Msingi wa Umoja wa Taifa letu aliotuachia Mwalimu Nyerere umeanza kumomonyoka kwa kasi kubwa

If they deliver and Tanzania uchumi unaimarika hamna shida. Ila kama watashindwa waondolewe haraka
Usijenge hoja ya kujustify huo upendeleo wa ukanda uliokithiri kwenye uongozi wa awamu hii ya 5

Jambo la muhimu ni kutoa fursa kwa maeneo yote kwa kuwa wote ni watanzania
 
Na tumefikia hapa tulipo kutokana na WABUNGE WA CCM. sharia nyingi OVU wamekuwa wakipitisha wao kwa kuona kama vile wanawakomoa UKAWA kumbe wanaikomoa nchi yao! Mfano hata mikataba ya gesi na mafuta iliyopitishwa na wabunge wa ccm kwa hati ya dharura ni OVU na haina tija kwa taifa kama ilivyokuwa ya madini. UKAWA wamekuwa makini sana Bungeni tofauti na ccm ambao ndio wengi.
Ni kweli kabisa Taifa hili limefikia hatua hii kutokana na wabunge wa CCM kupitisha mikataba mibovu......
 
Mkichagua rais angalieni awe angalau mtoto wa mjini au hata kasoma nje.
Hawa washamba waliotokea uswekeni kwenye shida wenye Ph.D za kuunga unga Manzese pale tabu sana.
Angalia wasije wakakuita mchochezi.....
 
Hu
Fear of the unknown due to political biasness, Umoja wa hili taifa umeletwa na Mungu, huyo Nyerere alitumiwa tu, kama JPM ataperform vizuri after ten years and we citizens find it necessary aongezewe muda, kura zitapigwa, ataongezewa kura zikiruhusu.
Hatuwezi poteza kiongozi efficient kisa katiba ya kwenye karatasi iliyotungwa na binadamu
Huyu mbaguzi,fala,mshamba ndo efficiency?mboma hamuoni ujinga wake?
 
Huwo ushauri wako ulipaswa uwape Wachaga wenzako waliotaka kumuua huyo huyo Nyerere ili wao watawale, nani alijaribu kumpindua Nyerere kijeshi ? Ni Wachaga, nani ana Chama cha Siasa ambacho kinapigiwa kura kwa 100% na watu wa ktk eneo moja? Ni Wachaga, hivyo shut the **** up!
Serikali yenu ya chuki. Kama wewe ndo unawakilisha hoja za wakuu wako kuna tatizo mahali
 
Kufikiri kwamba kazi ya ujenzi wa umoja wa kitaifa iliisha enzi za Nyerere na sasa tunaweza kudharau misingi iliyotupatia umoja huu ni makosa makubwa sana.

Umoja wa kitaifa kwa kawaida hupungua kadiri muda unavyoenda mbele. Hata kama kuna jitihada kubwa sana kupunguza mmomonyoko huu.Hii ni kanuni ya asili. Hata nyumba uliyomaliza kuijenga itataka kuipiga rangi na kuziba nyufa mara kwa mara. Itakuwa kitu kikubwa na chenye utata kama taifa?

Dharau hii ndiyo iliyoanzisha kumomonyoka umoja tangu enzi za Mwinyi.

Na sasa inaonekana kama tumetoka kwenye kudharau misingi ya umoja wa taifa, tunaona viongozi wanapanda mbegu za kutugawanya rasmi.

Ninasikitishwa sana na kauli za rais mstaafu Mkapa anapowaita baadhi ya Watanzania wapumbavu kwa sababu wako chama tofauti na yeye tu.

Hawa kina Magufuli wamekuja juzi. Wana elimu za kuungaunga. Wamekulia shamba. Hawajawahi hata kusoma nje. Wakikosea naelewa kwa nini. Ni washamba.

Mkapa alikuwepo serikalini tangu miaka ya sitini. Kabla Kambona hajaondoka. Amefundishwa na Nyerere Pugu. Kasoma Columbia. Kakaa New York. Kakaa Canada. Anajua mambo yanavyoenda dunia hii. Kaamua kujitoa akili tu kwa sababu za kisiasa.

Kama mtu kama Mkapa kaingia katika mtego huu, nina shaka sana na mustakabali wa nchi hii.

