Msigwa: Tanzania siyo nchi ya kuamuliwa na Wanaharakati

Msigwa: Tanzania siyo nchi ya kuamuliwa na Wanaharakati

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa mahojiano na Bongo FM Mei 15, 2026, amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayojiongoza kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni zake, na haitakubali kuendeshwa au kupangiwa namna ya kufanya mambo yake na wanaharakati.

"Tanzania sio nchi ambayo inatakiwa iamuliwe na mwanaharakati namna ya kuendesha mambo yake.

Tanzania inaendeshwa mambo yake kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni zake kama zinavyoongozwa na katiba ya nchi yetu. Lakini pia Tanzania inaendeshwa kwa maslahi ya Watanzania na sio kwa maslahi ya mtu mwingine yeyote aliyeko iwe ndani au nje ya nchi."

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa mahojiano maalum aliyofanya na kituo cha redio cha Bongo FM Mei 15, 2026, amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru inayojiongoza kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni zake, na haitakubali kuendeshwa au kupangiwa namna ya kufanya mambo yake na wanaharakati.

SG G.Msigwa is very right,

halafu the gentleman as days goes he becomes more brilliant politically speaking 🔥
 
Hata wakoloni weupe walikuwa wanasema maneno haya haya pindi wapigania uhuru wetu kina mzee kinjekitile ngwale, Mzee Mirambo, Mzee Isike, Mzee Mangimeli, Mzee Nyerere, Bibi Titi mohamed na wengine wote waliopigania uhuru ila hawakufua dafu mbele ya nguvu ya uma.

Ni sauala la muda tu Nchi itatoka kwenye makucha ya mkoloni mweusi CCM na kwenda kwa wenye Nchi, Iwe chadema, act wazalendo au chama kingine nje ya hivyo.

Msigwa akumbuke kuacha alama ambazo kizazi chake kitaendelea kukumbukwa kwa mema aliyotendea Nchi hii na sio kukiacha kizazi chake kikiishi kama panya kwenye utawala wa paka.

Uzalendo wa kweli ni kuipenda Nchi yako kwa kuisema kweli daima hata kama hiyo kweli inaumiza. Hakikisha kila kitu kinakuwa juu ya ukweli, Kweli humweka mtu kuwa huru, hizi tabia za kupenda wanasiasa balada ya kuipenda nchi yako haitatufikisha sehemu salama.

Binadamu huja na kuondoka na hata vyama vya kisiasa huja na kuondoka, tuipende nchi yetu kwa kuusema ukweli na kuondoa kila aina ya sheria ambayo ni ya kinyonyaji kwa watanzania wenzetu. Maisha yenyewe ni mafupi sana, hakuna haja ya kutesana, tuishi vizuri kwa kusimamia haki na kuhakikisha kila tunda na zao ambalo linalimwa nchi hii basi wananchi wote wanapata fursa ya kulila.
 
SG G.Msigwa is very right,

halafu the gentleman as days goes he becomes more brilliant politically speaking 🔥
Screenshot_20260516-003803~2.png
 
Ukishakua mwanaharakati unapoteza uraia au haki
 
Ila mafisadi, matapeli, majambazi, wahuni, wapiga dili, wauaji, watekaji, wezi wa kura, nk. Ndiyo wana haki ya kutuamulia siyo! Ok!!!
 
Back
Top Bottom