Msimamo : Sitashiriki dua ya kuiombea Taifa Stars iliyoitishwa na Makonda siku ya Jumamosi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paulo Makonda amejipachika uongozi wa Timu ya Taifa , haijafahamika malengo yake , bali kinachofahamika ni kwamba Mungu hataniwi , na kwa kadiri ninavyomfahamu mtu huyu hana uadilifu wa kuhamasisha wananchi kumuomba Mungu kwa ajili ya Taifa Stars au jambo lolote

Sitashiriki dua aliyoihamasisha maana nafahamu kwamba Mungu hatoipokea .

Ujumbe wangu huu haumaanishi kwamba siungi mkono timu ya Taifa langu , lakini ni wazi kwamba sitaki unafiki kwenye masuala yanayomhusisha Mwenyezi Mungu

Naomba kuwasilisha
 
Hata hivyo Mungu ni wa wote hawezi kuipendelea Taifa Stars na kuziacha nyingine kwakuwa na wao wana muomba Mungu huyo huyo hivyo hizo dua ni za kumpotezea Mungu muda. Na hapa ndipo huwa tunashindwa badala ya kujiandaa vizuri tunaanza kumtaka Mungu ndiye atufanye tushinde! Huo ndio upumbavu wa viongozi wetu. Sasa angalia yule mwingine naye aliyeokotwa pale jalalani eti ataleta watalaamu kutoka nje wa kuja kupanga ratiba ya ligi kuu!
 
Watu wanamchulia Mungu kirahisi sana. Huwa najiuliza kwa mfano Misri au Israeli wanamwagalia jangwani kuzalisha na kupata ziada. Sisi wengine tumezungukwa na maji, mito na vijito lakini tunaomba mvua inyeshe. Hivi huyo Mungu haoni? Akitulinganisha na wenye majangwa si anatuhesabu kama wazembe tu! Michezo hivyohivyo, kila siku harambee na kamati za dharura na sasa hadi maombi. Tutabadilika lini?
 
Hata hivyo Mungu ni wa wote hawezi kuipendelea Taifa Stars na kuziacha nyingine kwakuwa na wao wana muomba Mungu huyo huyo hivyo hizo dua ni za kumpotezea Mungu muda. Na hapa ndipo huwa tunashindwa badala ya kujiandaa vizuri tunaanza kumtaka Mungu ndiye atufanye tushinde! Huo ndio upumbavu wa viongozi wetu. Sasa angalau yule mwingine naye aliyeokotwa pale jalalani eti ataleta watalaamu kutoka nje wa kuja kupanga ratiba ya ligi kuu!
niliposikia taarifa ya kuleta mtaalam kutoka nje ili kupanga ratiba nilicheka sana !
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paulo Makonda amejipachika uongozi wa Timu ya Taifa , haijafahamika malengo yake , bali kinachofahamika ni kwamba Mungu hataniwi , na kwa kadiri ninavyomfahamu mtu huyu hana uadilifu wa kuhamasisha wananchi kumuomba Mungu kwa ajili ya Taifa Stars au jambo lolote

Sitashiriki dua aliyoihamasisha maana nafahamu kwamba Mungu hatoipokea .

Ujumbe wangu huu haumaanishi kwamba siungi mkono timu ya Taifa langu , lakini ni wazi kwamba sitaki unafiki kwenye masuala yanayomhusisha Mwenyezi Mungu

