momentoftruth
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 2,013
- 2,089
Robertinho ana chuki zawazi tu na Phiri, ukiwa na mchezaji kama Phiri ni lazima utafute mfumo ambao utamfaa mchezaji ili akupe mafanikio kwakua ni mchezaji bora...Phiri atetewi na mtu bali anajitetea mwenyewe, point sita za Simba kwenye mechi ngumu ni Phiri ndiye aliyezikusanya kwa utulivu wake na shabaha la goli. Mimi sio mshabiki wa Simba ila huyo jamaa ana chuki na Phiri pamoja na Usimba wake.
Sijui Phiri akifunga huwa anainuka kushangilia au ana kunja sura.
Robertinho yeye mfumo wake ndio huohuo tu mmoja habadiliki, kuna mechi cheza na 442 Phiri anakua second striker Chama au Saidoo mmoja anapumzika.kuna mechi ingia na 433 hapo Phiri anasimama kwakua kuna utatu ni lazima kunakua na hatari.
Simba haina kocha na siku mambo yakianza kubackfire itakua hatari watu watachapana fimbo.
Simba imefeli tena kwenye usajili wachezaji hawana mibadala sahihi hasa kwenye beki na midfield ndio maana kung'ang'ania na hao hao tu kila siku mpaka wananoki,ukiongeza na uoga wake wa kubadili wachezaji ndio kabisa.
Kuna mido kasajiliwa Hamis abdala alichezaga kenya ni mido mzuri tu lakini hamtumii, anajua akimtumia akaonesha ubora atakua pressured na washabiki aendelee kumtumia.