Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kuna baadhi ya watu wanashangaa ukengeufu wa Msigwa. Wengine wanahoji kama ana utimamu wa akili ama kawehuka.
Lakini lazima tukubaliane kuwa sote kama watanzania tunao ujinga wa kihalaiki.
Ujinga wetu mkubwa ni kuwategemea sana wanasiasa kusimamia maslahi yetu bila sisi kuwasimamia wao.
Matokeo yake ni wanasiasa ndiyo wanapanga watupe nini badala ya sisi kuwataka watupe tunachotaka.
Ndani ya vyama vyote vya siasa kujiunga na chama ni hiyari kama ilivyo kutoka.
Lakini hizo zinazoitwa Kamati Kuu huwa zinajiamulia mambo kuhusu vyama vyao bila ya kuwashirikisha wanachama wao na milango ya kuhoji kwa wanachama wa kawaida ama imefungwa au iko mbali sana kufikiwa.
Sasa Msigwa amekuwa kama samaki aliyevuliwa na Kamati Kuu ya CCM.
Kamati Kuu ya CCM Sasa ndiyo inayoamua imtumieje Msigwa dhidi ya CHADEMA na wala si wanachama wa kawaida.
Kama kwenye "makubaliano" yao Msigwa atapewa nafasi fulani basi hakuna mwana CCM anayeweza kuzuia au kukataa.
Kwa ivo mvuvi ndiyo huamua kama samaki auzwe au aliwe supu.