Sent from my Kimulimuli
 
Ninakushukuru sana Mkuu kwa uchambuzi wako makini sana.....

Lakini usishangae wale Lumumba buku 7 team wakakushukia na matusi......

Kwa kuwa hao jamaa zetu wakiishiwa na hoja wanakimbilia kwenye matusi!
 
Hu

Huyu mbaguzi,fala,mshamba ndo efficiency?mboma hamuoni ujinga wake?
Usije shangaa DC wako akakushukia na kudai kuwa umemtukana Mkulu.....

Lakini cha kushangaza Mkapa katutukana watanzania kuwa ni wapumbavu, lakini nashangaa DC wa Chato hajaamrisha Polisi wamkamate huyo jamaa na kumsweka ndani kwa yale masaa 'yake' 48!

Kumbe sheria za nchi hii zina macho na zina double standard ya hali ya juu....

Majuzi tu Halima Mdee kawekwa ndani kwa zaidi ya masaa 48 ya DC Hapi kwa kile kilichodaiwa kamtukana Rais kwa kusema tu kuwa kauli anazozitoa Rais anazichukulia kuwa zishakuwa sheria!
 
Bila uchochezi kwa Watanzania wengi moto wa kupikia hauwaki na watoto watalala na njaa.
Una maana kula yao Inabidi wafanye uchochezi ili waingie kwenye payroll?

Basi malipo ya aina hiyo yatawapeleka kuzimu....
 
Mnaomlaumu Ndugai mnamwonea kabisa, ameagizwa kufanya hivyo na hata pa kutokea. Mbaya zaidi ni pale tunapoanza ubaguzi wa ukabila, kiasi kwamba mkuu wa nchi anaweza kuhutubia umati wa watanzania kwa kisukuma ni hatari sana, maana hili halijawahi kutokea katika nchi.
Moja ya misingi muhimu kabisa kwa Taifa lolote duniani ni Umoja wa kitaifa wa Taifa hilo.

Muasisi wa Taifa hili Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alituachia urithi muhimu sana kwa Taifa letu ambao ni kuwa na Umoja, ambapo nchi yetu haikuwa na ubaguzi wa kikabila, Imani za dini au itikadi za kisiasa.

Kwa bahati mbaya, kwenye serikali hii ya CCM ya awamu ya 5 kumekuwa na viashiria vya mmonyoko mkubwa unaohatarisha msingi huo wa Umoja wetu wa nchi kitaifa kutokana na nchi kuendeshwa kwa kubaguana kutokana na itikadi za kisiasa.

Kwa Bahati mbaya vinara wa kubagua wananchi kwa itikadi za kisiasa imekuwa ni mihimili 2 ambayo ni Bunge chini ya Spika Ndugai na mhimili mwingine ni utawala ambapo unaongozwa na Mkuu wa nchi mwenyewe.

Hebu nianzie na mmonyoko wa Umoja wa kitaifa unaofanywa na Spika wa Bunge letu pamoja na wabunge wa CCM ambao ndiyo walio wengi Bungeni.

Moja ya jukumu lake la msingi la Bunge lolote ni kuisimamia serikali iliyoko madarakani kwa niaba ya wananchi waliowachagua kwa kuikosoa kwa yale mambo ambayo serikali hiyo haiwafanyii vyema wananchi wake.

Kwenye Bunge letu ambalo lina makundi mawili, kundi la wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ndiyo wengi na wabunge wenzao wa upinzani ambao ni wachache ambapo mara nyingi imeonekana kuwa wabunge wa upinzani ndiyo wamekuwa wakitekeleza kikamilifu wajibu wao mkuu wa kuisimamia serikali, huku wabunge wenzao wa chama tawala cha CCM wakiamini kuwa wajibu wao mkuu wakiwa Bungeni humo ni kuikingia kifua serikali yao iliyoko madarakani

Kutokana na kukinzana kwa fikra hizo kumekuwa na mitafaruku isiyokwisha Bungeni humo.

Nitatoa mifano michache kuonyesha namna gani wabunge wa upinzani wamekuwa wakitimiza jukumu lao la kuisimamia serikali na wenzao wa CCM wamekuwa wskiikingia kifua serikali yao ya CCM.

