Msimamo wa Nyerere, Mareale UN ulikuwa mmoja

Wickama,

..hapa nadhani national politics ziliingiliana na local politics.

..fuatilia kote ambako nime-highlight with red or black.

..Marealle alianza kwa kumshinda Shangali wa Machame ktk kuchagua Mangi Mkuu.

..baadaye Marealle akawa hana tatizo TANU au Mwalimu Nyerere.

..makala inasema " he[marealle] still supported the national aims of TANU for Tanganyika."

..tena wanaeleza kwamba alikuwa hata anam-support Mwalimu Nyerere "personally."

..mwaka 1957-58 Marealle aliandika barua kwa gavana akipendekeza Mwalimu Nyerere apewe nafasi ya kuhutubia Council of Chiefs. Hii council of Chiefs ilianzishwa na wakoloni kwa lengo la kupunguza kasi ya TANU. Marealle aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa hiyo Council.

..Pamoja na Marealle kuwa ktk council ya ma-chief, iliyoanzishwa na wakoloni, lakini bado tunaona anataka Mwalimu Nyerere apewe nafasi ya kuzungumza na machief na kuwasilisha hoja za TANU.

..Pia kuna taarifa kwamba hotuba ya Chief Marealle kule UN ilisisitiza matanio ya wa-Tanganyika kuwa huru.

..matatizo yalianza baada ya Abdieli Shangali,aliyeshindwa na Thomas Marealle ktk uchaguzi wa kumpata Mangi Mkuu,kuingia ktk siasa za TANU akim-support Solomon Eliufoo.

MY TAKE:

..Wamachame na Wamarangu wana matatizo yao ya kihistoria. Kuna kipindi jamii hizo mbili zilikuwa hata hazioleani.

..Kama TANU iliingia Uchagani kwa msaada wa familia ya Chief Shangali wa Machame,basi bila shaka kutakuwa na mgogoro na Chief Marealle wa Marangu.

..kwa mtizamo wangu tatizo halikuwa Uhuru wa Tanganyika, bali ni ule mgogoro wa Kihistoria kati ya Wamarangu na Wamachame.

..Kuna habari za kuanzishwa kwa Chama cha Siasa cha Wachagga na tetesi kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa akikiunga mkono chama hicho,lakini baada ya kutimiza malengo yake akakitupa mkono.

cc Nguruvi3, Mag3, Kudi Shauri, Jasusi, Abunuas, Kishimbe wa Kishimbe, ilboru1995, Pasco
 
joka,

Nisaidie kitu, Tunajua Nyerere alikwenda UN kwa tiketi ya TANU kuwatetea watanganyika kudai uhuru. Sasa, huyu Marealle alikwenda UN kudai nini kwa tiketi ya nani na agenda yake ilikuwa kwa maslahi ya kina nani tofauti na wale waliotetewa na JKN? Hapohapo tunaambiwa alikuwa anam-support Nyerere kisha strangely akapiga marufuku mikutano ya TANU mjini Moshi 1959?
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu
Hili la Marealle na Nyerere kwa kadri ninavyolifahamu na kupitia machapisho linapotoshwa


Tofauti yao ilikuwa muda wa Tanganyika kujitawala na wala si kupinga uhuru.

Kutokana na mgogoro wa kihistoria uliousema ambao bado upo kichini chini wapo watu wanatumia fursa hiyo na kusema Marealle alipinga uhuru.

Hapa kuna tatizo lingine linajitokeza na hili lipo kwa Nyerere na viongozi wetu wengine.
Confusion yote hii ni kwasababu Mwalimu hakuandika ''Memoir' yeye mwenyewe na hivyo kutoa nafasi ya ''inasemekana'.


Nadhani unaona jinsi mzee wetu Mohamed Said anavyopotosha sehemu ya umma kwa hisia zake kwa vile hakuna kumbu kumbu rasmi zaidi ya masimulizi ya second and third party.

