Ogopa wajinga wakiwa wengi Wanaweza Kuchagua Rais, hasa wajinga wanapolindwa na nguvu ya Dola katika kutoa maoni ya kijinga huku watu wenye maarifa wakikaa kimya na kuangalia yanayoendelea
Plato aliona kuwa watu wengi, ambao aliwataja kama "wajinga," hawana uwezo wa kufanya maamuzi bora ya kisiasa kwa sababu hawana uelewa wa kutosha kuhusu mambo muhimu ya kiserikali au kijamii. Kwa hiyo, akasema kwamba uhuru wa watu hawa kutoa maoni na kushiriki katika maamuzi ya umma unaweza kuwa hatari kwa ustawi wa jamii.
Kwa mfano, Plato alilinganisha demokrasia na meli inayoendeshwa na wafanyakazi wasio na uzoefu, huku mabaharia wenye maarifa na uzoefu wakiwa hawazingatiwi. Katika hali kama hiyo, anasema kuwa meli haitaweza kufika salama kwa sababu ya ukosefu wa uongozi wenye hekima na maarifa