Msimu 2023/24: Bajeti Yanga Bil 20, Bajeti Simba Bil 13.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Naanza kuona matunda ya Uongozi wa Eng Hersi Saidi. Alipoingia Yanga alikuta timu iko kwenye bajeti ya Bil 6. Kwa uongozi wake mathubuti jamaa ameweze kuibua vyanzo lukuki vya mapato.

Mpaka sasa Yanga ina wafadhili 9. Idadi kubwa ya independent sponsors kuliko klavu yeyote hapa Afrika Mashariki.

Kupitia hapo Yanga sasa inaweza kugenerate fund ambayo ni sawa na asilimia 70% ya thamani ya hisa za timu ya Simba SC, tena kwa msimu na wala sio lifetime.

Wakati Simba SC ikiwa na Matarajio ya Bajeti ya Tsh Bilion 13 katika msimu ujao, wenzako wameandaa Bilion 20 kama Bajeti. Hapa tunazungumzia Bilion 7 zaidi.

Yanga inaendelea kuchochora mawinguni in terms of mapato, taarifa zinaonyesha Gate collection Yanga imeongoza kwa msimu wa 3 mfululizo, kwenye upande wa sponsorship deals ndio usiseme, huko kwenye prize money ndio wameziokota vibaya mno.

Naiona Yanga SC ikifikia ndoto za kuwa Klabu ya Millenium mapema zaidi kuliko klabu yeyote ile kusini mwa Jangwa la sahara.

Shukrani ziwafikie Viongozi wote wa klabu kwa kutufikisha hatua hii ya mfano ambayo inatamaniwa na walio wenye, mmepambana kwenye kila idara kuhakikisha mambo yako perfect.

(Pichani ni Genius Eng Hersi Said)
 
Wewe ni Hersi mwenyewe au mchepuko wake? Muwe mnajitangaza mapema
 
Alianzisha tabia ya uchawa Tanzania alaaniwe milele na kama ameshakufa afukuliwe maiti yake icharazwe viboko. Nchi hii imekuwa ni vijana wa hovyo
 
Uchambuzi mzuri ila tu nauliza, hamuwezi kuzungumzia mambo yenu bila kuihusisha club kubwa afrika ya simba? Mbona mna mengi sana ya kuyajadili ya club yenu?

No wonder msemaji anaeongoza kuitaja simba kila akipata nafasi ya kuzungumzia mpira ni Ashura ma UTI kamwe aliyekaa paleee utopoloni, ahmed ali atasubiri.
 
INAONYESHA SIMBA INAWAKAZA BARABARA, HUWEZI UKAKAA BILA KUMTAJA MWANAUME WA MBUGA MNYAMA MKALI.

KABWILI FC.
 
Unaleta siasa kwenye mpira.

Pongezi zinastahili panapo stahiki.
Umeonekana chawa sana brother kama umepita shule makala yako iko very subjective sana hata mtoto mdogo akiisoma anaona kuna harufu ya kumpromo mtu mmoja wakati mafanikio ya taasisi yoyote yako chini ya watu wengi sana
 
Kama kuna mtu wa uchumi kwa hawa ndugu zetu yanga hebu ajitathmini vizuri mana hata kama ni biashara sidhani kwa huu uwiano kati ya MAPATO NA MATUMIZI ..Au kama wenyewe wamechukua chao huenda tunaweza kuelewa maana NYUMA YA PAZIA HUWA KUNA MAMBO MENGI
 
Umeonekana chawa sana brother kama umepita shule makala yako iko very subjective sana hata mtoto mdogo akiisoma anaona kuna harufu ya kumpromo mtu mmoja wakati mafanikio ya taasisi yoyote yako chini ya watu wengi sana
Mtu kama Eng Hersi haitaji Thread yangu kuwa promoted.

Murtaza Mangungu ndiye mwenye kuhitaji promo.kwa sasa.

Kizuri chajuiza.
 
Hahahah we utakuwa ndiyo yule jamaa alisimama jana akasema "yaani siwezi hata kuwasifia viongozi maana naweza kuliaaa"
Yule jamaa anaipenda sana Yanga SC.

Ana uchungu sana na klabu.

Ana shukrani kubwa sana kwa viongozi wake.


Natamani kuwa kama yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…