Tuanzie na Bunge kuonyeshwa live. Siku za nyuma tokea nchi yetu iingie kwenye mfumo wa vyama vingi Bunge letu limekuwa likionyeshwa live, lakini mara tu serikali ya awamu ya 5 ilipoingia madarakani ikapeleka hoja Bungeni la kusitisha Bunge kionyeshwa live na sababu kuu iliyotolewa ni kuwa muda huo ambapo Bunge linaonyeshwa live ni muda ambao wananchi walio wengi wanakuwa makazini kwa hiyo wanatakiwa wakati huo wachape kazi badala ya wakati huo kuwa kwenye luninga zao kuangalia Bunge live.

Hata hivyo hoja hiyo ya serikali imedhibitika kuwa ilikuwa ya uongo kwa kuwa tumeshuhudia media mbalimbali nchini zikifanya live coverage kwa matukio ya Mwenyekiti wa CCM Taifa anapofanya ziara mbalimbali nchini ambapo katika ziara hizo zinakuwa '2 in 1' kwa maana zinakuwa za kiserikali na pia za kichama.

Sasa kama hoja ilikuwa Bunge halionyeshwi live ili watu wafanye kazi badala ya kuangalia luninga, mbona kwenye hizi ziara za Mwenyekiti wa Taifa CCM vyombo vya media vinatoa live coverage wakati huo huo wa saa za kazi!?

Wazo hilo lililoletwa na serikali ya CCM lilipingwa vikali na wabunge wote wa upinzani na hoja yao kuu ni kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa hiyo wananchi hao waliowapigia kura na kwenda huko Bungeni wana haki ya kuwaona wabunge wao live wanavyochangia hoja mbalimbali humo bungeni ili wawatathmini na kujua ni wabunge wepi wanawawakilisha vyema bungeni na ni wabunge wepi wamekuwa wa ndiyo ndiyo humo Bungeni.

Wabunge wa CCM kwa hiyo wakaunga mkono hoja ya Bunge kutoonyeshwa live, kwa hiyo hoja ya serikali ya kutoonyeshwa Bunge live ikapita na wananchi wakaanza kunyimwa haki yao ya kuwaona wawakilishi wao wakitoa michango yao live Bungeni.

Baada ya Bunge kuanza kufanya shughuli zao gizani tukaanza kuona mfululizo wa wabunge wa upinzani kutimuliwa Bungeni kwa kile kinachodaiwa kuwa wabunge hao ni wavunjaji wakubwa wa kanuni za Bunge.

Hata hivyo katika tukio la hivi karibuni la kutimuluwa kwa wabunge wa upinzani Halima Mdee na Esther Bulaya, wananchi tumebaini kuwa wabunge hao wametimuliwa Bungeni kwa uonevu mkubwa kutohudhuria Bunge hilo kwa mwaka mzima kwa kilichodaiwa kuwa wabunge hao walitenda utovu wa nidhamu humo Bungeni.

Hata hivyo ukweli ni kuwa wabunge hao walionewa kwa kuwa chanzo cha wabunge hao kutimuliwa kilitokana na Mbunge mmoja wa CCM ambaye alifahamika kuwa ni Shonza ambaye aliwasha mic na kumuita Mnyika mwizi na Mnyika alipoomba mwongozo kwa Spika Ndugai kutaka mbunge aliyewasha mic na kumuita yeye mwizi afute kauli yake au athibitishe wizi wake, Spika Ndugai alimkingia kifua mbunge mwenzake wa CCM ambaye alimwita Mnyika mwizi na pale Mbunge Mnyika alipokuwa akisisitiza ni muhimu mbunge huyo wa CCM aidha afute kauli yake au athibitishe kauli yake, ndipo Spika Ndugai alipoita askari wa Bunge na kumtoa Mbunge Mnyika kama kibaka!

Baadaye Kamati ya maadili ya Bunge ambayo ina wabunge wa CCM watupu ikawajadili wabunge wa upinzani Halima Mdee na Esther Bulaya na kutoa uamuzi wa kuwafungia wabunge hao kutohudhuria vikao vya Bunge hadi mwakani!