Kuhusu mzee Kisumo, nadhani muda umefika apunzike.

Siku za karibuni amejivunjia heshima yake sana kiasi kwamba ile credibility aliyoijenga miaka mingi imekuwa eroded vibaya sana.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wale mnao changia hii thread i have to give you one thing to note kuhusu uhusiano wa Nyerere na siasa za Tanzania, na kwa nini kimantiki Nyerere asingeweza kupatana na either Mangi Marealle au Shaghali.

Point yenyewe ni hii. Wakati Nyerere anajanjaruka (ujanja wenyewe alipewa na wazungu), uchaggani watu walikuwa wameshajacharuka kabla yake. KWa sababu gani nasema hivyo. Wachagga teyari walikuwa na elimu na maarifa ya kutosha kuongoza serikali bila kuhitaji msaada wa mtu yeyote. Uchagani mifumo ya kiserekali ilikuwepo muda tangu na tangu. For your information, mifumo ya kiserekali imetokana na jamii zenye mifumo ya kilimo huko ulaya au asia. Jamii nyingi zilizookana na mifumo hii ya kijamii hata kwenye biashara ni wazuri popote pale duniani. Hivi ni vitu ambavyo vlilkuwepo uchaggani na maeneo ya jirani mpaka kwa wakikuyu. Organised agricultrure ndo imepelekea organised business tuliyo nayo leo.

Sasa swali linakuja hivi. Nyerere alikuwa anauwezo gani wakuongoza bila msaada wa watu makabila mengine? Alichokifanya Nyerere ni kukimbilia kwa waswahili, akajifanya yeye mswahili, na waswahili wanavyopenda sifa basi wakamtukuza kweli naye akapata kichwa. Waswahili wakitakakumzidi ujanja anakimbilia kwa wachagga, akiona wachagga wanataka kumzidi ujanja anakimbilia kwa waswahili. Hivyo hivyo ndivyo alivyoyafanyia makabila mengine kama wahaya. He was like an imaginary character kitu ambacho somehow kilimsaidia. Lakini laiti Nyerere angeenda na Uzanaki wake kulikuwa hakuna jinsi angeweza kukubalika au kufanya mambo aliyoyafanya.

Kwenye duru za siasa za ulimwengu wa leo, Nyerere kwa sasa namfananisha sana na Mch Mtikila. They are both like 'one man show'. Siasa za Nyerere, hata Mtikila, na kidogo Zitto alikuwa anaelekea huko, zilikuwa hazina interest yoyote ya kumtoa mwafrica kwenye umaskini bali kumtoa mwafrica kwenye kuonewa au kutawaliwa. Mwafrica wa leo anahitaji elimu, maarifa ya kisayansi na technologia ya viwanda. Mwafikra wa leo anahitaji mapinduzi ya kifikra ya kutokudhani kwamba kuna binadamu superior kuliko mwingine bali mwenye kujua kwamba mambo yote yanawezekana chini ya juua. Haya yote yanawezekana kwa kuwa na jamii imara yenye misingi bora ya kifamilia, kimalezi, kazi nk.

Kuna watu wanapenda kukaa na kuzungumza vitu hata wasivyo vielewa vizuri kuhusu wachagga. Waacheni Wachagga wenyewe wajieleze. Wanabaki kuzusha tu uzushi na hadithi zisizo za kweli. Ukiwauliza nia yao sidhani hata kama wanajua, zaidi ya stereotype mind. Ila ukweli utakuja dhihirika tu. Wachagga ni wapiganaji katika nyanja zote za maisha, hilo halina cha ubishi, na wameiipigania sana na kuitumikia sana hili taifa tangu kabla na hata baada ya uhuru, ni kwamba majina yao hayako kwenye rekodi kwa sababu they did not need it. Ila kwa sababu waswahili wanapenda kulalamikalalamika na kujikweza kweza hata kama ni kwa jambo dogo tu, basi makelele mengi kweli utasikia. Wao ndo wamejipa hati miliki ya nchi hii, kila kitu wao, ndo maana huyu mwingine anadhani uraihisi ni kupeana kula kwao, kila kitu bagamoyo.
 

