Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Nimemsikiliza waziri Kabudi ambaye alimwakilisha Rais Magufuli kwenye kikao cha Umoja wa Afrika. Wakati Rais Ramaphosa wa Afrika ya Kusini akiwa ni mwenyekiti anayemaliza muda wake, akieleza jinsi korona ilivyovuruga mipango ya maendeleo katika bara la Afrika, Tanzania ilitoa msimamo wake na pia kushauri Afrika ichukue msimsmo huo.
Msimamo wenyewe ni Tanzania na Afrika kwa ujumla zijiimarishe katika tafiti za chanjo na madawa ili kuondoa utegemezi kwa "mabeberu".
Sina tatizo kimsingi na hoja hiyo. Kwa kweli ni hoja nzuri tu. Tatizo langu ni kwamba hii hoja inatokana na kelele zinazopigwa na viongozi wetu hivi sasa, ili kuenda sawa na misimamo tata ya Magufuli. Kauli aina hii ndio kama anazotoa Profesa Mchembe, katibu mkuu wizara ya Afya. Na ndio zinafanya wengine wanadiriki kupiga marufuku uvaaji barakoa. Ni ujinga na ujuha wa kiwango cha pekee.
Hakuna sera ya utafiti inayotuongoza kufikia hayo anayodai Kabudi, na hata ile "political will" tu haipo. Magufuli arundike mabilioni katika elimu ya juu na utafiti? Apunguze matrilioni yanayokwenda kwenye miundombinu? Aache miradi yaje ya Chato? Wala sioni dalili ya hilo kutokea, hata kama hizo sera zingeandaliwa.
Magufuli huyu anayewafrustrate maprofesa, anayedai vyuo vikuu vitoe hela ya GAWIO serikalini ili ajenge barabara, ndio asimamie miradi ya utafiti wa chanjo za korona, ambayovinahitaji matrilioni, utaalamu wa ngazi ya cutting edge, ambao unahitaji kujengwa na kutunzwa? Sioni hata dalili.
Magufuli sio mtu wa miradi ya muda mrefu, matokeo yaje yeye kaondoka. Anataka afanye na kukamilisha sasa.
Kwa hiyo akina Kabudi na Mchembe wanapiga sound kama za yule waziri wetu mpendwa wa viwanda, aliyetufundisha kwamba hata vyerehani 4 ni kiwanda