Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Muda mchache kabla ya kuondoka nchini, Aliyekuwa mgombea uraisi wa kupitia Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu alifanya mahojiano mafupi na vyombo vya habari na kuseama kuwa uchaguzi uliopita ni uchaguzi ambao uliovurugwa na kuharibiwa sana, amesema kuwa katika vikao halali vya chama vya kamati kuu wameutathmini uchaguzi huo na kuona kuwa hakukuwa na uchaguzi pale bali uchafuzi. Kwa hiyo kutokana na uchafuzi huo chama hakiwezi kushiriki kuhalalisha uharamu huo. Amesema kwa hiyo Chadema haiwezi kuchukua viti maalum vilivyotokana na mchakato haramu, Amesema kuwa haramu ni haramu na haiwezi kuwa halali!
Pia ndugu Lissu amesema kuwa kwa mujibu wa sheria anayepeleka majina ya viti maalum ni katibu mkuu wa chama, kwa hiyo mtu yeyote atakayepeleka majina NEC kwa ajili ya viti hivyo kinyume na katibu mkuu wa chama bado atakuwa anafanya kitu ambacho siyo sawa kisheria.
Kwa maelezo zaidi unaweza kumsikiliza hapa: