Msimamo wa Tanzania kuhusu Korona uliotolewa katika kikao cha Umoja wa Afrika AU ni ubabaishaji

Eti "hana interest na miradi ya muda mrefu", SGR ni mradi wa wiki?

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Magufuli hata mradi ambao kwa nature ni wa muda mrefu, atalazimisha uishe haraka, bila kujali negative consequences. Kwa hiyo mkuu hiyo tu ndio umeona point kubwa kwenye huo uchambuzi.
 
Suala la Kilimo lina maeneo muhimu ambayo yanatakiwa kuangaliwa ili kubaini na kupima utendaji wa serikali katika eneo husika.
Umemsifia Magufuli kwamba anahakikisha mbolea inafika muda unaotakiwa. Hiyo ni administrative , logistical issue. Hiyo ni ngazi ya chini sana. Tuanze na ngazi ya kisera. Shida namba mojakatikakilimo ni RUZUKU. serikali ya nyerere iliweka ruzuku kubwa na kuwezesha kilimo bora kiwezekane kwa mtanzania wa kawaida. sasa hivi kilimo ni business venture kubwa inayohitaji mtaji mkubwa.
Ukiangalia bajeti zetu, miundombinu huteka zaidi ya Trilioni 4, wakati kilimo ni bilioni kadhaa, na hata hizo zinazotengwa humegwa na kuongezwa kwenye miundombinu. Magufuli ana obsession na miundombinu, na ana obsession na miradi isiyo ya lazima kama Dodoma na Chato, ambayo imegharimu matrilioni mengi. Hebu fikiri hayo yote yangeingizwa kwenye kilimo?

Katika kilimo, jambo muhimu sana ni muunganiko kati ya mkulima, vituo vya utafiti, na afisa ugani. Mkulima aimarishwe kwa mafunzo na ruzuku katika pembejeo. Afisa ugani apewe mafunzo makini, vitendea kazi, maslahi bora, athaminiwe, asimamiwe. Research centers kama Ukiriguru, Uyole, Naliendele, Tengeru, Mlingano, nk., ziimarishwe na kupatiwa fedha inayotakiwa kama ilivyokuwa hapo zamani.

Enzi za Nyerere vituovvya research vililindwa sana kama mboni. Magonjwa kama ya migomba huko Bukoba yanayotamba sasa, ingekuwa kama zamani wangeshakuja na ufumbuzi. Hata hii nguvu ya GMO isingekuwepo. Tumepiga marufuku GMO, lakini kiutafiti tupo vizuri? Vituo vya utafiti vimetelekezwa.
Nadhani umeelewa kwa nini napiga kelele. Magufuli angeelekeza hasira zote kwenye kilimo, tungevuka
 
Comedy phase 3.

Wazungu wamefanya utafiti wa kiyasansi wewe unasema haukubaliani nao na unaagiza waganga wa jadi wafanye utafiti na baada ya wiki 2 wanakuletea vichupa vya dawa unakubali.
Wazungu wenyewe Wapigaji tu,usizani wanakupenda sana,wanapenda tu hicho ulichonacho!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Comedy phase 3.

Wazungu wamefanya utafiti wa kiyasansi wewe unasema haukubaliani nao na unaagiza waganga wa jadi wafanye utafiti na baada ya wiki 2 wanakuletea vichupa vya dawa unakubali.
Utafiti upi huo ambao wewe kapuku unaukubali wakati wazungu wenyewe wanapingana?


''Spain's country's health chiefs have authorised the use of the drug to inoculate people aged between 18 and 55. However, they followed France, Germany, Italy and Austria in imposing age restrictions.''
 
Je, hao viongozi wa Wizara ya Kilimo wasio wabunifu huteuliwaje na ni nani huwateua?
 
Mzee wetu mbona hapendi kukutana na wakubwa wenzie? !! Ni nini mbaya wana CCM hebu tuoeni ufafanuzi!!
 
Kabudi ni mchekeshaji wa mfalme
Wakati Sauli Mfalme anatawala Israeli ya kale kulikuwa na watu kazi yao ilikiwa ni kumwimbia mfalme ili afurahi na baadaye apate usingizi na wao kukiowa ujira..... ndiyo hawa sasa kina kabudi katika Tanzania ya leo.
 
