Miradi yote mikubwa, kama ujenzi wa barabara, reli, hospitali, tunajenga kwa pesa ya misaada na mikopo. Makusanyo ya ndani yanaishia kwenye mishahara na posho za mafisadi. Anaposema kuwa tutatumia hela yetu, yaani bila misaada wala mikopo, ina maana hakutakuwa na miradi ya maendeleo?
Mwulizeni, ni kipande gani cha barabara angalao cha kuunganisha tu mkoa mmoja na mwingine, kilijengwa kwa makusanyo ya ndani. Hata reli tu, ni wapi tumetumia pesa ya ndani angalao kuunganisha makao makuu ya mkoa mmoja na mwingine.