Hatua hiyo ya uhasama ya wabunge imefikia hatua mbaya hadi wabunge wa upinzani wakasusia futari iliyokuwa imeandaliwa kwa wabunge wote na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Vile vile kulikiwa na Muungano wa wabunge wa vikundi mbalimbali vya kijamii vya wabunge wa CCM na wapinzani ambavyo vimeanza kuvunjika kimoja baada ya kingine.

Tukija kwenye mhimili wa utawala huku nako kumekuwa na ubaguzi wa wazi, hususani kwenye teuzi mbalimbali za utumishi wa Umma ambapo watumishi hao hawatakiwi kufungamana na siasa lakini tumeshuhudia katika teuzi za maDC, maRC na maDED Rais wetu akiteua kwenye nafasi hizo makada watupu wa CCM, ambapo wale waliopangiwa kwenye vituo vya kazi ambavyo vina wabunge kutoka upinzani, wabunge hao wamekuwa wakifanya majukumu yao katika mazingira magumu sana hasa kutokana na madaraka waliiyo nayo hao wateule wa Rais maDC na maRC kuwa na mamlaka ya kuwaweka watu ndani kwa saa 'zao' 48 pale waanapojisikia tu kuwaweka ndani watu hao walioko kwenye maeneo hayo.

Tumeshuhudia kwa kutumia sheria hiyo Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akisota rumande kwa miezi 4 mfululizo kwa tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi.

Tumeshuhudia pia majuzi Mbunge wa Kawe akiwekwa ndani kwa maelekezo ya DC wa Kinondoni kwa kile pia kinachodaiwa kuwa alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa nchi yetu.

Kwa mazingira hayo ingawa nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Ibara ya 3(1) lakini kiuhalisia wabunge wa upande wa upinzani wanakuwa treated kama wahaini!

Kwa Bahati mbaya sheria hiyo inakinzana hata na natural justice, kwa kuwa maDC na maRC hao wanakuwa ndiyo walalamikaji, ndiyo Polisi wanaopeleleza kesi hizo na wakati huo hup mahakimu wa kuwahukumu watuhumiwa wao!

Kauli mbalimbali zinazotolewa na Mkuu wetu wa nchi nazo zinazidi kumomonyoa misingi ya Umoja wa Taifa letu.

Nitanukuu baadhi ya kauli hizo. Wakati anapokea ripoti ya makinikia Rais wetu alinukuliwa akimpongeza Spika Ndugai kwa kazi 'nzuri' ya kuwatimua wabunge wa upinzani Bungeni na yeye akamhakikishia kuwa baada ya Spika huyo kukamilisha 'assigment' ya kuwatimua wabunge wa upinzani bungeni naye huku 'uraiani' atatumia Uamiri Jeshi wake mkuu kuwashughulika wabunge hao wa upinzani!

Inaonekana tukio la 'kushughulikiwa' kwa Halima Mdee kama ni kutimia kwa ahadi aliyoitoa Mkulu kuwa huku nje nako watashughulikiwa!

Vile vile tuliwahi kumsikia Mkuu wa nchi siku za nyuma akimkingia kifua RC wa Dar na kumwambia chapa kazi kijana, licha ya tuhuma lukuki zinazomkabili RC huyo, zikiwemo za kufoji vyeti na kuvamia studio za Clouds akiwa na askari wenye silaha na kuwatishia watangazaji wa kituo hicho kuwa wasipoonyesha clip yake ya Askofu Gwajima atawabambikia kesi ya uuzaji wa madawa ya kilevya!

Kwa Maelezo hayo niliyoyatoa ni dhahiri sasa kuwa Umoja wa Taifa letu upo shakani kwa kuwa nchi yetu kwa hivi sasa imegawanyika katika misingi hususani ya itikadi za kisiasa katika hatua ambayo inaweza kuhatarisha urithi wa Umoja wa kitaifa ambao tuliachiwa na baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere.

Lakini pia tukumbuke kuwa Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa kipindi kirefu sana, kwa hiyo tujifunze na nchi zinazotuzunguuka ambazo zilipoteza Umoja wa kitaifa nchini mwao na amani ikatoweka moja kwa moja nchini mwao.

Vile vile tujikumbushe maneno ya hekima aliyokuwa akiyatamka Mwalimu Nyerere kuwa amani ya nchi haishushwi toka mbinguni, Bali inatengenezewa mazingira ya kudumishwa kwenye nchi husika.

