Nimefuata ushauri wako.
"An invitation to treat is an invitation to a party or parties to make an offer. However, unlike a contractual offer, there is no intention for the invitation to treat to be legally binding. This is until the parties take steps to formalise the offer in a binding contract."
Kwa maana hii kama IGA ni Invitation to Treat basis sio legally binding. Kwa maneno mengine hakuna consequences kama URT itaamua haiutekelezi. Kwa maneno mengine article 23 haina maana yeyote kwa sababu URT wana uhuru wa kutoitekeleza wakati wowote bila kwenda Johannesburg. Na kumbuka article hiyo inazungumzia IGA, sio HGA.
Nilivyoelewa mimi hizo invitations ni yale mazungumzo yaliyofanyika Dubai na IGA ni mkataba ulio yaformalise. Hamna haja ya kupata baraka za Bunge kwa ajili ya mualiko wa kuanza mazungumzo. Baraka zinahitajika unapoingia katika mkataba ambao una masharti ya utekelezaji.
Amandla...
Nadhani umeshawai kukutana na hii phrase before ‘a contract is an agreement, but not all agreements are contracts’.
Kwanini, hapo mkataba unaozungumziwa ni commercial agreement. Ili uitwe commercial agreement (contract, kuna test zake na ya msingi ni consideration). Ambayo kwenye hiyo IGA aipo.
Hiyo article kwanza kabisa aizungumzii IGA per se, inachozungumzia ni HGA and project activities/agreements. Kwamba wakisha ingia hiyo mikataba (commercial agreements) huko mbele ndio aiwezi vunjwa kiholela.
Kwa hivyo hiyo framework ya IGA itatumika mpaka taratibu za kuisha kwa hayo makubaliano watakayoingia kwenye commercial agreement. Kwanini hiko kipengele kimewekwa kwasababu ndani ya IGA article 20 imeelezea namna ya kutatua dispute resolution.
Sasa basi mkataba wa kibiashara (hizo agreements) watakazo ingia baadae una implied terms kadhaa ambazo ata usipoziweka kwenye hiyo mikataba zinatumika mahakamani; laws za nchi husika, precedence’s (case laws) and industry customs.
Hiyo IGA imepitishwa na bunge ni sheria (moja kwa moja inakuwa implied term) ata mambo yake usipoweka kwenye mikataba ya baadae wanasisitiza hiyo sheria itatumika mpaka commercial agreements zote zitakapoisha.
Na hakuna commercial agreement inakufa kishamba ata mzazi akipangisha nyumba akifa kesho, watoto awawezi kwenda kuwatoa wapangaji kiholela kabla ya muda wa mkataba kuisha ndio kinachoongelewa hapo kwenye 23 (4) sentensi ya kwanza. Na ya pili inakwambia ukitaka kufanya mabadiliko yoyote lazima ufuate taratibu walizojiwekea article 20.
Shida yenu ata abc ya contract law amna, wataalamu wa serikali wakiwaelezea amtaki mmekazana tu. Mnasoma vitu amuelewi their legal meaning nyie mnatoa tafsiri kutoka vichwani kwenu.