Msijemwambia Pele kuwa anafananishwa na Messi

Msijemwambia Pele kuwa anafananishwa na Messi

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Jenga picha Pele Mchawi wa Mpira, Huyu katika Biblia ya Soka ni Moses. Ni nabii mkubwa sana. Just imajini akiwa kitandani aambiwe Lione Messi anafananishwa naye. Atakata roho hapo hapo kwa uchungu.

Msije mwambia jambo hili. Please sisi tuliokuwepo toka zamani tunao heshimu mpira na watu wake. Tuombee asije akasikia kuna vijana wanamkosea adabu kiasi hiki.

Nimeumia sana. Unaanzaje kumlinganisha Messi na Pele? Ni kuukosea mpira wa Miguu. Ni kuwatukana wahenga,mababu na watu wa kale wakubwa katika koo zetu.

Miaka ya nyuma mtu angechapwa viboko 100 na akiwa anachapwa akifuta wanaanza upya. Tena hadharani kabisa. Halafu angetengwa kwa muda usiopungua miezi mitatu akakae huko katikati ya pori la Mikumi, Serengeti au Manyara. Halafu arudi kuja omba radhi.

Nyie dot com. Mtaenda motoni vibaya sana. Pele msimfananishe na Messi. Hata kidogo. Msishiriki dhambi kama hii ambayo inakwepeka kirahisi tu. Na kama hata uliwahi fananisha watu hawa nenda katubu. Na utuombe radhi sisi kizazi cha 60s na kuendelea kasoro 90s na kuendelea.

Jamani.... Kwa nini mnapenda kwenda motoni kwa mambo yanayoepukika. Pele nakuomba uwasamehe hawa watoto. Hawajui wasemalo. Tusamehe na sisi kwa kuwazaa watoto wa namna hii baba. Tutajirekebisha...na tutajitahidi sana kuwaelewesha. Zaidi zaidi tutawaambia watu watumie kinga.

TAHADHALI.

MSIMFANANISHE PELE NA MAMBO MEPESI MEPESI.
 
Ngoma ikilia Sana hupasuka , watu wanatumia nguvu nyingi kumpambania Pele , so sad record zake zpo static huku Messi akiwa dynamic, mtakubali tuu dogo wa miaka 35 , anajitengenezea kibanda chake
 
Ngoma ikilia Sana hupasuka , watu wanatumia nguvu nyingi kumpambania Pele , so sad record zake zpo static huku Messi akiwa dynamic, mtakubali tuu dogo wa miaka 35 , anajitengenezea kibanda chake
Dynamic.. sawa. Dogo wa Miaka 35 ... ngoja tusubiri "dogo" huyu avunje rekodi ya kubeba kombe la dunia zaidi ya mara 3.
 
Mkiulizwa alifanya kipi cha kumzidi Messi mnakimbia ohh World cup , kachukua mnaanza ohh alichukua tatu wakati kwenye hizo tatu moja alicheza akaishia mechi ya pili tu , Yaani Brazil haikumtegemea yeye ichukue ubingwa.Hayo mawili nayo aliyocheza hadi fainali hakuwa Best scorer wala best assister sasa huo ubora wake unaoimbwa eti asifananushwe sijui ni upi hasa.
 
Brazil haikumtegemea Pele?

Mbona pundits wengi wanasema Argentina ilimtegemea Di Maria na Kipa Martinez nasiyo Messi.
 
Mkiulizwa alifanya kipi cha kumzidi Messi mnakimbia ohh World cup , kachukua mnaanza ohh alichukua tatu wakati kwenye hizo tatu moja alicheza akaishia mechi ya pili tu , Yaani Brazil haikumtegemea yeye ichukue ubingwa.Hayo mawili nayo aliyocheza hadi fainali hakuwa Best scorer wala best assister sasa huo ubora wake unaoimbwa eti asifananushwe sijui ni upi hasa.
Hata tukitoa trophies bado Pele alikua ni habari nyingine
 
Mkiulizwa alifanya kipi cha kumzidi Messi mnakimbia ohh World cup , kachukua mnaanza ohh alichukua tatu wakati kwenye hizo tatu moja alicheza akaishia mechi ya pili tu , Yaani Brazil haikumtegemea yeye ichukue ubingwa.Hayo mawili nayo aliyocheza hadi fainali hakuwa Best scorer wala best assister sasa huo ubora wake unaoimbwa eti asifananushwe sijui ni upi hasa.
Kwa hiyo ubora wa Messi unaoimbwa dhidi ya CR7 ni kwa sababu ya magoli na assist?
 
Huyu pigmiss ambae anakuzwa na vyombo vya habari ambavyo vinahongwa na makampuni yanayomdhamini ndio anafanishwa na PELE?.

NB: UKITAKA KUJUA KUKUZWA (KUBEBWA) KWAKE REJELEA PENALTY ZA MCHONGO KWENYE WC NA COPA AMERICA KUFANYIKA MARA 4 KWENYE MIAKA 8 HAYA YOTE YAMEFANYWA ILI DWARF ASHINDE HAYO MAKOMBE NA KWA UFAHAMU ZAIDI REJELEA CHANZO CHA FIFA KUVUNJA USHIRIKIANO NA BALLON D'OR.

MESSI MOST OVERRATED FOOTBALLER EVER.
 
FB_IMG_16722988473614754.jpg

Mzee kakubali yaishe
 
Messi ni mchezaji mzuri sana, Ronaldo hamfikii kiuwezo ila katika WC ya Qatar kuna namna Messi na Argentina kwa ujumla walibebwa.

Penalty waliyopewa wakicheza na Nerthelands haikustahili kuwa penalty

Messi ana uwezo ila bado hajamfikia Pele wala Maradona
 
Huyo mesi wao kombe la dunia lenyewe imetumika nguvu kubwa mno kumtengenezea mazingira ya kulichukua. Aishukuru sana fifa kwa kumbeba na kumpa magoli ya offside

Hivi ukiombwa utoe ushahidi wa hilo unalodai, utatoa? Kumbe hata kwenye matuta pia kuna kubebana!! Penda usipende messi ni zaidi ya babu.. statistics zinajieleza..

Swali! Mbali na world cup, nini kingine alichomzidi King Messi na Diego Armando?
Njoo na data zilizo shiba, na sio kuniletea world cup wakati hata Giroud, de lima na iniesta wanayo pia.
 
Back
Top Bottom