Msimamo wa Bunge ni upi kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo?

Punguza fix.
 
Hakuna ninapokataa katika haya uliyoandika hapa ila...
Siyo "mitizamo ya kiuoga', ni lazima uwe na mitizamo ya kujuwa unachokitaka katika uwekezaji huo na kujiamini kwamba unastahili na utakipata unachokitaka. Hata huyo mwekezaji naye haji hapa kiuoga, na atatumia kila fursa ili anufaike zaidi.

Kumbuka, uwekezaji ni mzuri kama unamanufaa kwetu. Hatuwezi kuwa na utitiri wa uwekezaji tukitegemea kwamba tutafaidika nao hata kama hauna manufaa kwetu.

Kwa hiyo sikubaliani na hiyo dhana ya kuwa na uwekezaji mwingi, ni uwekezaji wa manufaa ndio unaohitajika zaidi.

Hapa ndipo panaponikumbusha hii tabia yetu ya utegemezi. Uwekezaji siyo wa nje pekee, uwekezaji mkubwa unapaswa kuwa wa hapa hapa kwetu nyumbani. Tufanye kila juhudi kusaidia uwekezaji huo ufane zaidi.
Ninatambuwa huo wa mabilioni ya dola, kama hatuuwezi kwa sasa, siyo sababu ya kuacha kuhimiza na kulea huu wa vimilioni kadhaa.

Swala la wazungu/wachina, n.k.; wote wana maslahi yanayowaleta hapa, nasi tulinde maslahi yetu kila mara. Hakuna wakati wowote ilipotokea kwamba ukijiweka kupigwa utaacha kupigwa.
 
Watu Wana masikio lakini hawasikii, Wana macho lakini hawaoni.
Kwa akili ya kawaida tu unategemea watoke huko waje na pesa zao kwa ajili ya manufaa ya watu wa Tanzania?
 
Kilichomitisha ni kwa nini haya yanafanyika kwa mufa mfupi sana. Miezi mitatu fastafasta anafufua miradi ya bandari bagamoyo na gesi. Kwamba mama ana haraka sana? Hata kukaa mwaka aone yanaendaje hataki? Kazi ipo
 
Kilichomitisha ni kwa nini haya yanafanyika kwa mufa mfupi sana. Miezi mitatu fastafasta anafufua miradi ya bandari bagamoyo na gesi. Kwamba mama ana haraka sana? Hata kukaa mwaka aone yanaendaje hataki? Kazi ipo
Kuna jambo hapa, siyo bure.

Huyu mama atakuja kutuweka katika hali ngumu ambayo hatukuitegemea kabisa.

Watu hawakumpigia kura aongoze taifa hili, sasa anafanya kila kitu kwa haraka kwa sababu anazojuwa yeye mwenyewe.

Tatizo la nchi hii watu hawana ujasiri wa kuhoji, wanabaki wakilalamikia pembeni basi.

Hata hao mawaziri wake, sijui kama haya yote yamejadiriwa kwenye vikao vyao, na kama yamepitia huko, huenda hata wao ilikuwa ni kupewa taarifa tu, hakuna lolote walilotakiwa kulichangia mawazo na kulifanyia uamzi wa pamoja.Mawaziri kila mmoja wao analinda maslahi yake!
 
Swala la Bagamoyo bora lijadiliwe JF kuliko Bungeni.
Hamna Bunge mle
Umeongea point mkuu gonga tano bunge la Jamhuri ya JF liko kazini kila mtu anajiwakili ccm toeni password kwenye mkataba zishushwe nondo hapa, Dodoma nao wanajiwakilisha wenye na matumbo yao sante mkuu
 
Mkuu nakupinga tuko uchumi wakati sijui uchumi gani wakati mwingine unauzungumzia

Pili mchina sio mzungu wana mikataba mingi ya kilagai nchi kibao inawatesa

Hoja ni mikataba kuwa wazi kwanini mikataba hapa kwetu ni siri ?
 
Mkuu nakupinga tuko uchumi wakati sijui uchumi gani wakati mwingine unauzungumzia

Pili mchina sio mzungu wana mikataba mingi ya kilagai nchi kibao inawatesa

Hoja ni mikataba kuwa wazi kwanini mikataba hapa kwetu ni siri ?
Huyo mchina usiemuamini Nyerere alimuamini na kumpa reli ya TAZARA ajenge, na ndio ulikuwa mradi mkubwa sana kipindi hicho....kb pt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…