PostGE2025 Msimamizi wa uchaguzi Siha: Mawakala wa uchaguzi wameridhishwa na mchako wa uchaguzi

PostGE2025 Msimamizi wa uchaguzi Siha: Mawakala wa uchaguzi wameridhishwa na mchako wa uchaguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jumla ya wapiga kura 88,000 walitarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa kumchagua Mbunge wa Jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro, uliofanyika jana Desemba 30, 2025.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Siha, Marko Masue, amesema jumla ya vituo 230 vya kupigia kura vilitengwa kwa ajili ya zoezi hilo, akieleza kuwa mchakato mzima wa upigaji kura umefanyika kwa utulivu na kufuata taratibu, huku Mawakala wa Vyama vyote vya Siasa wakiridhika na mwenendo wa Uchaguzi.

Akizungumza baada ya zoezi la upigaji kura, Masue amesema Vyama vya Siasa vimeonesha ushirikiano tangu kuanza kwa mchakato wa uteuzi wa wagombea hadi kipindi cha kampeni.

“Tunashukuru Vyama vyote vya Siasa vimekuwa rafiki tangu mwanzo wa mchakato. Matarajio ni kuwa hakutakuwa na changamoto katika kupokea matokeo, kwani mawakala wamekuwa huru kusimamia zoezi na wameona haki ikitendeka. Sitegemei kuona mtu akikataa matokeo; hali ni ya amani kabisa,” amesema Masue.

Ameongeza kuwa wananchi wamejitokeza kupiga kura huku wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi, hususan kilimo, akibainisha kuwa hali nzuri ya hewa imechochea ushiriki mzuri wa wananchi katika zoezi hilo.

Masue ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura, hatua inayofuata ni kuhesabu kura na kutangaza matokeo, zoezi linalotarajiwa kufanyika leo Desemba 31, 2025

Katika uchaguzi huo, Vyama Viitano vya siasa vimeshiriki, ambavyo ni CCM, ACT-Wazalendo, Makini, NRA na SAU.

Uchaguzi mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Daudi Ntuyehabi, aliyefariki dunia Oktoba 7, 2025, baada ya kushambuliwa wakati wa tukio la ugomvi.

1767170055795.png
 
Akizungumza baada ya zoezi la upigaji kura, Masue amesema Vyama vya Siasa vimeonesha ushirikiano tangu kuanza kwa mchakato wa uteuzi wa wagombea hadi kipindi cha kampeni.
CHADEMA ndio imeshasahaulika tena. Hata Ile NRNE ndio imekufa kabisaaaaaaaa! Maisha haya... acheni tu.
 
Back
Top Bottom