Siyo kweli. Katika kipindi chake hata supply za mbolea zinatoka kwa wakati kuliko rais yeyote. Na amekuwa akisisitiza tulime kwa bidii ili tusaidie nchi waliojifungia. Amekuwa akisisitiza kuwa hata toa chakula kwa wasiolima. Mkuu wa mkoa, wilaya, Das na viongozi wote wa eneo ambao watakumbwa na njaa wakati mvua zinanyesha wajiandae kuondoka. So viongozi wanahimizwa Na Mheshimiwa rais MagufuliJP walime na wahimize wananchi walime. Shida ni moja tu kuwa tumekuwa na viongozi wa wizara ya kilimo siyo wabunifu kutafuta masoko nje ya nchi. So kuhusu kuhimiz kilimo amejitajdi sana na hapendi wananchi wake wazulumiwe. Kumbuka issue ya korosho.
Tuseme ukweli.
Kwenye issue ya kusisitiza kujitegemea bara nzima ni nzuri sana sema wanaopokea ndo shida. Nchi kama South Africa ingechukua Hilo kama wazo kuu ingeteka soko la Afrika na tuweze kumuunga mkono. Shida weusi sisi hatuaminiani.
Suala la Kilimo lina maeneo muhimu ambayo yanatakiwa kuangaliwa ili kubaini na kupima utendaji wa serikali katika eneo husika.
Umemsifia Magufuli kwamba anahakikisha mbolea inafika muda unaotakiwa. Hiyo ni administrative , logistical issue. Hiyo ni ngazi ya chini sana. Tuanze na ngazi ya kisera. Shida namba mojakatikakilimo ni RUZUKU. serikali ya nyerere iliweka ruzuku kubwa na kuwezesha kilimo bora kiwezekane kwa mtanzania wa kawaida. sasa hivi kilimo ni business venture kubwa inayohitaji mtaji mkubwa.
Ukiangalia bajeti zetu, miundombinu huteka zaidi ya Trilioni 4, wakati kilimo ni bilioni kadhaa, na hata hizo zinazotengwa humegwa na kuongezwa kwenye miundombinu. Magufuli ana obsession na miundombinu, na ana obsession na miradi isiyo ya lazima kama Dodoma na Chato, ambayo imegharimu matrilioni mengi. Hebu fikiri hayo yote yangeingizwa kwenye kilimo?
Katika kilimo, jambo muhimu sana ni muunganiko kati ya mkulima, vituo vya utafiti, na afisa ugani. Mkulima aimarishwe kwa mafunzo na ruzuku katika pembejeo. Afisa ugani apewe mafunzo makini, vitendea kazi, maslahi bora, athaminiwe, asimamiwe. Research centers kama Ukiriguru, Uyole, Naliendele, Tengeru, Mlingano, nk., ziimarishwe na kupatiwa fedha inayotakiwa kama ilivyokuwa hapo zamani.
Enzi za Nyerere vituovvya research vililindwa sana kama mboni. Magonjwa kama ya migomba huko Bukoba yanayotamba sasa, ingekuwa kama zamani wangeshakuja na ufumbuzi. Hata hii nguvu ya GMO isingekuwepo. Tumepiga marufuku GMO, lakini kiutafiti tupo vizuri? Vituo vya utafiti vimetelekezwa.
Nadhani umeelewa kwa nini napiga kelele. Magufuli angeelekeza hasira zote kwenye kilimo, tungevuka