Kwa kuwa tayari kuna viashiria vingi vya kuvunjika Umoja wetu wa kitaifa ambao tumeudumisha kwa miaka mingi sana, naamini ni wajibu wa kila mwananchi , kutumia haki yake ya kikatiba kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) ya kutoa maoni kwa kukemea na kupaza sauti kwa nguvu zetu zote ili dalili hizi zinazojitokeza kwa Taifa letu za kuvunjika kwa Umoja wetu kutokana na itikadi zetu za kisiasa tuziepuke ili kuliepusha Taifa letu lisiingie kwenye hatari kama ambavyo mataifa mengine yalitumbukia kwenye machafuko na yakashindwa kurejea kwenye amani.

Wananchi pia tukumbuke kuwa hili ndilo Taifa letu na hatuna Taifa lingine lolote tunaloweza kukimbilia iwapo yatatokea machafuko nchini mwetu na njia pekee ya kudumisha amani ya kudumu mwetu ni kwa watawala wetu kuhakikisha kuwa wanatenda haki kwa makundi yote ya kijamii bila kufanya ubaguzi wa aina yoyote.
 
Serikali yenu ya chuki. Kama wewe ndo unawakilisha hoja za wakuu wako kuna tatizo mahali
Mkuu hao ni wale propagandists wanaotambulika kwa jina la Lumumba buku 7 team....
 
Mnaomlaumu Ndugai mnamwonea kabisa, ameagizwa kufanya hivyo na hata pa kutokea. Mbaya zaidi ni pale tunapoanza ubaguzi wa ukabila, kiasi kwamba mkuu wa nchi anaweza kuhutubia umati wa watanzania kwa kisukuma ni hatari sana, maana hili halijawahi kutokea katika nchi.
Kama kweli Ndugai ndiye anyeagizwa basi Inabidi atumie ule msemo unaosema kuwa 'za kuambiwa changanya na za kwako'

Kwa kuwa mbegu ya ubaguzi wanayoipanda hapa nchini itakuja kuliangamiza Taifa letu siku za baadaye.
 
Hizo za kuchanganya atazitoa wapi wakati ameshamezwa mzimamzima?
 
Mnaomlaumu Ndugai mnamwonea kabisa, ameagizwa kufanya hivyo na hata pa kutokea. Mbaya zaidi ni pale tunapoanza ubaguzi wa ukabila, kiasi kwamba mkuu wa nchi anaweza kuhutubia umati wa watanzania kwa kisukuma ni hatari sana, maana hili halijawahi kutokea katika nchi.
Ndigai ni mkuu wa muhimili wa nchi unaojitegemea.

Usiwe apologist wake kama vile ni mtoto asiye na nguvu yoyote.

Sent from my Kimulimuli
 
Hizo za kuchanganya atazitoa wapi wakati ameshamezwa mzimamzima?
Hahaahaaahaaa

Kwa hiyo unachosema ni kuwa mzee wa 'bakora' amemezwa na ule mhimili ambao huwa unatamba kuwa eti wenyewe ndiyo umejichimbia zaidi chini?
 
Moja ya misingi muhimu kabisa kwa Taifa lolote duniani ni Umoja wa kitaifa wa Taifa hilo.

Muasisi wa Taifa hili Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alituachia urithi muhimu sana kwa Taifa letu ambao ni kuwa na Umoja, ambapo nchi yetu haikuwa na ubaguzi wa kikabila, Imani za dini au itikadi za kisiasa.

Kwa bahati mbaya, kwenye serikali hii ya CCM ya awamu ya 5 kumekuwa na viashiria vya mmonyoko mkubwa unaohatarisha msingi huo wa Umoja wetu wa nchi kitaifa kutokana na nchi kuendeshwa kwa kubaguana kutokana na itikadi za kisiasa.

Kwa Bahati mbaya vinara wa kubagua wananchi kwa itikadi za kisiasa imekuwa ni mihimili 2 ambayo ni Bunge chini ya Spika Ndugai na mhimili mwingine ni utawala ambapo unaongozwa na Mkuu wa nchi mwenyewe.

Hebu nianzie na mmonyoko wa Umoja wa kitaifa unaofanywa na Spika wa Bunge letu pamoja na wabunge wa CCM ambao ndiyo walio wengi Bungeni.

