Msigwa: Ukimwi bado upo, Vijana wenzangu acheni kutembelea Rim

Msigwa: Ukimwi bado upo, Vijana wenzangu acheni kutembelea Rim

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali imewatoa hofu watanzania wote wanaoishi na virusi vya ukimwi, kuwa dawa zipo na serikali tayari imesha andaa bajeti ya fedha zitakazo tumika kuhakikisha watanzania wanapata dawa hizo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Serena, Dar es Salaam, Machi 1, 2025.

Pia amewahasa vijana kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kuisaidia serikali kutokomeza ugonja huu hatari.
 
Mmeanza kusema ukimwi upo Kuna hati hati yale makontena ya dawa yameishia njiani na zilizopo mmeshagawana!
 
Hapa vijana wa ovyo wa CHAPUTA watakuja kuunga mkono hoja. Kaka zao wa KATAA NDOA wamepigwa na kitu kizito
 
Back
Top Bottom