Hilo la mwisho, nakubaliana na wewe. Mengine yabaki kuwa mtazamo na maoni yako, nayaheshimu sana...
Lakini CHADEMA iko maili nyingi zaidi ya ushauri wako ktk paragraph ya mwishoni...
Na nikuulize swali maana wewe na huyu ndugu
Stuxnet ni kama hamuijui CHADEMA na kwamba inaongozwa na watu wajinga sana wasiojua uongozi na pengine mkipewa nyie you can do more miracles than these already existed...
Huku nyie mkiwa na fikra hizo za kuiona CHADEMA si lolote, si chochote wenzenu chama chenye dola - CCM wakiiona CHADEMA the biggest threat of their entire political life since 1995 tulipokuwa na uchaguzi wa kwanza Wa vyama vingi. Usiku na mchana sana haha wafanyeje kuidhibiti mpaka wanaanza kutumia njia za kijambazi na mauaji na kutwngeñeza kesi feki zisizo na dhamana mahamakani..
Na kwa hofu hii, CCM kwa sababu tu wanà serikali mikononi mwao wanatumia kila njia OVU na HILA za kidola kukidhooficha chama hiki na ikibidi hata kukitoa katika picha (usajili)....
LAKINI ni takribani miaka 15 sasa majaribio yao ya kukidhoofisha yameshindwa spectacularly huku kikiendelea kuvutia maelfu ya watu wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume kujiunga na wengine kuwa wafuasi na mashabiki tu...
Ona sasa hivi M/kiti Wa chama taifa akiwa gerezani kwa kesi hatari ya kubumba, strategists wa chama wako field wakiandisha wanachama ktk mfumo wa ki - electronic maarufu kama CHADEMA DIGITAL...
Sasa wewe
Stuxnet hiyo hoja ya CHADEMA ni Mbowe na Mbowe ni CHADEMA inasimamia miguu gani eti? That's huko nyuma nimekuambia hata huijui CHADEMA wewe..!
Najaribu kujiuliza mtu kama
Stuxnet sijui hata anapata wapi guts za kusema chama hiki hakina wazee washauri na wana mikakati (strategists) ndani ya chama...
Hebu tuacheni mabezo ya namna hii jamani. Tuwape credits CHADEMA kwa sababu walishavuka viwango vya NCCR - Mageuzi ya kina Marando na Augustino Lyatonga Mrema ya (1995 - 2000) au CUF (2000 - 2015) ya Prof. Lipimba, hàyati Maalim Seif Sharif Hamadi na Hamad Rashidi...
For sure, CHADEMA hii kama chama cha siasa ina nguvu kuliko hata CCM bila kujali madhila kinachopitia. Sasa itakuwa ni mjinga pekee kubeza nguvu ya chama hiki hata kudai kina uongozi dhaifu.....!
Chama cha siasa chenye uongozi dhaifu au kisichokuwa na wazee washauri wazuri au kisichokuwa na Leadeship Organizational Structure nzuri huwa hakikui na hujifia chenyewe taratibu lakini sio CHADEMA hii. Hopefully, ndugu
Stuxnet utakuwa umenielewa...