Moja ya jukumu lake la msingi la Bunge lolote ni kuisimamia serikali iliyoko madarakani kwa niaba ya wananchi waliowachagua kwa kuikosoa kwa yale mambo ambayo serikali hiyo haiwafanyii vyema wananchi wake.

Kwenye Bunge letu ambalo lina makundi mawili, kundi la wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ndiyo wengi na wabunge wenzao wa upinzani ambao ni wachache ambapo mara nyingi imeonekana kuwa wabunge wa upinzani ndiyo wamekuwa wakitekeleza kikamilifu wajibu wao mkuu wa kuisimamia serikali, huku wabunge wenzao wa chama tawala cha CCM wakiamini kuwa wajibu wao mkuu wakiwa Bungeni humo ni kuikingia kifua serikali yao iliyoko madarakani

Kutokana na kukinzana kwa fikra hizo kumekuwa na mitafaruku isiyokwisha Bungeni humo.

Nitatoa mifano michache kuonyesha namna gani wabunge wa upinzani wamekuwa wakitimiza jukumu lao la kuisimamia serikali na wenzao wa CCM wamekuwa wskiikingia kifua serikali yao ya CCM.

Tuanzie na Bunge kuonyeshwa live. Siku za nyuma tokea nchi yetu iingie kwenye mfumo wa vyama vingi Bunge letu limekuwa likionyeshwa live, lakini mara tu serikali ya awamu ya 5 ilipoingia madarakani ikapeleka hoja Bungeni la kusitisha Bunge kionyeshwa live na sababu kuu iliyotolewa ni kuwa muda huo ambapo Bunge linaonyeshwa live ni muda ambao wananchi walio wengi wanakuwa makazini kwa hiyo wanatakiwa wakati huo wachape kazi badala ya wakati huo kuwa kwenye luninga zao kuangalia Bunge live.

Hata hivyo hoja hiyo ya serikali imedhibitika kuwa ilikuwa ya uongo kwa kuwa tumeshuhudia media mbalimbali nchini zikifanya live coverage kwa matukio ya Mwenyekiti wa CCM Taifa anapofanya ziara mbalimbali nchini ambapo katika ziara hizo zinakuwa '2 in 1' kwa maana zinakuwa za kiserikali na pia za kichama.

Sasa kama hoja ilikuwa Bunge halionyeshwi live ili watu wafanye kazi badala ya kuangalia luninga, mbona kwenye hizi ziara za Mwenyekiti wa Taifa CCM vyombo vya media vinatoa live coverage wakati huo huo wa saa za kazi!?

Wazo hilo lililoletwa na serikali ya CCM lilipingwa vikali na wabunge wote wa upinzani na hoja yao kuu ni kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa hiyo wananchi hao waliowapigia kura na kwenda huko Bungeni wana haki ya kuwaona wabunge wao live wanavyochangia hoja mbalimbali humo bungeni ili wawatathmini na kujua ni wabunge wepi wanawawakilisha vyema bungeni na ni wabunge wepi wamekuwa wa ndiyo ndiyo humo Bungeni.

Wabunge wa CCM kwa hiyo wakaunga mkono hoja ya Bunge kutoonyeshwa live, kwa hiyo hoja ya serikali ya kutoonyeshwa Bunge live ikapita na wananchi wakaanza kunyimwa haki yao ya kuwaona wawakilishi wao wakitoa michango yao live Bungeni.

Baada ya Bunge kuanza kufanya shughuli zao gizani tukaanza kuona mfululizo wa wabunge wa upinzani kutimuliwa Bungeni kwa kile kinachodaiwa kuwa wabunge hao ni wavunjaji wakubwa wa kanuni za Bunge.

Hata hivyo katika tukio la hivi karibuni la kutimuluwa kwa wabunge wa upinzani Halima Mdee na Esther Bulaya, wananchi tumebaini kuwa wabunge hao wametimuliwa Bungeni kwa uonevu mkubwa kutohudhuria Bunge hilo kwa mwaka mzima kwa kilichodaiwa kuwa wabunge hao walitenda utovu wa nidhamu humo Bungeni.

