea baina ya MSIGWA na SHANGAZI YETU Bint Karume maana wote wameonyesha kuwa na Bifu na CHADEMA kipindi hiki. Na pia wote wamekuwa na msimamo mmoja kuhusu issue ya Loliondo.

Ni suala la muda tu tuendelee kusubiri
 
Msigwa ana haki ya ku block yoyote asiyependa kuwasiliana nae, ni uhuru wake na asipangiwe. Tatizo kubwa ndani ya upinzani wanahubiri demokrasia ilia hawezi kuishi kwenye demokrasia. Ukiwa tofauti kimtizamo utaitwa msaliti, umefika bei, au kibaraka.
Msigwa ndio alitakiwa kuwa "advocate" wa hiyo demokrasia anayohubiri badala ya kuwa block wenzake, kitendo cha kuwa block maana yake pia hataki mawazo tofauti na yake, amefeli.
 
Yuko sahihi kuwablock, ktk mambo ambayo chadema wanakera ni pale mtu anapotofautiana nao ktk maamuzi akaitwa msaliti, kama tunaitaji chama imara tunahitaji kuwa na vifua vya kumeza nakupokea hata kama chungu nakuheshimu maamuzi ya kila mmoja
 
Chadema, wanaharakati hawajui siasa na ndio maana inakuwa taabu kuaminiwa...

Chadema ina vijana wengi ambao ni waropokaji tu
Kwa hiyo wewe siyo bavicha kumbe?

Wewe ni mwanangogwe?
 
Back
Top Bottom