Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paulo Makonda amejipachika uongozi wa Timu ya Taifa , haijafahamika malengo yake , bali kinachofahamika ni kwamba Mungu hataniwi , na kwa kadiri ninavyomfahamu mtu huyu hana uadilifu wa kuhamasisha wananchi kumuomba Mungu kwa ajili ya Taifa Stars au jambo lolote
Sitashiriki dua aliyoihamasisha maana nafahamu kwamba Mungu hatoipokea .
Ujumbe wangu huu haumaanishi kwamba siungi mkono timu ya Taifa langu , lakini ni wazi kwamba sitaki unafiki kwenye masuala yanayomhusisha Mwenyezi Mungu
Naomba kuwasilisha