Nara;
Uhalisia wa maneno ni kuwa wachagga wako very organised kuanzia na family tasks hadi society wanayokaa. Ikiharibika ni huko baadae lakini sio huko walikotoka. Matunda ya kuwa organised yanaonekana sana kuwa haipo familia ya kichaga inamwachia mtoto kuwa "zoba zoba haeleweki". Kwa sababu hii mpaka kesho ni vigumu ukakuta vijana wa kichagga kwenye orodha ya "stow away" waliorudishwa toka ughaibuni au wabebaji wa madawa. Ni malezi. Zingatia kuwa wachagga ni makabila na dini tofauti. Wachagga ni testimony kuwa issue ya maendeleo sio uDINI ni BIDII binafsi.

URAIS. Binafsi naamini kuweka aina yoyote ya kizuizi (cha wazi au kificho) ili kwamba mtu mwenye kutambulika kama MCHAGA asiwe kiongozi wa nchi itakuwa ubaguzi wa kiJINAI na ni kinyume cha katiba ya nchi hii. Hakuna aliyechagua kuzaliwa kwenye kabila lake. Lakini mtu kama anatoka jamii ya kichagga akijenga imani kuwa SISI TUNAZUIWA KUWA MARAIS pia ni tatizo kubwa kwa nchi yetu kwa vile huenda tutakosa mzalendo tena mwenye kipaji na tija na maono ya kusaidia nchi. Hii ni hofu ambayo lazima tuivunje ili vijana wetu wa KICHAGGA, KIHAYA, NA KINYAKYUSA waitupilie mbali na kuacha kuishi na MYTHS. We need their talents and energies.

Tufanye nini?

1. Mimi nadhani ni muhimu sana vijana wa kichagga wakachapa kazi kama walivyo sasa bila hofu yoyote moyoni ya kubaguliwa wala unyonge

2. Ipo haja ya vijana wa kichagga kuwa kwenye safu za CCM kama wanachama na viongozi (why not?)kwa vile wengi wao wana vipaji vizuri na ni wachapa kazi wazuri lazima Mbele ya Safari mmoja wao atajawakilisha chama hicho kugombea urais, after all patience is the key. Kuna timu za premier league (UK au Bongo) hazijawahi pata ubingwa tangu ligi ianze lakini hazijatangaza kuchoka. Ni Kweli au uongo? (why the haste?)

3. Issues za kina Nyerere/Marealle/Abdulwahid/Bibi Titi huwa naziona kama ni za wakati HUO. Walichoweza sawa, walichoshindwa pia sawa. Hatutawarudishia uhai ili warekebishe dosari zao hata kama tukishinda tunawasema kwenye studio/websites zote duniani. Sisi Tu-focus nguvu zetu kwenye mahitaji yetu ya leo na kuweka mikakati ya kesho
 
Wickama,

..sina uhakika Chief Marealle alitumwa na nani.

..huenda alikwenda UN kuzungumza kwa niaba ya Machifu wenzake wa Tanganyika.

..kuna mahali Nyerere ananukuliwa aki-endorse hotuba aliyotoa Marealle huko UN. hapa nakushauri utafute maandiko wa mwanahistoria John Illife.

..sasa kwa msingi huo utaona kwamba Chief Marealle hakuwa na ajenda tofauti na Mwalimu Nyerere au TANU.

..kwa mtizamo wangu, Mwalimu Nyerere na Chief Marealle, walipishana baada ya Mwalimu kuanza kuwa karibu na maadui wa kisiasa[za uchagani] wa Marealle.
 
Last edited by a moderator:
Wickama,

..nadhani kuna wa-Tanganyika wengine zaidi ya Japhet Kirilo, Chief Marealle, na Mwalimu Nyerere, ambao walipata kuwasilisha petition mbalimbali dhidi ya Waingereza before the UN.
 
