Watu wengi wanajua wanachopaswa kufanya hapa duniani ili kubadilisha maisha yao na kugusa maisha ya watu wengine katika jamii,lakini changamoto kubwa wanashindwa kuanza kufanya chochote kwa hofu ambayo kimsingi haina mantiki yowote.
Hawa ni wale wenye shauku kubwa moyoni mwao kufanya jambo la pekee na hawafanyi lakini ukiwauliza watakupangia sababu nyingi za kuhalalisha kwa nini hawawezi kuanza na wala hawafanyi jitihada yoyote kuanza kuishi kile wanachosikia moyoni.
Karibu tena katika makala zetu za kujenga katika mtandao wetu. Kwanza nikushukuru sana kwa kuendelea kutuamini na kufuatilia kazi zetu. Kazi hii ina maana tu kwa sababu wewe upo.
Hebu muulize mtu ambaye ana wazo la kufanya kitu fulani ambacho moyoni mwake anashuhudiwa kabisa kitakuwa na mafanikio,”ni kitu gani kinachokufanya ushindwe kuanza na kuishia kuongea tu?” Wengi watasingizia hawana mtaji.
Ukosefu wa mtaji ni wimbo ambao watu wengi wasiokuwa na uthubutu wanauchukulia kuwa sababu ya kuwafanya washindwe kabisa kufanya chochote na kuishia kuwa na ndoto ambazo hazitakaa zitimie.
Lakini ukiwachunguza watu wa namna hii utagundua kwamba tatizo lao sio mtaji tu bali lipo tatizo la msingi ambalo wangepaswa kulishughuliakia kwanza,kwani nini? Kwa sababu mtaji halijawahi kuwa hitaji la kwanza katika uanzishaji biashara yoyote.
Hebu kwanza nikuulize;unahitaji shilingi ngapi kubuni na kufanya uamuzi kuanzisha biashara? Ni dhahiri hakuna senti hata moja unayohitaji,kwa hiyo yapo mambo ambayo unahitaji kuyashughulikia mwenyewe kabla ya kuhitaji kufikiria kuhusu mtaji.
Kupitia makala hii fupi nataka tutafakari pamoja mbinu chache na rahisi zitakazokusaidia kuanza kutekeleza wazo lolote la biashara au mradi ambao kwa muda mrefu umekuwa ukiuahirisha kuuanza.
WAZO
Kupata wazo la biashara,mradi au shughuli unayotaka kufanya ndicho kitu ambacho kinapaswa kuwa cha kwanza kufikiria. Kwa kutumia kipaji chako cha ubunifu ulichopewa na Mungu unatengeneza maono ya kile unachotaka kitokee mapema kabisa. Nio hatua ya kujitafuta kujua nafasi yako uliyoitiwa kufanya hapa duniani ni ipi?
Kupitia hatua hii unakuwa na picha ndani mwako ya namna ambavyo mradi au biashara unayotaka kuanzisha itakavyokuwa,Kwa lugha nyingine unauona mwisho tangu mwanzo na hii ni hatua ya mtu na imani.Kuna kitu ndani mwako unaamini unaweza kukibadilisha siku moja kuwa kitu dhahiri.
ANDIKA WAZO LAKO
N imesikia watu wengi wakisema nina mpango wa kufanya kitu fulani,au mradi nfulani kumbe ukweli hawana mpango wowote ila wazo. Ili uwe mpango lazima sasa uhamishwe kutoka kichwani hadi kwenye karatasi. Kichwani hukaa wazo na mpango huwekwa kwenye karatasi. Kwa hiyo hatua ya pili ni kulitafsiri wazo au maono kwenye maandishi. Kwa hatua hii unahamisha maono kutoka picha uliyokuwa unaona pekee yako kwa macho ya ndani na sasa unaitafsiri kwenye karatasi kiasi kwamba hata mtu mwingine anaweza kusoma maono yako.
Hatua hii itahitimishwa na kuandika mpango wa wazo lako ambayo itakusaidia kujua unahitaji nini kwa maana ya rasilimali zote zinazohitajika ili kutimiza maono yako ikiwemo muda na kuainisha vipaumbele vyako.
Hapa pia utapima nguvu uliyonayo na mapungufu yako.Na kwa kufanya mambo hayo mawili ni dhahiri kwamba umekwisha anza safari yako ya kuelekea unakotaka kufika na hapo kwanza unaweza usiwe na hitaji lolote la fedha ikiwa kila kilichopo hapo juu kiko ndani ya uwezo wako.
ANZIA PALE ULIPO
Watu wengi wanashindwa kuanza kufanya chochote kwa kigezo tu cha kusubiri mpaka watakapokuwa na mtaji wa kutosha kwa kuwa hawana tu macho ya kuona thamani ya kile walichonacho mkononi. Kwa kifupi hakuna mtaji mdogo wala mkubwa mtaji wowote unafaa kuanza kitu kwa ukubwa unaolingana na nguvu yako.
Kitendo cha kuona kila fedha unayomiliki ni ndogo sana kukuwezesha kuanza kufanya biashara au mradi wa ndoto yako utachelewa kuanza mambo mengi. Kwa mtindo huu watu wengi wamezeeka na kufa bila kuanza kauishi maisha yao.
Hebu nikuulize,kama huna uwezo wa kuthamini kidogo ambacho kiko mkononi mwako unafikiri ni nani atakayekuwa tayari kukwamini kwa mambo makubwa? Haiwezekani mpaka pale utakapokuwa mwaminifu kuthamini kile ulichonancho.
FANYA UNACHOWEZA
Huenda ikawa unatamani kuanza kwa kishindo lakini ukweli ni kwamba rasilimali ulizo nazo hazikuwezeshi kuanza kwa kishindo.Ushauri wangu ni kwamba badala ya kuendelea kusubiri kufanya unachotaka,anza kufanya unachoweza na utaona kwa kufanya hivyo utajifunza sana katika safari hiyo uliyoanza kidogo kidogo.
Kuna tofauti kubwa kati ya kutamani kufanya unachotaka na kufanya unachoweza kufanya.Kufanya unachotaka ni pale unapofanya bila kuwepo na vikwazo vyovyote na kufanya unachoweza ni pale unapofanya tu kile ambacho kiko ndani ya uwezo wako hata kama una uwezo wa kufanya zaidi.
Anza kidogo kidogo huku ukiwa na picha kubwa mbele yako ambayo unaiendea.Rudia na kurudia na utaanza sasa kupata wateja wadogo, mwisho utaanza kupata wateja wakubwa,utapata fedha na fedha yako itakua siku kwa siku.
Utaanza kujijengea heshima kwa watu na taasisi mbalimbali za fedha pia,miongoni mwao watakuja kukushauri namna gani unaweza kufanya biashara yako na kupata mtaji mkubwa ambao ulikuwa unatamani kuwa nao hata kabla ya kuanza.
Kama ni biashara sasa unajua soko,na mahitaji yako pia unayajua uwe na uhakika utakuwa katika nafasi nzuri sana ya watu kukusikiliza ukiwasilisha hoja yoyote ya kuhitaji uwezeshwaji wa fedha au raslimali zingine. Nakushauri anza bila visingizio anza.Kama biashara anza.kama ni kitu cha kipaji anza,kama ni chochote unachoaka kuanza aacha visingizo.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi.Ukiwa na uhitaji wowote wa ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasili nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno,whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.
MSDK PJ