Hata hivyo ukweli ni kuwa wabunge hao walionewa kwa kuwa chanzo cha wabunge hao kutimuliwa kilitokana na Mbunge mmoja wa CCM ambaye alifahamika kuwa ni Shonza ambaye aliwasha mic na kumuita Mnyika mwizi na Mnyika alipoomba mwongozo kwa Spika Ndugai kutaka mbunge aliyewasha mic na kumuita yeye mwizi afute kauli yake au athibitishe wizi wake, Spika Ndugai alimkingia kifua mbunge mwenzake wa CCM ambaye alimwita Mnyika mwizi na pale Mbunge Mnyika alipokuwa akisisitiza ni muhimu mbunge huyo wa CCM aidha afute kauli yake au athibitishe kauli yake, ndipo Spika Ndugai alipoita askari wa Bunge na kumtoa Mbunge Mnyika kama kibaka!

Baadaye Kamati ya maadili ya Bunge ambayo ina wabunge wa CCM watupu ikawajadili wabunge wa upinzani Halima Mdee na Esther Bulaya na kutoa uamuzi wa kuwafungia wabunge hao kutohudhuria vikao vya Bunge hadi mwakani!

Hatua hiyo ya uhasama ya wabunge imefikia hatua mbaya hadi wabunge wa upinzani wakasusia futari iliyokuwa imeandaliwa kwa wabunge wote na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Vile vile kulikiwa na Muungano wa wabunge wa vikundi mbalimbali vya kijamii vya wabunge wa CCM na wapinzani ambavyo vimeanza kuvunjika kimoja baada ya kingine.

Tukija kwenye mhimili wa utawala huku nako kumekuwa na ubaguzi wa wazi, hususani kwenye teuzi mbalimbali za utumishi wa Umma ambapo watumishi hao hawatakiwi kufungamana na siasa lakini tumeshuhudia katika teuzi za maDC, maRC na maDED Rais wetu akiteua kwenye nafasi hizo makada watupu wa CCM, ambapo wale waliopangiwa kwenye vituo vya kazi ambavyo vina wabunge kutoka upinzani, wabunge hao wamekuwa wakifanya majukumu yao katika mazingira magumu sana hasa kutokana na madaraka waliiyo nayo hao wateule wa Rais maDC na maRC kuwa na mamlaka ya kuwaweka watu ndani kwa saa 'zao' 48 pale waanapojisikia tu kuwaweka ndani watu hao walioko kwenye maeneo hayo.

Tumeshuhudia kwa kutumia sheria hiyo Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akisota rumande kwa miezi 4 mfululizo kwa tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi.

Tumeshuhudia pia majuzi Mbunge wa Kawe akiwekwa ndani kwa maelekezo ya DC wa Kinondoni kwa kile pia kinachodaiwa kuwa alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa nchi yetu.

Kwa mazingira hayo ingawa nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Ibara ya 3(1) lakini kiuhalisia wabunge wa upande wa upinzani wanakuwa treated kama wahaini!

Kwa Bahati mbaya sheria hiyo inakinzana hata na natural justice, kwa kuwa maDC na maRC hao wanakuwa ndiyo walalamikaji, ndiyo Polisi wanaopeleleza kesi hizo na wakati huo hup mahakimu wa kuwahukumu watuhumiwa wao!

Kauli mbalimbali zinazotolewa na Mkuu wetu wa nchi nazo zinazidi kumomonyoa misingi ya Umoja wa Taifa letu.

Nitanukuu baadhi ya kauli hizo. Wakati anapokea ripoti ya makinikia Rais wetu alinukuliwa akimpongeza Spika Ndugai kwa kazi 'nzuri' ya kuwatimua wabunge wa upinzani Bungeni na yeye akamhakikishia kuwa baada ya Spika huyo kukamilisha 'assigment' ya kuwatimua wabunge wa upinzani bungeni naye huku 'uraiani' atatumia Uamiri Jeshi wake mkuu kuwashughulika wabunge hao wa upinzani!

Inaonekana tukio la 'kushughulikiwa' kwa Halima Mdee kama ni kutimia kwa ahadi aliyoitoa Mkulu kuwa huku nje nako watashughulikiwa!

