LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: CHADEMA wameweka mawakala 55 katika vituo 666

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwandishi Wetu

DODOMA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.
 
Vyama vya upinzani vipo 18, je vingine vimeweka?
Elewa mantiki ya Msimamizi wa Uchaguzi. Leo John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema amekaririwa akisema CCM HAIJAWEKA mawakala wake kwenye vituo isipokuwa wao Chadema tu. Sasa hayo ndio majibu anayopata. Mimi nipo Mwanza Jiji ninajua idadi ya mawakala wa CCM katika vituo vyote ndio maana niliposikia taarifa yake leo nikacheka sana na kununua K Vant kubwa na kichanganyio cha Tonic! Ahahahahaha!!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂
Hivi uchaguzi huru na haki ni sharti kuwepo mawakala? Na wasipokuwepo ccm inaona tayari washashinda?
 
..tumeweka msisitizo mkubwa kwenye mawakala kwasababu ya FIGISU zinazofanyika ktk vituo vya kupiga na kuhesabu kura.

..vyama vidogo visivyopata RUZUKU kabisa tunategemea vitashiriki vipi uchaguzi kwa utamaduni huu tunaoujenga?
Kumbuka Dodoma ni ngome ya CCM
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂

Chama Cha X zamani Twitter mnaona mnavyopuuzwa? Tuliona kwenye maandamano ya kutaka kuleta vurugu Hadi huku mtaani.

Mafuriko ya mitandaoni Huwa yanawadanganya sana na bahati mbaya hamjifunzi.Watu wenye uwezo wa kununua bando hawafiki hata 5% ya Watanzania wote,mkiangukia Pua Utasikia tumeibiwa 😂😂😂
Hichi Chama kina uhusiano na shetan? Kwa nn kimeweka no.ya shetan (namba ya mnyama?) ufunguo 13:18 ?
 
Kumbuka Dodoma ni ngome ya CCM

..pia Ccm ina MABILIONI inayoyapata toka kwenye ruzuku kufanya shughuli zake.

..Chadema hawana rasilimali, na mapesa ya kushindana na Ccm kila mahali.
 
Yaani Tanzania wizi ni kama vile umehalalishwa na ni sehemu ya maisha ili mradi unaweza kujustify kijanjajanja.

Kwa nchi ambazo hakuna uhuni uhuni kwenye mambo kama haya huhitaji mawakala wa vyama kusimamia uandikishaji. Wanachoweza kufanya ni rondom verification tu kuwa zoezi linaenda vizuri. Imagine kama kila chama kitapeleka mawakala kila kituo si itakuwa ni vurugu moja kwa moja. Yaani, kila kituo kitakuwa na mawakala 17 .... Seriously!
Mimi nakumbuka miaka ya 90 wanafunzi ndiyo walikuwa wanatumika kusimamia uchaguzi na kuhesabu kula tulikuwa tunalipwa mia tano miatano wala hakukuwa na vurugu wala nini wala gharama kubwa za maandalizi. Mimi nadhani turudi tu kwenye mfumo wa chama kimoja mfumo wa vyama vingi umetushinda, mfumo huu unalitia taifa gharama kubwa kisha tunapata viongozi wabovu. Tuhakikishe tunarudi mfumo wa chama kimoja haraka iwezekanavyo na kwa upande wa Raisi kuwe kunakuwa na mgombea mmoja tu. Huku picha ya mgombea na huku picha ya nyudo siyo yule nyundo Aliyebaka.
 
Kwanini kuwe na mawakala wa vyama ikiwa uchaguzi inafuata taratibu zote za kisheria, na unaamuliwa kwa haki?

Yaani ni kama tumejenga imani kwamba bila kusimamiwa na mawakala uchaguzi hauwezi kufanyika kwa kufuata taratibu.
Kuna ujinga mwingi sana katika kujitawala, na hii changamoto yapaswa kuondolewa kwa ujenzi wa taifa imara.
Kuandikisha wapiga kura siyo kazi ya vyama, ni kazi ya watumishi wa Uma wanaotumika kwa mujibu wa sheria.
Kimsingi ilitakiwa orodha ya wananchi iwepo muda wote na siyo kuandikisha wakati wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom