Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!
Kwanini Nasema Azam au Simba mmoja wapo atakuwa Bingwa Msimu huu?
1.Kocha Fadlu Davis amekuwa kocha wa Simba huu unaelekea msimu wa pili;mazingira ya ligi Kuu tayari keshayajua,tayari kesha tambua na kifamu kikwazo Cha yeye kutochukua Ubingwa kilikuwa ni Nini!,Benchi lote la Ufundi limebaki kama lilivyo na hakuna kilichobadilika.
Hivyo naamini Kwa usajili alioufanya Kwa kuboresha na kuongeza wachezaji kadhaa,hii itakipa kikosi Cha Simba nguvu ya kutawala zaidi ligi Kuu msimu Ujao na kuweza Kuwa Bingwa,kama asipokuwa Bingwa basi atakuwa mshindi wa pili nyuma ya Azam !
2.Azam Fc ya Florent Ibenge inaonekana kama ni timu isiyopewa nafasi yoyote ya kutwaa Ubingwa kwasababu ni timu isiyokuwa na kelele nyingi kama zilivyo timu za kariakoo!
Azam kumleta Ibenge Kuwa kocha mkuu wamedhamiria kabisa kumaliza ukame wa makombe Kwa msimu huu,Ibenge ni kocha ambaye siyo mgeni sana Kwa timu za hapa Tanzania hasa Yanga & Simba,hivyo ujio wake naamini unakuja kuondoa ufalme wa hii miamba miwili ya Soka hapa Tanzania.
Azam inaonekana kama haishitui kwenye usajili wake lakini trust me,hii timu mwaka huu inakuwa Bingwa,kama isipokuwa Bingwa inakuwa nafasi ya pili nyuma ya Simba.
Azam hadi muda huu wako Kambini wakijifua kisawasawa Kwa ajili ya msimu mpya,wachezaji wa Ibenge mara nyingi huonekana kama hawana Majina makubwa lakini jamaa mbinuo zake huwa zinawaduwaza wengi !,naamini huu msimu atawashangaza wengi .
3.Yanga Africans hadi muda huu haijulikani kambi wataweka wapi na itakuwa lini,wakati timu nyingi Ulaya na barani Afrika zikiwa zipo kwenye maandilizi ya msimu mpya,Hawa Yanga wao haijulikani kambi wataianza lini !
Mimi ni mwanachama na shabiki wa Young Africans,nikiri kabisa kama Kuna jambo ambalo Uongozi wa Yanga umekosea ni kumuachia kocha Miloud Hamdu aondoke,kibaya zaidi tumeamua kuvunia benchi lote la ufundi na kuleta benchi Jipya !,Hili jambo litaigharimu sana Yanga msimu huu!
Yanga siyo timu ya kocha kuja kujaribu bahati yake !
Huyu kocha hawezi kuivusha Yanga kuingia Makundi klabu Bingwa Afrika !,Muda utazungumza !