Msimamo wa Bunge ni upi kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo?

Msimamo wa Bunge ni upi kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo?

Rejea maoni ya Spika kuhusu Mh. Rais (Mwendazake) kushauriwa vibaya.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Je, msimamo wa bunge kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni upi?

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Bunge lenyeww ni hili linaloongozwa na Ndugai!! Ndugai ni Bendela fata upepo hana msimamo hata kidogo. Kumbuka alisema ana faili Milembe
 
JK bado ana ushawishi mkubwa nchi hii. Spika alikuwa akiwaandaa kisaikolojia wabunge kabla Rais ajahutubia taifa kuhusiana na suala la bandari ya Bagamoyo.

Ni mchakato unaoendelea chini kwa chini wenye kuongozwa na Mzee wa Chalinze, sio mbaya lakini ukizingatia anaacha heshima nyumbani alipozaliwa na itadumu miaka mingi ijayo.

Isije kuwa ni kwa gharama ya kuiuza Tanzania, tukabakia na uhuru wetu wa bendera tukiwa na eneo ndani ya mipaka, ambalo hatuna nguvu ya kulimiliki.

Naomba Mungu hizo conditions za mradi zisije kutuumiza siku zijazo.
 
Bunge la WanaCCM
Wananchi wameikabidhi nchi kwa CCM, waache wafanye walitakalo
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Je, msimamo wa bunge kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni upi?

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Ni ule alioutoa kilaza Ndugai, au hukuusikia?

Na yeye bado analiona bunge kama mali yake; haya ndiyo maajabu ya Tanzania. Mtu kama yule na yeye kuteka taasisi nzima yenye watu wenye akili zao timamu?
Hana bunduki wala mabomu, kwa sababu 'sponsor' aliyekuwa anamwezesha kishajiondokea zake, bado watu wameganda kama wamenyofolewa akili zao kichwani?
 
Isije kuwa ni kwa gharama ya kuiuza Tanzania, tukabakia na uhuru wetu wa bendera tukiwa na eneo ndani ya mipaka, ambalo hatuna nguvu ya kulimiliki.
Mkuu, huelewi mkiendeleza fyokofyoko zenu hata hiyo Bagamoyo mtaikosa?

Hoja zitaanza kujengwa kueleza historia nzima ya ukanda huo wa Pwani. Mzanzibari na mtu wa Pwani watadai wao siyo sehemu ya Tanganyika, mnayoitambua nyinyi kama Tanzania kwa sasa.

Mama na ndugu yake watairudisha Bagamoyo mahali pake, na huo ndio utakuwa mwisho wa habari yenu.

'Seriously', kuna mkakati mkubwa kati ya hawa wawili na jamaa zao akina Rostam na Zungu na wenzao. WaTanzania wasiposimama kidete na kupiga kelele, maskini wa nchi hii hataambulia kitu. Tuna majitu manyang'anyi wakubwa wanaosubiri kunyakuwa kila kitu.

Ngoja tusubiri, tutayaona mengi safari hii.
 
Kwani Magufuli alipozuia mradi usianze bunge lilifanya nini?
 
Wakati wengine wanademand uwazi mikataba bungeni uliwaunga mkono? Kama la, tusipotezeane muda
 
Mkuu, huelewi mkiendeleza fyokofyoko zenu hata hiyo Bagamoyo mtaikosa?

Hoja zitaanza kujengwa kueleza historia nzima ya ukanda huo wa Pwani. Mzanzibari na mtu wa Pwani watadai wao siyo sehemu ya Tanganyika, mnayoitambua nyinyi kama Tanzania kwa sasa.

Mama na ndugu yake watairudisha Bagamoyo mahali pake, na huo ndio utakuwa mwisho wa habari yenu.

'Seriously', kuna mkakati mkubwa kati ya hawa wawili na jamaa zao akina Rostam na Zungu na wenzao. WaTanzania wasiposimama kidete na kupiga kelele, maskini wa nchi hii hataambulia kitu. Tuna majitu manyang'anyi wakubwa wanaosubiri kunyakuwa kila kitu.

Ngoja tusubiri, tutayaona mengi safari hii.
Mkuu akipatacho mtu hutokana na jasho lake. Mwanasiasa ukimuamini sana utaishia kulaumu unapokuwa umekaa na marafiki zako.

Nimemuelewa vyema Rais anapozungumzia uwekezaji, huwezi kuwa na mitazamo ya uoga halafu ukaweza kufanikiwa kimataifa. Huwezi kuwa na pato kubwa la taifa kwa kutegemea wigo mwembamba wa ukusanyaji wa kodi.

Unauongeza wigo wa kodi kwa kuwa na wingi wa shughuli za kiuchumi kwa maana ya uzalishaji. Kusema kila siku kwamba wazungu wana nia mbaya na sisi ni kuendeleza dhana potofu za kimaskini.

Mzungu aliichora mipaka ya afrika mwaka 1884 wakati huo babu zetu wakiwa wanavaa vibwaya kama kipepe wa gazeti la sani. Mzungu huwezi kumkwepa kama kweli unataka kuwa na Tanzania yenye maisha ya uchumi wa kati na ule wa juu.
 
Tanzania hamna bunge, ile ni halmashauri kuu ya ccm, atakachoamua rais ndicho kitakachofanyika. Utaniambia.
 
Back
Top Bottom