Msigwa: Vijana msinitukane mtakamatwa tu, Polisi wameshakusanya zaidi ya Watu 80

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwa bahati mbaya wanaowaponza na kuwarubuni Vijana na kuwaingiza kwenye uvunjifu wa sheria ya Mtandaoni wamekuwa wakiwafuata Vijana kutoka familia duni, suala ambalo limekuwa likizigharimu familia nyingi maskini kuweza kumudu uendashaji wa kesi, akihimiza Vijana kutumia vyema mitandao ya kijamii ili kutojikuta katika mikono ya sheria.

Msigwa amebainisha hayo leo Alhamisi Mei 07, 2026 wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 21 cha Maafisa habari, mawasiliano, itifaki na uhusiano serikalini, kinachofanyika Mjini Njombe, Kusini Magharibi mwa Tanzania, akihimiza Vijana kujiepusha na matukio ya kufuata mkumbo ama kurubuniwa na baadhi ya wanaharakati wanaovunja sheria za nchi na kutoitakia mema Tanzania.

"Mimi huwa nakutakanwa sana kwenye mitandao ya kijamii na ninawaambia msinitukane mtapatikana, hawanisikii leo Polisi imekusanya wengi na mule ndani kuna watoto wa maskini kisa tu kaamasishwa. Leo teknolojia ilipofika huwezi ukatukana mtandaoni ukabaki salama, lazima utashikwa. Na bahati mbaya wanaowapotosha Vijana wanatafuta Vijana ambao wanatoka familia duni. Ukifanya uhalifu utakamatwa ukiwa ni mtumishi wa umma ama ukiwa si mtumishi wa umma utapatikana." Amesema Bw. Msigwa.

Kiongozi huyo pia katika hatua nyingine amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii nchini, akiwataka pia vijana kujiepusha na mikumbo kwani asilimia kubwa ya wanaohamasisha vijana kuvunja sheria za nchi hawapo nchini na pale hatua za kisheria zinapochukuliwa waathirika wakubwa wamekuwa ni watoto na Vijana wa kitanzania wanaotokea familia duni zisizokuwa na uwezo wa kusimamia kesi mahakamani dhidi ya Vijana wao waliovunja sheria kwa hamasa kutoka nje ya Nchi.
Wananchi ni maboss zenu,waheshimuni na wao watawaheshimu.
 
Ninalipongeza kwa dhati jeshi la polisi kwa kazi nzuri. Mnaosema kwamba hao wahalifu walikuwa wana sababu za kufanya hivyo ni vyema mkaenda mahakamani kuwatetea. Hakuna uhalali wowote wa mtu kutukana. KUTUKANA NI KOSA KISHERIA. Kama kitu unaona hakipo sawa kosoa kwa facts na sio kutukana. Maskini wengi wataangamia kwa ujinga wao wa kukubali kuhamasishwa na kina Sugu na Rugemeleza Nshala kutukana.
Juzi nimemdharau sana huyo Msigwa, anasema 99% walitoa michango ya kumtia moyo, ila 1% ndio walimtukana! Inawezekana vipi 99% wasikutukane, ila uumizwe na 1% ya watukanaji? Ukiona unatukanwa ujue kabisa hauko sawa kiuongozi. Hayo ndio madhara ya kupora chaguzi wakati hukubaliki. Na hizo mahakama zingekuwa huru watu wangeenda vilevile kufafanua hayo yanayoitwa matusi.
 
Kwahyo hao 80 wanauliwa au inakuwaje, maana Kuna ambao waliuliwa bila kutukana hiyo oct.29.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwa bahati mbaya wanaowaponza na kuwarubuni Vijana na kuwaingiza kwenye uvunjifu wa sheria ya Mtandaoni wamekuwa wakiwafuata Vijana kutoka familia duni, suala ambalo limekuwa likizigharimu familia nyingi maskini kuweza kumudu uendashaji wa kesi, akihimiza Vijana kutumia vyema mitandao ya kijamii ili kutojikuta katika mikono ya sheria.

Msigwa amebainisha hayo leo Alhamisi Mei 07, 2026 wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 21 cha Maafisa habari, mawasiliano, itifaki na uhusiano serikalini, kinachofanyika Mjini Njombe, Kusini Magharibi mwa Tanzania, akihimiza Vijana kujiepusha na matukio ya kufuata mkumbo ama kurubuniwa na baadhi ya wanaharakati wanaovunja sheria za nchi na kutoitakia mema Tanzania.

"Mimi huwa nakutakanwa sana kwenye mitandao ya kijamii na ninawaambia msinitukane mtapatikana, hawanisikii leo Polisi imekusanya wengi na mule ndani kuna watoto wa maskini kisa tu kaamasishwa. Leo teknolojia ilipofika huwezi ukatukana mtandaoni ukabaki salama, lazima utashikwa. Na bahati mbaya wanaowapotosha Vijana wanatafuta Vijana ambao wanatoka familia duni. Ukifanya uhalifu utakamatwa ukiwa ni mtumishi wa umma ama ukiwa si mtumishi wa umma utapatikana." Amesema Bw. Msigwa.

Kiongozi huyo pia katika hatua nyingine amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii nchini, akiwataka pia vijana kujiepusha na mikumbo kwani asilimia kubwa ya wanaohamasisha vijana kuvunja sheria za nchi hawapo nchini na pale hatua za kisheria zinapochukuliwa waathirika wakubwa wamekuwa ni watoto na Vijana wa kitanzania wanaotokea familia duni zisizokuwa na uwezo wa kusimamia kesi mahakamani dhidi ya Vijana wao waliovunja sheria kwa hamasa kutoka nje ya Nchi.
Aache ujinga
 
Kama Anafahamu Ametukanwa,,Kuna Namna Na Yeye Aliwatukana Hao Watukanaji,,,Huwezi Kutukanwa La Hasha Kama Na Wewe Si Mtukanaji...
###....KUTUKANAOYEEHH..!!!###(in Hon;Makongoro Nyerere's Voisi)
​
 
Mtu mwenye akili ndogo huangaika na matokeo, mtu mwenye akili kubwa hungaika na sababu
 
Kama Anafahamu Ametukanwa,,Kuna Namna Na Yeye Aliwatukana Hao Watukanaji,,,Huwezi Kutukanwa La Hasha Kama Na Wewe Si Mtukanaji...
###....KUTUKANAOYEEHH..!!!###(in Hon;Makongoro Nyerere's Voisi)
​
Juzi tu aliwaita watu nguchiro
 
Mbona kama kalichukulia hili so personal?

Watu wakikutujana Msigwa, Ni serikali inatukanwa sio wewe, Sijui unapanick nn.
 
Back
Top Bottom