Serikali imewatoa hofu watanzania wote wanaoishi na virusi vya ukimwi, kuwa dawa zipo na serikali tayari imesha andaa bajeti ya fedha zitakazo tumika kuhakikisha watanzania wanapata dawa hizo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Serena, Dar es Salaam, Machi 1, 2025.
Pia amewahasa vijana kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kuisaidia serikali kutokomeza ugonja huu hatari.