Last edited by a moderator:
Mnawawaza sana wachaga .....shame on u all ....hata mfanye mfanyavyo waliotangulia wametangulia tuu... Ukweli ni kwamba hata nyie mnaowaponda wachaga mnataman mngezaliwa wao....waacheni wenzenu wale maisha walijua elimu mapema wakat babu zetu wakiwasisitizia baba zetu kuchunga ng'ombe na kulima kwa jembe la mkono....wachaga kwenye kila sekta wako na ni ukweli usiojipinga kuwa wao kwa asili mia kuubwa wameichangamsha tz wakipeana tough na wahaya na wanyakyusa...fika kilimanjaro migomban magorofa kibao sio sisi had tuje dar ndio tuone majumba ya kifahar au wengne tunaishia kuziona kwenye bongo movies
 


Ukichunguza historia ni vigumu kuona ni wapi machame imekuwa na mgogoro wa kihistoria na wamarangu. Machame ilipata matatizo na kibosho miaka ya mwisho ya 1880 ambapo Mangi Sina, mtawala wa Kibosho (ambaye yeye mwenyewe alikulia Machame) aliunda zengwe na kuuwa wamachame kadhaa kule Kibosho na kutumia fursa hiyo kuivamia Machame na kusababisha uharibifu na maafa makubwa. Tokea wakati huo wamachame na wakibosho walikuwa na uhasama wa kufa mtu. Kitendo alichokifanya Mangi Sina kilisababisha Kibosho kuingia kwenye mgogoro na Mangi Mandara wa Moshi (rafiki wa Mangi wa Machame) akisaidiwa na Mangi Marealle wa Marangu (kwa kumlazimisha) ambapo waliishambulia Kibosho kwa nguvu zote ingawa hata hivyo walishindwa vibaya.

Inaaminika kihistoria kwamba baadaye Mangi Marealle aliunda urafiki na Mangi Shangali wa Machame, ili yeye (kwa kuunda urafiki na wakoloni wa kijerumani baada ya kufariki kwa Mangi Mandara) awe mkuu kule mashariki ya uchagani na Machame irudi tena kwenye historia yake ya kuwa nguvu kubwa magharibi mwa uchagani (baada ya kifo cha Mangi Sina mwaka 1897). Hata hivyo urafiki huu haukudumu muda mrefu sana na usingeweza kurejesha uchagani kwenye miaka yake ya zamani. Wakoloni wa Kijerumani walikuwa wameshashika hatamu kwa hiyo utawala wa kimila usingekuwa na nguvu tena waliyoiotea ndoto. Shangali alijiuzulu umangi mwaka 1900 na kaka yake aliyeshika nafasi kule Machame hakufahamiana sana na Marealle. Marealle alifariki mwaka 1911 na utawala wa Marangu uliofuata haukuwa maarufu kwa wakoloni na hivyo kupoteza nguvu ya ukaribu aliyokuwa nayo Mangi Marealle. Kibaya zaidi wakoloni wa kijerumani waling'olewa mara baada ya vita kuu ya kwanza na Uingereza ikachukua nafasi yao Tanganyika mwaka 1917.

