Alichosema Kisumo ndicho sahihi!. Mjerumani alikuwa akitumia utawala wa direct rule, Muingereza ndio akaleta indirect rule ya devide and rule!. Wagawanye uwatawale kwa kuanzisha utawala wa uchifu!. Machifu walifanywa wajione wao ndio bora zaidi, na mkuu wa machifu wote Tanzania ndio Mangi Mkuu, Thomas Marealle!.
Ni ukweli usiopingika watu wa koo hizi za kichifu walipendelewa ikiwemo kupewa nyumba na Malkia kule London!. Hawa walikuwa ni vibaraka wa wazungu!, walinuona mkoloni ni bora zaidi kuliko mtu mweusi!. Mpaka leo, mpaka kesho Mchagga anajisikia fahari sana kuishi kuzungu, kuvaa kuzungu, kutembea kizungu, kuongea kuzungu na kutokana na kuupenda uzungu, baadhi ya wanawake wa kichagga Mungu amewapa shape za kuzungu (pasi)!.
Mpaka leo mpaka kesho, zile familia zenye uwezo za kichagga, wanakwenda kujifungulia London!.
Nimebahatika kusoma na one of the Marealles toka ukoo wa Mangi Mkuu, hawa jamaa ni mayai kweli kweli!. Tulipomaliza tuu form four, mwenzetu huyoo London!. Nilipopata fursa ya kuja Uingereza, nilimtembelea, life ilikuwa safi!, jamaa wana nyumba ya ukoo London ila yeye na mkewe walipanga nyumba nzima jirani!. Maisha ni ya kudeka deka tangu Tanzania hadi London!.
Tangu tulipoachana Bongo hadi tunakutana London ilipita yapata miaka 10!. Tulipafanya tathmini ya pamoja kati ya miaka 10 ya bongo, mimi nina nini, na miaka 10 ya London mwenzangu ana nini!, akatamani kurudi bongo na mimi nikamuunga mkono. Miaka miwili baadae alirudi na familia yake ila its very unfortunatelly maisha ya bongo yalimshinda!, family ilisambaratika for sometimes, ila kutokana na kuona familia bora, family ili take controll, familia ikatengamaa na jamaa akaona bora arudi kuishi London, huko amezoea zaidi na maisha anayaweza kuliko maisha ya huku!.
Back to Mangi Mkuu, aliside na wakoloni kuwa Watanganyika bado hatiko tayari kujitawala mpaka labda baada ya miaka 15-20!. Akapendekeza kwa vile Kilimajaro ilikuwa juu kimaendeleo, watoe uhuru kwa majimbo kwa Kilimanjaro kupewa uhuru wake kwanza, maeneo mengine yakishaendelea nayo ndio yapewa uhuru hadi Tanganyika yote iishe!.
Chief Marealle ali undermine juhudi zozote za Tanganyika kujiwala, Nyerere baada ya kulijua hili, ali team na wale Waswahili masikini wenzake na wale wazee wa Gerezani, tukapata uhuru!. From there alifutilia mbali uchifu, Mareale akamind sana!. Akawasideline Wachagga kwenye urais!. Never will this country be ruled na rais Mchagga!. Laana ya Nyerere itatushukia!.
Poleni!
Merry X-mass
Pasco