Msilete Umjini wenu mkija kuzika kijijini

Msilete Umjini wenu mkija kuzika kijijini

Kwanza waambie hao wamama wa msibani waache kihelehele chao cha kukimbilia kupanda magari kuelekea makaburini

halafu wakifika huko hawana cha kufanya wanakaa tu kusubiria wanaume ambao wamekuja kwa miguu baada ya kukosa nafasi ya gari ndio waje wazike

Pili ongea vizuri na mapasta wajue namna ya kucheza na muda kwenye mahubiri yao pale makaburini.

Kuna siku tulitaka tumuachie maiti pasta mmoja baada ya kuona anaji less. Msimu wa kifuku wingu limetanda tunaona mvua inakuja kutoka nga'mbo karibia na makaburini eti ye bado anaendelea kunena kwa lugha

Tatu waambie serikali yako ya mitaa kua waheshimu muktadha wa tukio husika. Wasitumie msiba kama njia ya wao kutangaza majitoleo ya kijiji tukiwa huko makaburini.
 
Nyie ndo mnawaharibu, hawachimbi kaburi, chakula wanapewa chao kulala sehemu maalum na mnawaita watu wa darisalama
 
Sasa nyie wa Vijijini si hiyo mgeuze kuwa fursa?. Mgeni njoo Mwenyeji apone.

Hakikisheni wakija kwenye eneo husika zaidi ya milioni moja inabaki hapo, maduka ya reja reja, vi grossary, viduka vya e pesa n.k.
 
Ni nyie mkija mjini muache kulalamika chakula kidgo tuna ishi kwa budget uku
Umenikumbusha mara ya kwanza kufika mjini kakasongwa kaugali nikafikiri labda kuna mtoto anasongewa alafu wakwetu utasongwa tena,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ebwanaee, nikashngaa hako kaugali kanatengwa mezani na sahani kila mtu ya kwake madume kama 3 hivi eti ndio mlo wa mchana huo.
.
Nikajipa moyo labda jioni itakuwa afadhali.
Dadek jioni ukaletwa ubwabwa kwenye kihotport eti ndio mlo wa watu kama 4,

Nilitamani kulia.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
ni kweli ila na wao wawwe waelewa,siku nimezama kijijini kurekebisha kaburi la mdingi toka mbali sana na muda hauruhusu kukaa sana nilikua na siku 3 tu,nafika Mbeya mjini usiku huhu zikatumwa taarifa za msiba pale kijijini...
Hilo ndio kosa lako aliekwambia msibani wanaaga nani, we unazunguka nyuma unachomoka ki style unaenda kupiga usingizi kisha unarudi ki style hivo hvo
 
Hivi watu wanao kaa wapi ndio wanaitwa wa mjini ?


Nisije nikahesabu hapa kwetu katengele ni mjini kumbe kijijini
 
Siwezi kubadili tabia yangu eti tu niwafurahishe watu never ever..

Vyakula vingi vya vijijini vinaandaliwa kwenye mazingira ambayo sio masafi, so siwezi kula, mwaka jana nimeenda nimeshiriki msiba kila kitu lkn kula ni no, kunyenyekea sijui kusalimia na kupita kila nyumba hayo siyawezi
 
Waambie na hao wavijijini waache kusema sema hivyo ukipita wanasema,wanakutumbulia macho Kama wameona sijui nani kapita! Ukisema uchimbe kaburi ukishika sururu tu wanaanza kusema vilugha vyao! Waambie na wenyewe wabadilike..
Huyu hawajui watu wa vijijini most of them kwanza hawatupendi sisi watu wa mjini, utasikia " yaan linaringa" na hapo hakujui
 
Wakaapo wenyeji usihangaike weka kitambaa eti nguo zitachafukaaa.... [emoji23]
Nguo zikichafuka usikimbilie fuaa, [emoji23]
Ikipita rubisi/ulanzi/mbege/gongo/buza etc kwenye kata/kikombe we piga pafu mojaaa mpasie na mwenzoo, hapo mwenge hauvuki kijiji!!! eti we wakuja kutoka mujini unataka utengewe special yako [emoji485][emoji481]....dadekiii
Kushare kikombe kimoja ndo kabisa siwezi

Ha ha ha, Kuna kitu umenikumbusha ila watu wa vijijini huwa wanafurahisha sana
 
Back
Top Bottom