SI KWELI Msigwa amesema Tanzania inaongoza Afrika katika kuzalisha umeme

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Akizungumza na wanahabari katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani siku ya Jumapili Februari 16, 2025, Msigwa amesema kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati uliofanyika Januari 27-28, 2025 jijini Dar es Salaam, ni uthibitisho wa mafanikio ya Tanzania katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Msigwa, hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%, huku serikali ikipanga kuhakikisha asilimia 100 ya Watanzania wanapata huduma hiyo ifikapo mwaka 2030.
 
Tunachokijua
Gerson Msigwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali.

Mnamo tarehe 16 Februari 2025 Msigwa alifanya mkutano na waandishi wa habari ambao ulirushwa mbashara na vyombo mbalimbali vya habari kutoka bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Rufiji mkoani Pwani ambapo pamoja na mambo mengine alieleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo wa kufua umeme akisema umefikia asilimia 99.8

Kumekuwapo taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii Kuwa katika mkutano huo Msigwa alisema Tanzania inaongoza Afrika katika kuzalisha umeme.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa kauli hiyo haikutolewa na Gerson Msigwa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP)

Aidha JamiiCheck ilibaini nchi ambazo zinaongoza kwa uzalishaji wa umeme barani Africa kuwa ni Afrika kusini, Misri, Algeria, Morocco, Nigeria, Libya, Ghana, Tunisia, Msumbiji, Zambia

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022 za Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) linalotoa uchambuzi, takwimu, na mapendekezo ya sera, linaainisha orodha ya nchi zinazozalisha umeme kwa kiwango kikubwa zaidi ukiongozwa na Afrika kusini ikichangia asilimia 25.9% ya uzalishaji wote barani afrika ikizalisha Gigawatt 234 850 ikifuatiwa na nchi za Misri, Algeria, Morocco, Nigeria, Libya, Ghana, Tunisia huku Tanzania ikishika nafasi ya 18 katika orodha hiyo.

Kwa mujibu wa ceicdata kwa mwaka 2024 hadi mwezi Novemba Afrika kusini ilizalisha umeme hadi kufikia Gigawatt 216,310 sawa na wastani wa Gigawatt 19,664.55 kwa mwezi,

Uzalishaji wa umeme barani Afrika
Mwaka 2022, Afrika ilizalisha jumla ya GWh 905,136 za umeme, ikiangazia ukuaji wa sekta ya nishati barani humo. Afrika Kusini iliongoza kwa kuzalisha GWh 234,850 (25.9%), ikifuatiwa na Misri yenye GWh 208,739 (23.1%). Algeria ilichangia GWh 91,231 (10.1%), ikionyesha umuhimu na upatikanaji wa nishati Kaskazini mwa Afrika. Morocco na Nigeria zilichangia GWh 42,722 (4.7%) na GWh 37,915 (4.2%), huku Morocco ikipiga hatua katika nishati mbadala.

Libya, Ghana, Tunisia, Msumbiji, na Zambia zimeingia nafasi kumi bora, kila moja ikichangia kati ya 2.2% na 3.9%. Mgawanyo huu unaonyesha tofauti ya upatikanaji wa nishati barani Afrika, huku msisitizo ukiwa kwenye hitaji la ukuaji endelevu, kuboresha miundombinu, na kuongeza upatikanaji wa nishati ili kusaidia maendeleo. Kadri mahitaji yanavyoongezeka, uwekezaji katika nishati safi ni muhimu kwa mustakabali wa bara la Afrika.

Wakuu nimekutana na taarifa hii iliyochapishwa na mwanahabari digital kwamba Gerson Msigwa amesema Tanzania inaongoza kwa uzalishaji umeme Afrika Je, ni kweli?
====

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Akizungumza na wanahabari katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani siku ya Jumapili Februari 16, 2025, Msigwa amesema kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati uliofanyika Januari 27-28, 2025 jijini Dar es Salaam, ni uthibitisho wa mafanikio ya Tanzania katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Msigwa, hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%, huku serikali ikipanga kuhakikisha asilimia 100 ya Watanzania wanapata huduma hiyo ifikapo mwaka 2030.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…