Hapa namuunga mkono Pro majalala. Africa inaweza kuanzisha na kuendesha chombo kama hicho. Kila nchi ikichangia Tsh bilioni moja kila mwaka tunapata Tsh 54 bln. Hizo zinatosha kuanzisha taasisi ya kutafiti tiba na chanjo ya magonjwa yanayoisumbua Africa.
 
Idiot.
 
COSTECH kimsingi wanafadhili tafiti, hawafanyi utafiti moja kwa moja. Ile ni Tume ya Sayansi na Tekinolojia. Kwa maoni yangu, imepitwa na wakati kimuundo, na pia haipati Bajeti ya kutosha, na ndio maana haishangazi kwamba wasomi wetu kwa asilimia kubwa wanahangaikia scholarship toka nje na sio COSTECH.

NIMRI ingeweza kusaidia, lakini tatizo vipaumbele vyetu ni nini? NIMRI wanaongozwa na sera zipi? Wanatengewa bajeti ya kutosha?

Sasa hivi kuna maendeleo makubwa sana katika sayansi ya tiba. Tunahitaji watanzania wenye vipaji wapate elimu bora katika basic science, kisha tuwapenyeze kwenye maabara kubwa za utafiti za nje, na kisha ndio tuwawezeshe hapa kwetu. Hiyo pekee inahitaji mikakati, political will, na bajeti.

Tunahitaji pia kutumia kikamilifu ujuzi wa jadi na kuuendeleza. Kweli kuna vitengo vya tafiti za dawa asili Muhimbili, nk. Lakini havijapewa umuhimu mkubwa kwa maana ya mafungu, mikakati na vipaumbele.
 
Huyo Magufuli alikinywa kikombe cha babu hakukidharau yuko mzima wa afya na ni Raisi wewe ambaye hukukinywa mbona uko choka mbaya tu maisha umepigika
Inawezekana shida zooote ndio zilianzia hapo kwenye kikombe cha babu. Ndio maana nchi inapelekwapekekwa tu
 
Hujui usemalo. Pale chuo kikuu Dar kuna rundo la tafiti, kweli, lakini ni nani anatakiwa kuzifanyia kazi? Hata PhD ya Magufuli kuhusu korosho, ipo pale.

Nchi za wenzetu, sekta binafsi imeimarika, inaagiza na kulipia tafiti katika vyuo vikuu, na inazinunua zile wanazohitaji.vkwa nchi yetu ni juu ya serikali kuchochea hali hiyo. Bila hivyo hatutoboi
 
Comedy phase 3.

Wazungu wamefanya utafiti wa kiyasansi wewe unasema haukubaliani nao na unaagiza waganga wa jadi wafanye utafiti na baada ya wiki 2 wanakuletea vichupa vya dawa unakubali.
Tutauona huo utafiti wa kisayansi matokeo yake Mkuu.
 
Comical Ali.

Wafanye utafiti kikombe cha babu alichokunywa Jiwe.
Na kile cha Madagascar, alichokunywa Kabuti Kalamaganda; mwokotwa 'Jalalani'.

Jambo ninaloweza kumsifia Magufuli kulifanya kwa ufanisi, ni namna anavyowaibua na kuwatambua 'comical Ali' wake na kuwaweka sehemu sitahili. Kuna yule msemaji wa serikali Abas, hata Ali waSaddam hamfikii! Na Popole je, kakalia sehemu inayomkaa vyema ndani ya CCM kwa nyakati hizi.
 
 
Hili suala la covid-19 lina ukakasi mwingi sana:
1. Tusidanganyane hii kitu imetengenezwa, mbona dunia haizungumzii walio sababisha hili balaa
2. Kwao huko ndo madhara ya corona ni makubwa sana, kwa nn wanahimiza kila mtu achanjwe? Huoni issue ni biashara hapo.
Yako mengi ya kujiuliza mwisho wa siku raisi ana access na intelligence information. Nadhani anapo ongea anavigezo.
Ushauri:
Kama nchi moja moja tumeona udhaifu mkubwa sana kwenye sector ya afya. Ni wakati wa kuwekeza huko.
Pia tufafiti dawa asili na zitumike kitaalamu.
Kwa leo yanatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…