Inawezekana sera waliyokuja nayo waingereza ndiyo ingeweza kuzaa uhasama kule uchagani. Mwaka ule tu walioingia rasmi Tanganyika, wakaingizwa kwenye zengwe lililopikwa kwa ufundi kule uchagani na hata kuamua kuwakamata watawala wote wa kichaga na kuwapeleka rumande sehemu mbalimbali kwenye mwambao wa Kenya. Hata hivyo yaliyotokea baada ya hapo ndipo wakagundua ule ulikuwa ni ujanja wa kisiasa ambao ulijikita zaidi Machame. Shangali alirudi tena kwenye umangi kule Machame kupitia zengwe hilo. Waingereza wakapiga presha kwamba Shangali asiendelee kutawala wakihisi zengwe. Hata hivyo makubaliano yalifikiwa kwamba ataachia madaraka mmoja wa watoto wake wakubwa atakapokuwa amekua na kuwa tayari kutawala. Hatimaye 1922 Shangali alistaafu rasmi siasa na mtoto wake Abdiel akatawala mahali pake. Kwa kuona Machame imekuwa na mizengwe mingi ya kisiasa, waingereza waliamua kumvuta kwa karibu Mangi Abdiel ili kumdhibiti na hata kudhibiti Machame. Wakamfanya awe ndiyo mwakilishi na msemaji wao kule uchagani, nafasi ambayo baadhi ya wazee hasa kule Vunjo waliona alikuwa nayo Marealle kwa Wajerumani na hivyo mtoto wake aliyekuwa akitawala, yaani, Petro Itosi, aliistahili. Hii ilileta maneno na minong'no mingi huku wakimtuhumu Mangi Abdieli wa Machame kuwa kibaraka wa wakoloni. Maneno hayo yalisababisha mwaka 1930 Waingereza waitishe uchaguzi wa mwakilishi wa wakoloni kwa wazawa atakayekuwa kiongozi wa watawala wote wa kichaga. Ili kufuta minong'ono, waliwapendekeza Mangi Abdiel wa Machame na Mangi kijana wa Marangu, Petro Itosi, wagombee hizo nafasi. Matokeo ya uchaguzi yaliyofanywa kwenye baraza la watawala wa jadi kule uchagani yalionyesha kuwa Petro Itosi alishinda kwa zaidi ya 99% ya kura zote. Kutokana na matokeo hayo kuwa kinyume kabisa na walichokitaka wakoloni, walidai uchaguzi ulivurugika na hivyo matokeo kuwa batili. Sintomfahamu hiyo iliendelea mpaka mwaka 1946 walipoamua kuunda watawala wa majimbo kule uchagani na kuigawa uchagani yote kwenye majimbo matatu tu, yaani Hai (iliyokuwa na asilimia karibu 50 ya uchagani yote) wakampa mtu wao, Abdieli Shangali wa Machame; Vunjo ikawa chini ya Mangi Petro Itosi wa Marangu; na Rombo iliyokuwa chini ya Mangi Selengia Kinabo wa Rombo Mkuu.

Haya matukio ndiyo yanaweza kudhaniwa kusababisha uhasama kuwepo kati ya Machame na Marangu, ambapo walionekana kama wapinzani (rivals) kwenye kinyang'anyiro cha kuwa juu ya watawala wote wa kichaga. Pamoja na kuteua watawala hao wa majimbo, inaonekana wakoloni waliendelea kumfanya (isivyo rasmi) Mangi abdieli Shangali kuwa ndiyo kama mkubwa wa wengine na mwakilishi wa wakoloni kule uchagani. Walimteua kuwa mtanganyika wa kwanza kuwakilisha wazawa kwenye baraza la kutunga sheria na mwaka 1947 alialikwa Uingereza na Mfalme wa Uingereza kupewa nishani ya MBE. Mambo haya yalizidisha chuki na chokochoko zilizidi hasa kutokea Marangu na baadhi ya wapinzani wa siku nyingi wa kisiasa kule Hai ambao hawakumpenda Mangi Abdieli. Kwa kuona Mangi Petro Itosi asingeweza kukabili mikakati hiyo, walimshawishi mtoto wa kaka yake, Thomas Marealle agombee nafasi ya cheo walichokipendekeza cha Mangi mkuu wa uchagani. Hii sokomoko yote ndiyo imekuwa ikionyesha historia ambayo inawezekana imekuja kutafsiriwa kuwa wamachame wamekuwa na uhasama wa kihistoria na wamarangu. Lakini usaili wa wamachame kihistoria unaonyesha hawadhani kama Marangu imekuwa na nguvu ya kihistoria ya kuwa mahasimu wao wa kisiasa (yaani rivals).
 