Vile vile tuliwahi kumsikia Mkuu wa nchi siku za nyuma akimkingia kifua RC wa Dar na kumwambia chapa kazi kijana, licha ya tuhuma lukuki zinazomkabili RC huyo, zikiwemo za kufoji vyeti na kuvamia studio za Clouds akiwa na askari wenye silaha na kuwatishia watangazaji wa kituo hicho kuwa wasipoonyesha clip yake ya Askofu Gwajima atawabambikia kesi ya uuzaji wa madawa ya kilevya!

Kwa Maelezo hayo niliyoyatoa ni dhahiri sasa kuwa Umoja wa Taifa letu upo shakani kwa kuwa nchi yetu kwa hivi sasa imegawanyika katika misingi hususani ya itikadi za kisiasa katika hatua ambayo inaweza kuhatarisha urithi wa Umoja wa kitaifa ambao tuliachiwa na baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere.

Lakini pia tukumbuke kuwa Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa kipindi kirefu sana, kwa hiyo tujifunze na nchi zinazotuzunguuka ambazo zilipoteza Umoja wa kitaifa nchini mwao na amani ikatoweka moja kwa moja nchini mwao.

Vile vile tujikumbushe maneno ya hekima aliyokuwa akiyatamka Mwalimu Nyerere kuwa amani ya nchi haishushwi toka mbinguni, Bali inatengenezewa mazingira ya kudumishwa kwenye nchi husika.

Kwa kuwa tayari kuna viashiria vingi vya kuvunjika Umoja wetu wa kitaifa ambao tumeudumisha kwa miaka mingi sana, naamini ni wajibu wa kila mwananchi , kutumia haki yake ya kikatiba kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) ya kutoa maoni kwa kukemea na kupaza sauti kwa nguvu zetu zote ili dalili hizi zinazojitokeza kwa Taifa letu za kuvunjika kwa Umoja wetu kutokana na itikadi zetu za kisiasa tuziepuke ili kuliepusha Taifa letu lisiingie kwenye hatari kama ambavyo mataifa mengine yalitumbukia kwenye machafuko na yakashindwa kurejea kwenye amani.

Wananchi pia tukumbuke kuwa hili ndilo Taifa letu na hatuna Taifa lingine lolote tunaloweza kukimbilia iwapo yatatokea machafuko nchini mwetu na njia pekee ya kudumisha amani ya kudumu mwetu ni kwa watawala wetu kuhakikisha kuwa wanatenda haki kwa makundi yote ya kijamii bila kufanya ubaguzi wa aina yoyote.
Mystery,
Hapakuwa na msingi wa umoja.

Naweza kukuwekea ushahidi mwingi tu ikiwa utapenda tena kutoka
katika jamii kubwa ya Watanzania ambao walibaguliwa katika wakati
wake na hadi leo tatizo bado halijaondoka.
 
Sikutegemea kabisa hata siku moja kuona chuki za kutisha kiasi hiki ndani ya nchi yetu ambazo zinazidi kukithiri kila kukicha. Nilidhani nchi yetu itaendelea kuwa ile ya hekima, umoja na amani na mshikamano mkubwa miongoni mwa Watanzania bila kujali dini zetu, itikadi, rangi na makabila yetu.

Naisikitikia sana Tanzania yetu hasa siku za usoni naliona giza nene likizidi kutanda na kuwapa hofu kubwa Watanzania walio wengi sana. Matukio ya kutisha ya akina Ben Saanane, Roma Mkatoliki na wenzie yatazidi kukithiri kisa tu ni uroho wa kung'ang'ania madarakani.

Mungu inusuru nchi yetu na uipushe na janga kubwa sana lililopo mbele yetu.
Walioiharibu wanasema wanainyoosha!
(kwa stail ya kupandikiza chuki)
 
Walioiharibu wanasema wanainyoosha!
(kwa stail ya kupandikiza chuki)
Kauli hiyo siyo nzuri na inamomonyoa Umoja wetu kwa kisingizio kuwa Mkuu anainyoosha nchi!
 
Mystery,
Hapakuwa na msingi wa umoja.

Naweza kukuwekea ushahidi mwingi tu ikiwa utapenda tena kutoka
katika jamii kubwa ya Watanzania ambao walibaguliwa katika wakati
wake na hadi leo tatizo bado halijaondoka.
Weka ushahidi Mkuu
 
Back
Top Bottom