Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
MISIBA NA UMJINI WA WATU WA MJINI.
Vijana wa mjini ninawaomba sana bamyiitu, mkienda kijijini msilete umjini wenu kwenye mambo ya msingi. Jaribuni kufanya yale ya utaratibu wa kijijini. Salimia, nyenyekea, piga stori, chekesha, yaani fanya yote yafaayo kwa jamii ya wanakijiji uliowakuta pale kijijini. Vaa uhusika wote wa uanakijiji. Hautapungukiwa kitu.
Ukifika kijijini, pita nyumbani kwa watu wa pale kijijini wasalimie. Pita kwenye nyumba zilizopata misiba ili kuwapa salamu ya pole, nenda kawaambie "poleni na msiba". Wasalimie waambie "ndaga mwasyilile". Kufanya haya yote hakukuondolei umjini wako, yaani hakukupunguzii kitu.
Kukitokea msiba wakati upo pale shiriki, hudhuria msibani. Kama wewe ni mkaka ukiona watu wa umri wako ndo wanaofanya shughuli ya kuchimba kaburi nawe shiriki kuchimba kaburi, chimba. Kama ni mdada shiriki hata kupikapika. Kufanya hivyo hakukupunguzii umjini wako, yaani hakukupunguzii kitu.
Muda wa chakula ukifika hakikisha unashiriki. Usikipuuze kile chakula kwasababu ya kuwa kina makabeji yaliyopikwa hovyo, wewe kula tu. Na kwa wale wa kwetu Unyakyusani: hakikisha zile kande (ingaati) zetu zile unazila kisawasawa. Usiseme "hapana sili nimeshiba", kula. Kufanya haya hakuuondoi umjini wako, yaani hakutakupunguzia kitu.
Ninataka kumaanisha nini?
Tukutane siku nyingine, twaganile isiku ilingi...
@ Lusako