Msimu wa mvua unakaribia, chukua tahadhari ya Radi

Msimu wa mvua unakaribia, chukua tahadhari ya Radi

Kuna watu wana ushahidi kuwa radi ni LIVING THING ORGANISM
 
Nilipokuwa mdogo tulikuwa tunaambiwa tuepuke kuvaa nguo nyekundu.
Sijui kama radi za sasa zinafuata pia nguo nyekundu?
 
Kwanini mokoa mingine ina radi kali zaidi?
Mimi ni mwenyeji wa arusha nilienda dodoma zile ngurumo zinatisha nilitamani kupaa kurudi arusha
 
Huwa ni nadra sana ndege kupigwa radi kwa sababu zimefungiwa teknolojia ya kuzuia radi.........
Sio kweli mkuu. Radi inapiga vizuri ndege na hata gari sema haileti madhara kwa kuwa hazigusi chini moja moja hivyo mfumo wa umeme unakuwa haujakamilika.
 
Kuna dada mmoja aliponea kwenye tundu la sindano..Mungu akitaka kukuepusha na janga hakuna kinachozuia.

Nafikiri ilikuwa 2002 mvua ilikuwa ikinyesha, iliambatana na radi, binti badala ya kwenda maliwatoni akaona arahisishe chini ya mti, pale kwao kulikuwa na miti mingi mirefu.

Ile kamaliza huduma tu radi ikatua pale alipokuwa, ikapasua mti katikati binti katoka mbio, ile anafika mlangoni tu radi hiyo ikatembea na mlango (Yaani ilikuwa kama movie) dada kajirusha ndani, radi ilipasua mlango. Dada akanusurika, mzima kabisa.

Haikuishia hapo ikahamia kwa jirani ikatoboa bati, kuna mmama alikuwa nje ikapita nae (Alizimia baadaye akawa sawa).

Baada ya hekaheka zote hizo, kufuatilia maeneo yaliyopigwa radi yamekwaruzwa kwaruza kama jogoo ndo kaparua parua.

Radi isikieni tu.
 
Watanzania wengi wamekuwa na uhusishaji hasi kati ya radi na matumizi ya simu za mikononi. Wengi wanaamini radi ina nafasi kubwa ya kuishambulia simu na mtu anayeitumia, lakini watu wajue kuwa radi haina sifa ya kushambulia vitu vidogo vidogo bali vitu virefu ambavyo vitafanya ile charge iweze kusafiri kwa kasi kuelekea ardhini.
So watambue kuwa ni salama kabisa kutumia simu hata kipindi cha mvua iliyoambatana na radi.
Unadanganya wenzako wewe,utasababisha watu wapoteze maisha kizembe,tafuta baadhi ya shuhuda zenye kuelezea waliokoswakoswa na radi kisa simu;
hapo sio kufata simu bali mawimbi ya mawasiliano ya simu;
na ndio maana vifaa vingi vya mawimbi utaambiwa haifai kutumia kwenye radi;
 
Mwanga radi usiku ikipiga jirani ni kama jua la saa 6
 
Unadanganya wenzako wewe,utasababisha watu wapoteze maisha kizembe,tafuta baadhi ya shuhuda zenye kuelezea waliokoswakoswa na radi kisa simu;
hapo sio kufata simu bali mawimbi ya mawasiliano ya simu;
na ndio maana vifaa vingi vya mawimbi utaambiwa haifai kutumia kwenye radi;
Sikatai ulichokisema ila nakuomba ujiongeze kimaarifa. Ila jua kuwa umeme wa zaidi ya 600000V haukosi kosi kama unavyosema bali huunguza na kupasua kila kilichopo ndani ya 5M.
 
Mwaka 2004 shule ya msingi katwe Buchosa, radi ilipasua mti katikati na kunyenyua paa la jengo...

2010 shule ya sekondari zakia Meghji Chato, radi ilipiga nguzo na kuipasua katikati.

Radi ni kitu naogopa mpaka kesho.
 
Kama huna mahali pa kukimbilia heri kukaa chini kabisa na kutosimama, huu kichwa mtu umeinamisha
Kwanini kondoo husumbuka sana kwenye radi je kuna tafiti zozote zinaendelea kuhusu uhusiano wa radi na kichwa cha kondoo?
 
Back
Top Bottom