Msimlaumu kocha Robetinho, hakuna kocha asiyependa kumpanga mchezaji mzuri, Ni maelekezo kutoka juu ya kuyatii bila shuruti

Msimlaumu kocha Robetinho, hakuna kocha asiyependa kumpanga mchezaji mzuri, Ni maelekezo kutoka juu ya kuyatii bila shuruti

Phiri atetewi na mtu bali anajitetea mwenyewe, point sita za Simba kwenye mechi ngumu ni Phiri ndiye aliyezikusanya kwa utulivu wake na shabaha la goli. Mimi sio mshabiki wa Simba ila huyo jamaa ana chuki na Phiri pamoja na Usimba wake.
Sijui Phiri akifunga huwa anainuka kushangilia au ana kunja sura.
Robertinho ana chuki zawazi tu na Phiri, ukiwa na mchezaji kama Phiri ni lazima utafute mfumo ambao utamfaa mchezaji ili akupe mafanikio kwakua ni mchezaji bora...

Robertinho yeye mfumo wake ndio huohuo tu mmoja habadiliki, kuna mechi cheza na 442 Phiri anakua second striker Chama au Saidoo mmoja anapumzika.kuna mechi ingia na 433 hapo Phiri anasimama kwakua kuna utatu ni lazima kunakua na hatari.

Simba haina kocha na siku mambo yakianza kubackfire itakua hatari watu watachapana fimbo.

Simba imefeli tena kwenye usajili wachezaji hawana mibadala sahihi hasa kwenye beki na midfield ndio maana kung'ang'ania na hao hao tu kila siku mpaka wananoki,ukiongeza na uoga wake wa kubadili wachezaji ndio kabisa.

Kuna mido kasajiliwa Hamis abdala alichezaga kenya ni mido mzuri tu lakini hamtumii, anajua akimtumia akaonesha ubora atakua pressured na washabiki aendelee kumtumia.
 
Hilo swali nimemjibu mwenzako kitambo sana humu humu na kaishiwa hoja katulia we kolowizard ndo umekurupuka nalo mda huu. Goli la Feitoto Kirumba ni mara mbili ya goli la Kibu na liliwalaza na viatu na goli la Bishoo Inonga lilipatikana kwa Simba kupiga Kona ya kimagumashi na kuvizia kupiga Kona bila filimbi ya refa!

Jiangalie mbumbumbu una tatizo la kuwa nyuma ya mda! Angalia usirithishe wanao tabia hiyo!

Kolo be careful Kuna siku utaamka ukimbie mbio Msimbazi kwenye sanamu la Rage mwenye akili peke yake Simba kuwahi pepa ya "national exam" unakutana na kina Kibu kukurukakara , Mzee Boko, Mzee Saidoo, Bishoo Inonga na Ayubu mdaka panzi wanarudi home, washakufa kiume kwa kushindwa maswali , pepa ishapigwa!!

Nawakumbusha wanathimba Makolokwinyo mbumbumbu wahed kuwa hamna kombe lolote hata la kuku kwa misimu miwili na huu ni wa tatu! Kwasasa inachoweza Simba ni kusindikiza madume ya mamba kwenye safari zao za ligi!! Ngao ya jamii ni mbao ya kupewa baada ya mechi mbili tu sio marathon kombe la ligi! Sasa Simba pigeni mavuvuzela tani yenu jisifuni tani yenu ila Yanga gari limewaka na Yanga inasema, Max Nzengeli and Ki Aziz actions speak louder than makelele ya Simbas!

Hatuoni Tena nyuzi za Simba kujisifia kufurushwa safari ya madume ya mamba ya African Super cup league! Simba wote kimyaaaa mavuvuzela chini ya uvungu, ila tulishasema sana Simba ni debe tupu fc litavuma Dunia nzima ila mechi zake mbili tu na ikawa kama Kawa mkafa kiume kwa mara nyingine Tena!

Yanga oyeee!
Unaonekana ulikua ni vitu vizuri vya kuelezea lakini ushabiki umeweka mbele, inanifanya nikubaliane na maneno ya Manara kwamba Yanga ni wawili tu, babaake mzee Sunday na Kikwete basi!!!!
 
"MASHABIKI YA YANGA NI MAMBWA HAKUNA LOLOTE YANALOJUA KUHUSU KANDANDA ILA MUDA WOTE YANAZOMEA TU UTADHANI MANYANI"

- DR LUC EYMAEL 2020
Mambwa yanayoshangilia Pira GAMONDI, Pira burudani, ushindi wa kihalali sio wa kubebwa na marefa na makombe!! Rejea goli la halali la Singapore Big Stars waliloipiga Simba na kukataliwa!
 
