Msigwa kumbe yuko soft minded sana, sikujua; ieleweke siku zote kutofautiana na wenzio kimsimamo kwenye taasisi yenu kuhusu jambo fulani, hakumaanishi umejiunga kwa wale unaodhaniwa, unachotakiwa kufanya ni kubaki ukijitambua huku ukiujua uelekeo wako.
Namaanisha kwamba, hata mkitofautiana jambo moja kitaasisi/binafsi, bado kuna uwezekano mkakubaliana kwenye jambo lingine, na hili kama lingefanyika lingemrudishia Msigwa kuaminiwa.
Lakini kwa kisirani chake cha kuwablock wenzake, na kuendelea kubaki na msimamo wake kuhusu Ngorongoro huku akipigiwa debe na lumumba, ameharibu; alitakiwa awaache wale waendelee kuwa pamoja, awe marafiki nao asijenge nao uadui, mbele angekuja kuaminika tena hili litakapopita, huu ni upepo tu, lakini Msigwa ameacha huu upepo umchukue.
Matokeo yake kwa huu uamuzi wake sasa atazidi kuwa na maisha magumu ndani ya Chadema, na asipokuwa makini atajikuta anakimbilia CCM bila kupenda ila kwa kukosa kwake maarifa ya kui handle situation aliyopo.