Msimamo wa Olimpik mpaka mchana wa leo

Marekani ni watu wa-bad sana, kila sekta wao huongoza, Ni taifa la namna gani aisee?!
Ni mchanganyiko kutoka watu wa mataifa mbalimbali. Utakuta wachina, warusi, waarabu, wahindi, waafrika, walatino, wajapani bila kusahau black Americans. Wote hao wanabeba bendera ya Marekani
 
Lkn sisiem haimwambii Bayi afanye hovyohovyo
Tatizo sio kufanya kazi ovyo ovyo, tatizo tulilonalo ni la kulindana, yaani atavurunda weee mtapiga kelele ila wapi, kila uchaguzi ukifika anachaguliwa tena, hiyo ndio advantage ya kuwa Chama tawala, Sasa hapo unatarajia kuna siku tutasonga mbele?
 
Hatimae mpk India wamepata Gold sisi patupuu
 
Nchi moja inapeleka wanamichezo zaidi ya 200 unategemea wote watakuwa watupu..

Alafu bongo kuna watu wanajiita wadau wa michezo dah sijui michezo ipi hata olimpiki hatuonekani..

Kila kitu siasa tu..UVCCM kwanini hamjatuwakilisha?
 
Marekani ni pool ya vipaji, pale utakuta hata 30% ya washiriki sio wazawa. Arnold Schwarzenegger kazaliwa na kukulia Austria ila kawa gavana wa jimbo kubwa kiuchumi Marekani. Ile nchi ishajielewa hata sisi tunatamani kuishi kule
Mbio za mita 10000 wanawake leo mshindi wa kwanza ni mdada mwenye asili ya Ethiopia lakini raia wa Uholanzi,mshindi wa pili ni wa Bahrain na yeye ni mwenye asili ya Ethiopia na watatu ni Muethiopia mwenyewe,wenzetu vipaji vipo na vinaendelezwa haswa,wanapewa mauraia ya nchi za kizungu huko sisi huku ndiyo kila siku vita UVCCM na BAWACHA..
 
Kesho saa ngapi?I cant wait to see them but as country mbona hatujapeleka wengi hata 10?
Wanamichezo wa kitanzania hawazidi wa 3 walioko Tokyo ila si ajabu wameongozana na viongozi kutoka Wizara ya Michezo,BMT,Viongozi wa kutoka Ubalozi wetu Japan,viongozi unakuta ni zaidi ya 10..
 
Wanamichezo wa kitanzania hawazidi wa 3 walioko Tokyo ila si ajabu wameongozana na viongozi kutoka Wizara ya Michezo,BMT,Viongozi wa kutoka Ubalozi wetu Japan,viongozi unakuta ni zaidi ya 10..
Hahaaaaaaahaaa
 
Tatizo sio kufanya kazi ovyo ovyo, tatizo tulilonalo ni la kulindana, yaani atavurunda weee mapinga kelele ila wapi, kila uchaguzi ukifika anachaguliwa tena, hiyo ndio advantage ya kuwa Chama tawala, Sasa hapo unatarajia kuna siku tutasonga mbele?
Kama Mwenzake wa futiboli.
 
Wanamichezo wa kitanzania hawazidi wa 3 walioko Tokyo ila si ajabu wameongozana na viongozi kutoka Wizara ya Michezo,BMT,Viongozi wa kutoka Ubalozi wetu Japan,viongozi unakuta ni zaidi ya 10..
Viongoz hawanaga aibu hata chembe
 
men marathon ...Alphomce felix simbu kashika namba 7...mkenya Eliud kipchoge kaua band..jamaa anakimnia hatar...kavunja rekod ya dunia...
 
men marathon ...Alphomce felix simbu kashika namba 7...mkenya Eliud kipchoge kaua band..jamaa anakimnia hatar...kavunja rekod ya dunia...
Simbu amejitahidi sana, anaonekana ana uwezo shida ni maandalizi duni kwasababu hafanyi hiyo riadha kama kazi yake ila anafanya kama kitu cha ziada, na hapo ndipo tunapofeli, angekuwa na uwezo wa kuwapatia familia yake mahitaji ya kila siku na kuamua kukomaa na riadha labda muda huu tungekuwa tunaongelea mambo mengine.
Siwezi kumlaumu kwa kweli, unakomaa na riadha huku huna pesa mfukoni kwa ajili ya kuendesha maisha yako ya kila siku ni ngumu sana kwa kweli
 
Marekani wameshamvuruga Mchina huko, kuanzia kwenye idadi Gold medal mpaka idadi ya Medali, na hapo wanasema hawakupata muda mzuri wa maandalizi kutokana na ishu ya Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…