Naomba kuwasilisha

TUMELOGWA.
Na Thadei Ole Mushi
PhD Holder Harrison Mwakyembe amewataka watanzania waichangie timu ya taifa ili wapate motisha wa kucheza mpira. Hii ndio Tanzania na watanzania wenyewe ndio sisi tuna Tabia kama ya patasi hatuendi wenyewe mpaka tugongwe kwa nyuma.
Sikia....
AFCON 2019 ina wadhamini lukiki ambao wanahakikisha timu zote pale misri zinapata mahitaji yao yote, haya ndio mashindano ya juu kabisa kwa ngazi ya mataifa kwa bara la Africa. Kwa kutambua hivyo makampuni makubwa yamejitokeza na yamemimina fedha ya kutosha kuendesha mashindano. Makampuni rasmi ni kampuni la mafuta la TOTAL, Kampuni la Digital payments la VISA, Kampuni la Magari YAMAHA, Kampuni la Simu la ORANGE, Kampuni la matairi la CONTINENTAL, Kampuni la madawa la GILEAD, na Kampuni la vyakula la TEMMY`S. Hawa ndio official sponsors kila kitu kipo under Control.
Si hivyo tu.....
Timu zote zilizopo Misri zina vyama vyao vya mpira toka nyumbani. Vyama hivi vimejiandaa na timu zao toka na hata kabla ya kufuzu kwa timu zao. Hapa kwetu tuna TFF ambayo ilipata gawio la FIFA na Gawio la match zote (Gate Collection) kwa ligi zote nchini.
Si hivyo tu Bali.....
Timu zote katika nchi zao zina wizara ambazo zinashughulikia michezo huko nako wamejipanga toka timu zao zilivyofuzu. Fifa nao wametoa gawio kwa CAF ili kuendesha Haya mashindano.
Kubwa kuliko.....
Timu yetu ina sponsor wake ambaye ni Serengeti lager naye anamimina mamilioni kwa vijana......
Kupitia hayo yote sioni sababu ya watanzania kuchangishwa tena kwa ajili ya kusapoti timu.
Hoja ya MOTISHA.
Wachezaji wote waliopo pale misri mentality zao ni kunyakua kikombe hii ni motisha ya kwanza. Yaani kama kuna mchezaji anasubiri fedha zichangwe ndio acheze hatutafika mbali. Nani hataki kuweka historia kuwa alichukua Afcon 2019? Wachezaji wote pale Misri nia yao ni kucheza final na kuvaa medal za dhahabu.
Pili ni kitita cha fedha watakachoondoka nacho, bingwa anaondoka na $4.2 milioni ambazo ni sawa na bilioni karibia kumi (9,659,580,000). Unataka wapewe motisha gani nyingine?
Sisi waalimu tunajua utaratibu wa motisha kuwa ni kuimarisha Tabia Flani iliyotokea au kukomesha tabia flan isijirudie. Sasa taifa Stars haijacheza match hata moja tumeanza kuwachangia. Jukumu lao la pili ni kuwinda hizo dola za mshindi wa kwanza.
Hata hivyo wafahamu kuwa kuanzia robo final kuna kitita cha fedha watapata. Kwa nn wasiwaze hizi fedha?
Motisha ya tatu ni mchezaji kujiuza yeye binafsi, pale alipo Samata wala hawazi fedha anachowaza ni kuchukua ubingwa ili aandike historia yake binafsi na ajiuze zaidi kimataifa. Wachezaji wote pale Misri kichwani mwao hilo lipo, kwao hii ni motisha tosha.
Kuhusu hamasa!!!
Tumewekeza mno mbwembwe nje ya uwanja badala ya vitu technically, timu tumeshaimilikisha kina Makonda tumeitoa kwa wananchi sasa hivi wanakimbia nayo wanaoitwa kamati ya kuhamasisha timu ishinde. Maajabu kama haya unaweza kuyaona tu Tanzania. Kilichotokea watanzania wamekaa pembeni wamewaachia kamati ifanye mambo yao.
Sioni impact ya hiyo kamati ikibadilisha matokeo ndani ya uwanja. Kwamba tukishavaa hayo madera yaliyoshonwa kwa bebdera za Taifa ndio tutapata matokeo? Hivi ni vituko vya aina yake.
Nasikia TBC hawataonyesha Haya mashindano, yaani timu ya taifa inashiriki jambo kubwa hivi halafu Chanel ya Taifa wala haina habari inakimbizana na Chereko Chereko. Wanajua ni shilingi ngapi wanapoteza hapa za matangazo?
Je kwa watanzania ambao hawana kingamuzi cha Azam wataenda vibanda umiza kila Siku? Je wale ambao hawana uwezo wa kulipia vingamuzi vyao hawataona?
Dr Mwakyembe unafeli wapi mheshimiwa mbona nilikuwa nakuamini sana? Master planner wa wizara ni nani kwa sasa ni wewe au katibu mkuu au Mh Makonda? Maana kila mahali nakuona naye....naona mmeshampa na cheti cha kutambua mchango wake Haya mngeyafanya mwisho wa mashindano haraka ya nn?....
Tumelogwa
Ole Mushi
0712702602
Image may contain: 3 people, people standing
 
Sijawahi kuafiki yeye kujihusisha na stars, Mungu atatenda kulingana na matendo yake, tff wamekwama sana,ndo maana kila mtu anaitakia stars mabaya
 
Hivi kwanini Mwakyembe asivuliwe uwaziri ?
 
Sijawahi kuafiki yeye kujihusisha na stars, Mungu atatenda kulingana na matendo yake, tff wamekwama sana,ndo maana kila mtu anaitakia stars mabaya
Tatizo kubwa ni Mamluki kama hawa akina Makonda
 
We’re on the same page Mkuu. I have made the decision to stay far away from those hooligans and killers.,

Back
Top Bottom