LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: CHADEMA wameweka mawakala 55 katika vituo 666

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂
Na wewe vitu vingine huwa unavimeza kishabiki sana....kuwa na mawakala wachache haimaanishi zoezi halina kasoro....hebu angalia ushahidi hapo chini wa watoto kutakiwa kuandikishwa

View: https://x.com/HildaNewton21/status/1846163076338319515
 
14 October 2024
Arusha, Tanzania

VITUO VYAONGEZWA GHAFLA KUTOKA 154 HADI ZAIDI YA VITUO 462 ILI VYAMA VIKOSE MAWAKALA

View: https://m.youtube.com/watch?v=PFpNvDqeong
Vyama vilijipanga kuwa na mawakala kusimamia vituo 196, lakini kisiri CCM wakaambiwa mapema kabla ya vyama vingine kuambiwa dakika za lala salama ...

Kuongezwa kinyemela kwa vituo kwa zaidi ya asilimia 300 yaani toka ile ya awali 154 hadi 462 kwa mahesabu vimepindukia mara 3 kulliko vya awali ni kuwa yule DC wa Loliondo aliposema tumeshamaliza michezo ndiyo hii michezo ya CCM na serikali yake.

Toka maktaba:

DC WA LOLIONDO ATUMBULIWA KWA KUTOA SIRI ZA CCM KUSHINDA UCHAGUZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=M4rve_wh2IY
 
Ccm ndio Ina baraka ya Dola kutawala!

Wapinzani hasta wapate kura nyingi kuliko CCM Bado hawana baraka za Dola hivyo hawatatangazwa washindi!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂
Kazi ipo kwa msimamizi mkwe wa rais ambaye pia ni kada na mdau wa uchaguzi aliyesema CCM lazima ishinde kwa gharama yeyote
 
Tulishasemaga siku nyingi sana hiki chama cha X hakina wanamikakati na chama hakiwezi kutoba bila ya uwepo wanamikakati na sio kutegemea wapiga kelele mitandaoni na kuongea na waandishi wa habari kuli uchao(Lema)
Mkakati wa kwanza ni ukusanyaji wa fedha wakuweza kuendesha chama cha, mkakati huo hawana, Wanatumia fedha nyingi kuandaa mikutano na maandamano wakati fedha nyingi zinatakiwa kipindi kama hiki.

Wamenunua Ofisi ghali mikocheni wakati wangeza kupata Eneo kubwa tu kigamboni nakujenga ofisi pamoja na vitega uchumi kama maduka ofisi na parking za kulaza magari. Sioni dalili zozote za wapinzani kushinda kwani wananchi wamepoteza imani kabisa na vyama hivi.

Pamoja na kwamba CCM inawatendea sivyo ndivyo lakini wananchi wanawaona wapinzani kama ni mandumi kuwili.Nadhani ni kweli sasa mda umefika wakati wa CDM kujipanga upya. Unaweza kujiuliza kwanini watu wengi wanalia na CDM, ni kwasababu wananchi wengi wamejenga matumaini juu ya hichi chama ilq kimekuwa kikizidiwa ujanja na mbinu kila siku huku kikibaki kiki lalamika
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂

Yaani Tanzania wizi ni kama vile umehalalishwa na ni sehemu ya maisha ili mradi unaweza kujustify kijanjajanja.

Kwa nchi ambazo hakuna uhuni uhuni kwenye mambo kama haya huhitaji mawakala wa vyama kusimamia uandikishaji. Wanachoweza kufanya ni rondom verification tu kuwa zoezi linaenda vizuri. Imagine kama kila chama kitapeleka mawakala kila kituo si itakuwa ni vurugu moja kwa moja. Yaani, kila kituo kitakuwa na mawakala 17 .... Seriously!
 
Tulishasemaga siku nyingi sana hiki chama cha X hakina wanamikakati na chama hakiwezi kutoba bila ya uwepo wanamikakati na sio kutegemea wapiga kelele mitandaoni na kuongea na waandishi wa habari kuli uchao(Lema)
Msimamizi wa uchaguzi ni vyama viwili tu vimeweka mawakala Chadema na Ccm vingine vimeungana na ccm.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂
Msimamizi mwenyew ni mwanachama wa ccm halafu utegemee haki au uhuru kwenye uchaguzi. Itakuwa ndoto.
 
Back
Top Bottom