Inaonekana hapa Nyerere aliwakilisha Chama ..Wakati Marealle aliwakilisha ..Native authorities ..chiefs au Sasa Mameya .......inaonekana Nyerere akiwa fix Kina Marealle ...ambaye alimuunga mkono lakini baada ya Uhuru Akawapa native leaders ( chiefs ) wengi uongozi Kama Kina Chief Mkwawa ,Cheef fundikira ,kunambi etc kazi ....a kamtosa Marealle ...plus INAJENGWA propaganda inayoendelea kuwatesa watu hadi Leo kuwa Hawakutaka Uhuru ..au walitaka KUJITENGA .......
ni muhimu Sasa Wakati umefika ukweli UWE wazi ili Jamii zingine NAZO zipumue
 

Hapa tutajadili mengi sana ila ukweli wazungu walimtaka Merrealle kwa sera zake na ndiyo maana wakampa mafasi ya ukuu wa machifu kwani walijua angekuwa bepari tofauti na sera za Nyerere kwani wazungu walishamjua Nyerere kuwa ni right wing conservatives ila bahati mbaya walishachelewa kwani wakakuta tayari Nyerere ana nguvu kuliko melleale walijiitahid kumpigania Melleale lakini waap kwani Nyerere nae alikuwa mjanja, msomi na tayari alisha jua lengo la Melleale na wazungu wake na ndiyo maana alipopata uhuru tu akampeleka hukohuko(UN) akae nao na yeye(Nyerere) akafanya mission yake hapa nyumbani

Mimi sidha kama kunakitu kipya cha kuandika kuhusu hii historia kwan hata hayo maelezo ya mtoa mada kaanza kana kwamba anaishu nyeti iliyotofauti ambayo hata mallecture hawaijui lakini maelezo yake yenyewe mepesi tu juu ya chuki za machifu wa kichaga

Nothinng is hidden hapa na wala msitumie nguuvu kuuubwa kupambana na ukweli kwani always ukweli ukweli huwa unajipigania.

Mellealeku kumsemea Nyerere ama Nyerere ku recomend speech ya Melleale hai justfy kuwa hawakuwa wahasimu, kwenye politics tunasema thats politics na always if you cant fight him just join him so hatujui who? joined who?.

Thats it
 
Tumkumbuke Nyerere.
Pasco
 
Hakika mkuu shukrani sana.
Paramount chief mariale alikua na wazo zuri sna hapa kuwaunganisha watanganyika wote pamoja pamoja na kusaidia machifu wenzake wa sehemu tajwa.
 
Kuna shida mahali kichwani mwako
 
Asante
 
Waingereza mwanzoni waliwa avoid walutheri weusi kwa sababu ya uhasama wao na Wajerumani during WW I. Walijaribu kueneza uprotestanti wa kwao Tanganyika (uanglikana kwanza na pili u presbyterian). Sometimes kidogo wali import watu hao kutoka makoloni jirani na Tanganyika. Baadae wakaona wa shirikiane na walutheri weusi baada ya kuanza kuwa na mahusiano mazuri kidogo na wajerumani. Vile vile walijenga ushirikiano huu kama njia ya kudhibiti ukatoliki ambao ulikuwa una anza kuwa na nguvu Tanganyika. Lakini walikua wamechelewa kidogo.

Nyerere alikuwa mjanja, lakini pia alisaidiwa na kushauriwa na ma Jesuit.

Na hisi vile vile machifu wa kiprotestanti huenda pia walikua na ukaribu na freemasons wa kiingereza. Nyerere huenda alikuwa ana juana na hao freemasons lakini alikuwa mtiifu zaidi kwa ma Jesuits.
 
Kidogo Kama naelewa nia ya marealle.sababu tangu tupate uhuru bado tupo palepale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…