Unaonekana ulikua ni vitu vizuri vya kuelezea lakini ushabiki umeweka mbele, inanifanya nikubaliane na maneno ya Manara kwamba Yanga ni wawili tu, babaake mzee Sunday na Kikwete basi!!!!
Uko sahihi! Wenye akili Yanga wawili tu!

Ukisoma my comments kishabiki hutaelewa nilichoandika ila ukichambua vizuri ukaweka ushabiki pembeni utapata kitu angalau kimoja mf Simba Ina makelele mengi ila Haina kombe lolote misimu miwili na inacheza potelea mbali bila fomesheni Kila mtu kivyake magoli ya kulazimisha Kwa tabu , mengine ya kupewa na marefa , hapo ushabiki hamna

Marefa wanaua spirit ya timu ndogo zinapocheza na Simba Kwa kuwaonea kwa kuwapa kadi za uonevu na kuwanyima faulo na magoli Yao na kuwapa Simba penati za mchongo, rejea kipyenga Cha mwisho Othman Kazi akichambua madudu ya marefa wetu wasioitwa nje kuchezesha, hapo ushabiki hamna!!

Yule kolo Mkuu , Mr Karai anataka Simba ibebe kombe la ligi msimu huu Kwa lazima na Yanga tushamshtukia tutaua plan yake Kwa kuikanda Simba ndani nje point 6 zote zetu hapo ushabiki hamna!!
 
Phiri Hana mpira wowote kama walivyo wachezaji wengine wote wa Simba hii mbovu, Phiri akija Yanga anapelekwa Yanga B! Jana kafunga goli kindondokela tu kwa papara za kipa wa Ihefu kuwahi kutoka bila akili maana Kuna mabeki wawili wa Ihefu walikuwa wakimkaba na asingepiga! Diarra humfungi magoli ya kijinga ya short range kama lile, hutulia na kumsoma mfungaji! Mwaka huu Diarra ataongoza kwa clean sheet Duniani!

Goli la Phiri Jana halikuwa goli la kiufundi kama yalivyo Yale magoli ya Max Nzengeli au Mayele!!

Hata goli la Baleke la kwanza Jana Simba vs Ihefu halikuwa la kiufundi! Na dizaini kama vile magoli ya Simba ni magoli ya kichawi! Magoli ya kichawi Huwa hayafuati formula ya goli linapatikanaje!! We utashtukia tu gooooal!! Mnabaki mnaulizana nani kafunga wakati wote mmetumbua macho mkiangalia mpira!

Simba imeshuka kiwango na kuwa sawa na timu zingine ndogo za ligi kuu, kinachoibeba ni juhudi binafsi za mchezaji mmoja mmoja, marefa na uchawi basi, ushindi wa Simba kwasasa ni wa tabu na kulazimisha. Timu zikikomaa kuifunga Simba mbovu marefa wanazilegeza mfano Singida Big Star walipiga goli safi la kideoni, goli halali muda ukiwa umeenda refa na kibendera wakalikataa kwa kujaa ujinga eti kuibeba Ili Simba ishinde na ndo maana marefa wa bongo hawaitwi kuchezesha michuano ya CAF na Fifa!!

Ukitaka kujua mpira wa miguu ni kibarua kizito angalia mechi za Simba hii mbovu wanahaha majasho kama yote haijulikani wanacheza fomesheni gani, ukitaka kujua mpira wa miguu ni rahisi sana na ni burudani basi angalia Yanga ikicheza na uhakikishe Skudu Makudubela yuko uwanjani!!

Simba hii inapuliza kweli kweli japo haitasaidia kipigo Derby Kiko pale pale maana Yanga ni haki yetu kukaa kileleni na kubeba Tena kombe msimu wa tatu!!

Kama wewe ni mbumbumbu kolowizard na hujakereka na hii comment from utopolo og basi piga piga makofi uende peponi ila pia now now nikurushie vocha ya kujaza bando la kuingia JF!
Uongooo,huo ni uongooooooo
 
Phiri atetewi na mtu bali anajitetea mwenyewe, point sita za Simba kwenye mechi ngumu ni Phiri ndiye aliyezikusanya kwa utulivu wake na shabaha la goli. Mimi sio mshabiki wa Simba ila huyo jamaa ana chuki na Phiri pamoja na Usimba wake.
Sijui Phiri akifunga huwa anainuka kushangilia au ana kunja sura.
Hawajui chochote hao,muwe mnawasamehe tu..tatizo wanajiona wanajua sana.
 
Back
Top Bottom